Tatizo la Ajali za Barabarani Litatumaliza Watanzania. Je, Kweli Serikali Haiwezi Kufanya Kitu?

Tatizo la Ajali za Barabarani Litatumaliza Watanzania. Je, Kweli Serikali Haiwezi Kufanya Kitu?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Tatizo la ajali za barabarani linazidi kuitafuna taifa la Tanzania na kuwaacha wananchi wakiwa kwenye misiba mizito ya wapendwa wao, pamoja na na simanzi zisizoisha, ni jambo hilo ndilo limenifanya nitakari kwa kina kuhusu ni nini haswa huwa kinawafanya waliokabidhiwa ofisi za umma kuwa na ukakasi linapokuja suala la maamuzi yanayohusu usalama na ustawi wa watanzania kwa ujumla.
images (30).jpeg

Kwa sasa Tanzania imekuwa ni jambo la kawaida kusikia taarifa za ajali huku baadhi tukishuhudia ajali nyingi za barabarani zikitokea katika maeneo kadha wa kadha ndani ya nchi, ajali baadhi zikihusisha vifo na majeraha ya maelfu ya watu katika kiwango ambacho, ninapata hofu kubwa sana. Kwa sasa mioyoni mwa watanzania tunaishi na dhana mbovu katika akili zetu kwamba ajali ni kitu cha kawaida sana, na hivyo kufanya viwango vya kujali miongoni mwetu ndani ya jamii kupungua kwa kiasi kikubwa.

Ni ajabu ila ndo uhalisia, kutokusikia tamko lolote au watu kujitathimini kuhusu ajali iliyotokea kule Mbeya Juni 5, 2024, na kupelekea vifo vya watanzania 16 na kuacha majeruhi wengine kadhaa, tukio hili limechukua nafasi ndogo sana kwenye mijadala ya Watanzania walio wengi haswa ukizingatia wengi wetu ni watu wa kupuuza, kwenye vijiwe vya kahawa, mitandao ya kijamii, ni kama vile hakuna kitu kilichotokea ndani ya ardhi ya Tanzania.
images (31).jpeg

Ajali hii, tumepata kuambiwa kuwa ilitokana na lori ambalo lililogonga gari nyingine mbili baada ya breki zake zote kufeli, ni ajali ambayo imetokea wiki chache tu baada ya ajali nyingine huko Kilwa, mkoani Lindi, ajali ambayo iliondoka na roho za watu 13 na kujeruhi wengine kadhaa hapo Aprili 22, 2024.

Hatufahamu ni wastani wa watu wangapi wanaporwa zawadi zao za uhai au kiwango cha ulemavu ambacho watu hupata wakiwa kwenye barabara zetu kila siku, na nimefanya jitihada za kutafuta takwimu na taarifa mtandaoni kuhusu hili nmetoka mtupu, lakini bila shaka yoyote, hii inatosha kuwa ni ishara zinazonesha kwamba hili ni tatizo kubwa sana ambalo kwa mtu mwene utimamu anaweza kuthutubu kusema linahitaji utatuzi wa haraka, ikibidi hata litangaziwe hali ya dharura na vyombo vya usalama.
images (32).jpeg

Fikiria, katika siku 12 tu ndani ya mwezi Disemba 2023, Tanzania ilipoteza watanzania 46, wastani wa watu wanne kila siku, kwenye ajali za barabarani. Kwa nini hii isiwe ni taarifa ya kupuuza? Ni kwamba RTO za mikoa hawaoni kinachoendelea, je ni kweli SACP Ramadhani Ng’azi ameshindwa kutoa maagizo kwa RTO na kuja na namna ya kuzuia hivi vifo?

