wegman
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 1,468
- 2,090
Wakuu kwema humu? Bila shaka jitihada za kupambana na maisha zinaendelea vizuri tukiwa tunasubiri kusherehekea sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya naomba niwatakie sikukuu njema mapema wakuu, Nirudi kwenye mada moja kwa moja ambayo ndio haswa imenileta niandike hapa jukwaani, Gari yangu Toyota Cami baada ya kupata mzinga mfumo wake wa AC sijui imekuaje ni kwamba sasa hivi ukiwasha AC inakuwa inapoza vizuri lakini tatizo moja ni kuwa inakuwa inatoa harufu ya petrol fulani hivi hapa tatizo linaweza kuwa ni nini? kabla ya kupata mzinga gari ilikuwa haina shida kama hii? Bila shaka humu tuna mafundi wengi naombeni munijuze tatizo linaweza kuwa ni nini.