Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka

Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Duniani kote ajira ni changamoto, lakini namna ya kulishughulikia ndiyo tatizo zaidi hapa kwetu Tanzania.

Kwanza Serikali imekuwa chanzo kikubwa cha tatizo hili na kupelekea kutengeneza mpaka propaganda ili ionekane imeajiri.

Suala la Serikali kudai imeongeza kiasi cha ajira kinakifikirisha sana.

Sekta binafsi in Tanzania imekufa na chanzo ni Sera mbovu za serikali awamu ya tano.

Vijana wasomi wamekata upepo mpaka wanatamani kujiua ama kufanya chochote ilimradi apate mkate.

Duh ama kweli akunyimae kazi amekuvua utu wako.

Vijana endeleeni kubet na ligi zinaelekea ukingoni sijui mtaishije.
 
Unaposema sekta binafsi imekufa weka takwimu. Au shuleni ulifundishwa kulalama tu bila takwimu. Weka takwimu za 2015 vs 2020 tuone kweli sekta binafsi imekufa. Maana unaweza kuwa umekufa wewe (kifikra) ukadhani nchi yote imekufa.

Kuhusu suala la serikali kuajiri hili sijui wasomi wetu huwa mnalitoa wapi. Hivi ni wapi mnafundishwa kuwa serikali ina wajibu wa kuajiri kila mwaka?

Mnapaswa kuipongeza serikali hii kuwa pamoja na changamoto kubwa inazopitia bado haijawahi kufanya redundancy kama ilivyowahi kutokea miaka ya nyuma. Sasa badala yake kutwa mitandaoni kulalamika.

2607682_Screenshot_20201101-2117262.jpg
 
Binafsi naona kama Magufuli ataondoka Ikulu basi atamwachia Rais ajaye Zigo kubwa mnoo lisilobebeka.

Kibwengo 👿 ni Kivuruge. Kavuruga kila kitu.

Mfumo wa ajira kavuruga, tangu 2015 hakuna ajira za kueleweka, imagine after miaka 10.

Biashara zimekufa, nchi imejaa vibanda ( Hawa ni machinga wameruhusiwa wazagae ili wasiwasumbue watawala walaji )

Nchi kibao za Ulaya n.k mpaka sasa mahusiano yetu na wao siyo mazuri.

Zigo la Deni la Taifa ( imagine miaka 5 kakopa pesa kama ya Kikwete ya miaka 10 je, miaka 5 ijayo itakuwaje )

Kesi kesi, tumeshtakiwa ndani na nje ya nchi, watu wamefutwa kazi watashtaki.

Watumishi wa umma, kupandishwa madaraja na annual increments ambazo zipo kisheria watadai, yote yatamhusu Rais wa awamu ya 6.

Mamaaaa!!!!!

Kina Ben Saanane, Azory Gwanda Alphonce Mawazo, Tundu Lissu kupigwa risasi mchana kweupee watu watataka kujua hilo ni jipu!!!
Korosho za wana Mtwara, hapa alilichomeka Jeshi ili asihojiwe


Summing up,

Nchi ina watu milioni 60 lakini serikali yenyewe imeajiri watu Laki 5 tu Kati yao, ambao na wao pia imeshindwa kuwadumia.

Hao watu wengine kwa mamilioni wanaungaunga sana.

Yaani hii nchi tangu Kibwengo 👿 ameingia, kwanza kapiga PAUSE matatizo yote yaliyokuwepo aiyoyaacha Kikwete, rais ajae atayakuta.

Pili, kavuruga zaidi na hivyo kurudisha nyuma na kutengeneza rundo la matatizo mengine.
 
USITUTISHEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Nchi ina WATU milioni 60 lakini serikali yenyewe imeajiri watu Laki 5 kati ya hao milioni 60 ambao na watu hata kuwahudumia imeshindwa.

Sasa redundancy gani tena ifanye, labda ifute kabisa wasiwepo.

Tuwe na serikali isiyo na watumishi maana hao Laki 5 wameonekana mzigo mpaka serikali imeelemewa.
 
Dangote amefungasha virago, Ngurdoto hotel imekufa nk. Hii ndo maana halisi ya sector binafsi imekufa.
 