Hiki ndio kitu ambacho kinanipeleka kwenye hoja yangu ya msingi, kwamba je, kama wananchi, tumerudhika na kinachoendelea haswa pale ambapo ajali zinatokea?
images (34).jpeg

Tumetosheka na kusema kuwa mapenzi ya Mungu yatimie kwa matatizo na ajali ambazo zinaepukika? Tumekosa imani kuhusu usalama wetu tunapokuwa barabarani kiasi kwamba hata taa zikiruhusu watembea kwa miguu kuvunja barabara basi bado utavuka kwa hofu, ukiogopa bodaboda asije kupita na roho yako?

Fikiria, kama wahalifu wangeingia barabarani na kuwaua watu 13 huko Lindi Aprili mwaka huu, kisha mwezi Mei wakaua watu saba Morogoro, halafu mapema mwezi Juni wakaua watu wengine 16. Je, tungebaki kwenye hali kama ya sasa inayoashiria kutokuwepo kwa utashi wa kufikiria njia za utatuzi wa kitu miongoni mwa wale waliokabidhiwa dhamana ya kulinda maisha na usalama wetu kama raia?
1000567633.jpg

Je sababu ya mwanadamu kupoteza maisha inaweza kuweka uzito katika kutoa maamuzi na ufutailiaji kiasi kwamba maafisa polisi waone kesi ipi inatakiwa ipewe kipaumbele kuliko kesi nyingine?

Je Basi X likipinduka na kuua watu 10, uchunguzi na utatuzi wa tukio hili ni sawa na wahalifu wakitoa roho za watu 10 pale Kihesa Kilolo Iringa? Je, udhaifu wa dereva wa basi X ukisababisha ajali na watu 10 wakapoteza maisha ni sawa na mtu mmoja aliyeingia Kariakoo na kupiga risasi na kuwaua watu 10?
images (39).jpeg

Ni mpaka mtu akutwe na mauti ya namna gani ndipo vyombo vya usalama vitaona uzito wake? Ni kifo kipi kinahuzunisha zaidi ya kingine? Kifo cha mtu ambaye amefariki kwa kunywa sumu ni sawa na kifo cha mtu ambaye amegongwa na lori akiwa anavuka kwenye zebra? Ni mazingira gani ya kifo ni ya kuogofya zaidi ya mengine?

Ni kweli Serikali inataka kutuaminisha kwamba hakuna kitu inaweza kufanya kuondokana na tatizo hili linalowajengea hofu Watanzania kuhusu kutumia usafiri wa barabara – usafiri unaotumiwa na mamilioni ya wananchi wa tabaka la chini na, kwa kiwango fulani, lile la kati? Je kuna mtu ambaye ana imani na vibao ambavyo vipo pembezoni ya barabara? Je, ni watanzania wangapi wana imani kuwa gari walilopanda breki zake zipo salama?
images (33).jpeg

Je mzazi ana uhakika kuwa mtoto wake akienda shule atarudi salama ikiwa kuna madereva wanaendesha magari kwa fujo kupindukia? Ni nani ambaye ana ujasiri wa kutembea kwenye barabara zetu akiwa na imani ya 100% kuwa gari lililopo nyuma yake linatembea kwa usalama?
images (36).jpeg

Mikakati bora ya serikali inaweza kusaidia uwajibishwaji wa askari wa usalama barabarani ambao wanakula rushwa pamoja na udhibiti wa vyombo vya usafiri vinavyoingia barabarani kuhakikisha ubora. Lakini, kwa nini Serikali kila siku inasema itaifanyia marekebisho sheria ya Usalama wa Barabara na mwisho wa siku hakuna marekebisho yoyote yanafanyika?
images (35).jpeg

