CyberTz
New Member
- Jun 14, 2024
- 2
- 2
Habari wanajukwaa.
Kuna changamoto tunapitia katika uhakiki wavyeti vya kuzaliwa kupitia RITA.
Wengi tupo katika mchakato wa kuomba mkopo wa elimu ya juu lakini kikwazo kimekuwa kwa RITA.
Mimi binafsi nina wiki ya 2 sasa kuelekea ya 3 cheti hakijahakikiwa na nimeshalipia.
Mbaya zaidi hata namba waliyoweka ya huduma kwa wateja yaani Toll Free ile namba ipo kama pambo kwa sabbau ukipiga kweli inaita na kutoa maelezo ya ukaribisho lakini wakati wa kusubiri uunganishwe na mtoa huduma inakata katika sekunde ya 28. Mara ya kwanza nilijua labda ni tatizo la mtandao lakini nimefatilia nimekuja kugundua ndivyo ilivyo maana hata wengine wamekuwa wakilalamikia tatizo hilo hilo.
Tatizo lilipo zaidi kwa kuwa hakuna sehemu tunaweza kuwapata kwa mfumo wa mawasiliano ili watolee ufafanuzi wa swala hili na wako kimya, account zote za social media hawapokei sms utaisgia ku-comment tu na atakwambia andika control number yako lakini nothing is solved. Sasa kama unatatua tatizo kwa kuomba control number ya kila mmoja utatua mara ngapi badala ya kutafuta tatizo lilipo kama ni kwenye mfumo au watendaji kazi ulitatue.
Pia soma: Madai ya kuchelewesha Vyeti, RITA yasema imepokea maombi 143,157, yaliyofanyiwa kazi ni 61.2%
Hii inatuathiri sisi sana kwa sababu dirisha la kuomba mkopo liko wazi lakini cheti hakiko verified maana yake wanatukwamisha kuendelea na maombi huku muda nao unazidi kuyoyoma.
Pia kuna shida hata katika watu wanaoomba vyeti vipya, uhakiki wa vyeti vya kifo yaani kiujumla ni shida tu, wengine wamelipia huduma lakini mfumo unawaonesha bado hawajalipia.
Hizi taasisi za kiserikali huwa zinakwama wapi? Na wamekalia kuhamasisha kuwa tumalize shida zetu kidijitali wakati huduma ni mbovu namna hii.