KERO Tatizo katika uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi wanaoomba Mkopo na huduma za RITA kwa ujumla

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Habari! Kuna tatizo Gani linalochelewesha verification ya vyeti? Ni Karibu Mwezi mzima mmeshindwa kuhakiki vyeti vilivyotumwa kwenye mfumo. Changamoto ni nini?
 
Pale RITA kuna upigaji
Rafiki yangu alitaka nakala ya cheti cha kuzaliwa. Alisumbuliwa na majibu ya kipumbavu mpaka alipotoa shilingi 10,000 mara moja cheti kikatolewa
 
Waende katika mfumo wa digital, kuna mabenki yanapigwa kwa kuwa Rita hawana mfumo kama wa ofisi za ardhi ku-verify documents za ndoa
 
Wanatengeneza mazingira ya rushwa

Ova
 
Mkuu ukiongea nao vizuri (🏧) Ndani ya nusu saa cheti kiko mkononi
 
Habari! Kuna tatizo Gani linalochelewesha verification ya vyeti? Ni Karibu Mwezi mzima mmeshindwa kuhakiki vyeti vilivyotumwa kwenye mfumo. Changamoto ni nini?
Toa mlungula period
 
HII NI KERO
 
Rita makao makuu kuna rushwa kubwa sana inayotekelezwa kupitia mawakala ambao wanakaa sehemu ya maegesho ya magari mkabala na ilipokuwa Club Billicans. TAKUKURU kazi kwenu

Forgery of clinic cards, leaving certificates, and personal registration by the birth certificate online applicant is complex and jammed to reach the required credentials until you consult the false agents carrying backpack outside the vehicle parking compound.
 
Tatizo hilo ni la kutokea june 2024 hakuna hatua zozote zinachukuliwa na waombaji wanashindwa kuendelea kufanya maombi ya Elimu ya Juu hasa kwa Tanzania Bara.

Visiwani wanaweka tu barua na wanaendelea safi kabisa

Je hii ni mbinu ya kupunguza kuondoa wanufaikaji wa mikopo maana watu wamekwama hapo na hakuna hatua za kueleweka zinachukuliwa na muda wa kufunga dirisha la maombi ni August 31?

Soma Pia: RITA wanalipisha kupata verification code, kwanini wasitengeneze vyeti kama NECTA then wakaweka zile code kama namba ya cheti kama ilivyo namba NECTA

JamiiForum fuateni hii ishu wanafunzi wanaotarajia kuendelea na elimu wamekwama
 
hadi na kadi ya chama
 
Kama uko Dar kaverify pale pale RITA makao makuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…