TATIZO LA AFYA

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,164
Reaction score
1,293
Habari wakuu wangu,
Najua humu kuna wataalam na wenye uzoefu mbali mbali na changamoto za afya. Naomba msaada juu ya shida hapa chini.
Mimi ni ME umri wa arround 33 nani mtumishi wa umma.
Changamoto yangu ni kila ninapopata taarifa mpya au safari basi naumwa kabisa.
Mfano mtu anambie kesho tutasafiri kwenda mkoa, basi nikilala lazima usiku usingizi utakata, ntaanza kuiwazia hiyo safari na asbh nikiamka kichwa kitauma, ntatapika na nakua mgonjwa kabisa nikiweka kitu mdomoni natapika.
Nikipata taarifa kuwa kesho kuna wakaguzi au ratiba mpya nje ya utaratibu wangu wa kawaida hiyo hali inanitokea.
Yani mf nikiwa na wife na kesho yake awe anasafiri basi kuna hali najisikia naumwa kabisa.
Kifupi mazingira mapya, ratiba mpya kwangu ni changamoto hivyo baadhi ya safari huwa nazikataa mpaka watu wananishangaa.
Nikiwa kwenye ratiba zangu za kawaida am very strong ila ilukinibadilishia tu naumwa.
Naombeni ushauri tiba gani nitumie au nani ana utaalam na changamoto kama hii?
Nawasilisha
 
Pole sana, ndio maumbile, juzi tulitoka mombasa hadi pemba kwa mashua, mvua njia yote hata kusikia vibaya hatuku sikia mimi na watoto wangu. Mungu ana maajabu yake. Usiku mzima siku lala nawaza safari tu napanga nikipangua. Jambo dogo tu lanikosesha usingizi.

Anyway kuna kidonge unaweka chini ya ulimi husaidia katika mambo haya lakini side effect yake ni kisunzi sana. Bora utafute dawa mbadala kama kula lozi wakati wa kulala.

Pia jaribu kupigana na mawazo ya safari chukulia kama ni kwenda kazini kwa daladala.
 
Hicho kidonge kinaitwaje bos niki google,nitajitahidi kukielewa kwanza kabla sijakitumia so ntajie jina tu
 
Inaitwa kwells
Nimeisoma vyema, hii ni kutibu motion sickness yani ile hali mbaya unayojisikia gari ikitembea.
Hii ni tofauti na ishu yangu, mi najisikia vibaya kabla hata sijaanza safari. Ni mood disturbances na ni kama nakua na shauku au tension ya kijacho.
Ninapopata tu taarifa ya jambo jipya hapo hapo hali inabadilika hata sielewi ni ishu gani hii kuna muda nakata tamaa kabisa
 
Mkuu nikuongezee swali, vipi ukiwa na promise na demu mpya, hali inakuwa kama kawa?
 
Umri unavyozidi kwenda juu hali hiyo itapotea yenyewe! Umri wako bado hujakomaa.
Mimi wakati na umri kama wako, mtu akinipangia nikasimame mbele ya hadhara kikwapa hutoka jasho sana, siku hizi hakuna.
Hata nikiwa na safari kesho yake usingizi unakuwa wa mang'amung'amu siku hizi imepotea,nina 43yrs.
 
Fanya sana mazoezi ya viungo pia pendelea kufanya yoga exercises itasaidia.....punguza vinywaji vyenye caffeine. Mm nina umri kama wako nilikua napata shida kama yako hasa kuzungumza mbele ya kadamnasi. Lakin siku hz niko poa.
 
Fanya sana mazoezi ya viungo pia pendelea kufanya yoga exercises itasaidia.....punguza vinywaji vyenye caffeine. Mm nina umri kama wako nilikua napata shida kama yako hasa kuzungumza mbele ya kadamnasi. Lakin siku hz niko poa.
Yoga exercises ndo zinafanywaje boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…