Kwa nini Serikali, iliyojijengea sifa ya kupitisha sheria mbalimbali bungeni kwa hati ya dharura, licha ya kulalamikiwa na wadau, inahofia sana kuifanyia marekebisho Sheria ya Usalama Barabarani? Je, inawezekana sababu ikawa ni wamiliki wa mabasi na malori ya mikoani, ambao baadhi yao wanajulikana kuwa vigogo na wafadhili wakubwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Bila shaka serikali wanahisi sheria mpya itakinzana na maslahi yao binafsi ya kujitengenezea faida pana zaidi na nono kwa wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri. Ni wazi serikali kupitia wizara husika inafahamu kuwa kuna wamiliki wa vyombo vya usafiri ni viongozi wa CCM, ila je ni kweli maisha na ustawi wa viongozi wachache wa CCM ni bora kuliko maisha ya watanzania?
images (37).jpeg

Serikali, pamoja na Bunge, kwa nyakati tofauti tofauti wamekuwa wakali sana kuhusu madereva wa bodaboda nchini na ajali wanazozisababisha ambazo wamekuwa wakizihusisha na uendeshaji wao ulio wa hatari na usiofuata sheria. Sasa kwanini, hatuoni Serikali pamoja na Bunge, zikizungumza kwa hisia kali kuhusu ajali zinazosababishwa na mabasi ya abiria na malori ya mizigo ya mikoni?

Je, sababu inaweza kuwa ni vile hakuna kigogo wa CCM au viongozi wa waliopo serikalini ambao ni wamiliki wa bodaboda na hivyo ni rahisi kuwashambulia bodaboda kila siku na kwa hisia hasi muda mwingine?
images (38).jpeg

Nadhani ifike wakati Serikali iache kurusha mipira yote kwa boda boda kuendeleza visingizio na kuanza kubuni na kutekeleza hatua madhubuti zinazolenga kukomesha ajali za barabarani nchini. Kama watanzania hatuwezi kuendelea kuishi na kufanya mambo yetu kama vile suala la ajali za barabarani ni kama ni suala ambalo Mungu amepanga litokee, kwamba lazima litokee haijalishi hali iliyopo na binadamu hawezi kuzuia.

Ni wakati sahihi sasa kwa serikali kutazama kwa jicho la tatu vifo vya watanzania vinavyotokana na ajali zisizokwisha za barabarani na kujiuliza kama ingeendelea na mambo mengine kama kawaida endapo kama vifo hivyo vingetokana na matukio ya kigaidi, uhalifu au ajali za ndege, na kama jibu ni hapana, ianze kuchukua hatua stahiki sasa na sio kupuuza.
images (35).jpeg

Sehemu ya kuanzia ni kwa Serikali kutimiza ahadi yake ya kuifanyia marekebisho Sheria ya Usalama Barabarani, hatua itakayowezekana tu kwa Serikali kutoa kipaumbele kwa maisha ya Watanzania badala ya maslahi ya kifedha ya wamiliki wa mabasi na malori, pamoja na kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza mikakati mingine imara ya kutokomeza kabisa ajali za barabarani Tanzania. Huku elimu ikitolewa kwa watumiaji wa barabara mara kwa mara ili watu wafahamu wajibu na haki zao wakiwa barabarani.​
 
Wacha tukufe...... Kwani Dunia ni yetu. We traffic anaingia kwenye gari anauliza tu abiria Kuna changamoto yeyote .... Anashuka anazunguka anapewa chake imeisha hiyooo.....
Yaani hilo jambo sijawah kulielewa 😔 Anashindwa hata kukagua gari kama lina tatizo
 
Yaani hilo jambo sijawah kulielewa 😔 Anashindwa hata kukagua gari kama lina tatizo
Hata na sisi abiria kiasi flani ni viande.... Kuna siku tunatoka Dodoma kwenda iringa Kuna sehemu wanakaaga matrafiki bus ilijaa kinyama mpaka watu wamesimama ilikuwa kipindi Cha Christmas...Si wakashushwa nyumanyumaa hapo wakakodiwa bajaji tukawapakia mbele .... Asee tulikula mzinga yaani tulipiga pasi chwaaaaa...... Tungeanguka tungekufa wengi sana ila dereva alijitahidi kulielekezea machakani tukagonga mtu tukabaki hapo.
 
Back
Top Bottom