Acha ubishi we kiazi mbatatata, kampuni bila sekta binafsi imara hakuna ajira imara.
 
Hilo bomu kama humjui aliye na remote ya kulilipua basi fahamu halitokaa lilipuke miaka nenda rudi
 
Duniani kote ajira ni changamoto, lakini namna ya kulishughurikia ndiyo tatizo zaidi hapa kwetu Tanzania.

Kwanza Serikali imekuwa chanzo kikubwa cha tatizo hili na kupelekea kutengeneza mpaka propaganda ili ionekane imeajiri....
Mpaka leo mkuu wa chuo kikuu cha drs katoa neno
 
Unaposema sekta binafsi imekufa weka takwimu. Au shuleni ulifundishwa kulalama tu bila takwimu. Weka takwimu za 2015 vs 2020 tuone kweli sekta binafsi imekufa. Maana unaweza kuwa umekufa wewe (kifikra) ukadhani nchi yote imekufa...
Kazi ya serikali ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili ziweze kuajiri watu.

Sasa fatilia vizuri tangu serikali ya amamu ya tano imeingia, taasisi nyingi zipo taabani na zingine zimefungwa(taasisi za ujenzi nyingi zikefungwa coz serikali inatumia jeshi maeneo mengi, Fast jet na mashirika mengine ya ndege yamefungwa kwasababu figisu za serikali kuiinua ATCL)

Hiyo ni mifano michache sana, ni dhahiri serikali haiwezi kuepuka lawama juu ya hili.
 
Duniani kote ajira ni changamoto, lakini namna ya kulishughulikia ndiyo tatizo zaidi hapa kwetu Tanzania.

Kwanza Serikali imekuwa chanzo kikubwa cha tatizo hili na kupelekea kutengeneza mpaka propaganda ili ionekane imeajiri...
Umeandika kwa uchungu sana mkuu
 
Kukata tamaa sababu ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu ambalo litalipuka muda si mrefu kwa nchi nyingi za Kiafrika waache tu waendelee kulipana posho na kujengeana masanamu halafu vijana waambiwe wajiajiri. It's only a matter of time, the only thing left is the right trigger for this bomb to explode.

Kinachotokea South Africa ni mfano ukiwa huna kazi and there's no hope ya kuipata leo wala kesho any opportunity for a violence utaichukua.
 
Kukata tamaa sababu ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu ambalo litalipuka muda si mrefu kwa nchi nyingi za Kiafrika waache tu waendelee kulipana posho na kujengeana masanamu halafu vijana waambiwe wajiajiri. It's only a matter of time, the only thing left is the right trigger for this bomb to explode.

Kinachotokea South Africa ni mfano ukiwa huna kazi and there's no hope ya kuipata leo wala kesho any opportunity for a violence utaichukua.
Ni kweli kabisa,kwa ushauri wangu kwa serikali wangeaanza kuwaandaa vijana kwenye fani zao na kuwapa mikopo nafuu,mfano wa kilimo wawakopeshe matractor, wawape ardhi na pembejeo zingine,

wahasibu waaanzishie kampuni za uhasibu na mahesabu kwa ajili ya sekta binafsi,watu wa masoko waanzishe ofisi za masoko ili wahamasishe bidhaa zetu kwenye balozi zetu na serikali ipewe mrejesho mwisho wa mwaka.Hii itakuwa ajira tosha hata wengi hawatataka kusubiria ajira za serikalini.
 
Ni kweli kabisa,kwa ushauri wangu kwa serikali wangeaanza kuwaandaa vijana kwenye fani zao na kuwapa mikopo nafuu,mfano wa kilimo wawakopeshe matractor,wawape ardhi na pembejeo zingine,wahasibu waaanzishie kampuni za uhasibu na mahesabu kwa ajili ya sekta binafsi,watu wa masoko waanzishe ofisi za masoko ili wahamasishe bidhaa zetu kwenye balozi zetu na serikali ipewe mrejesho mwisho wa mwaka.Hii itakuwa ajira tosha hata wengi hawatataka kusubiria ajira za serikalini.
Serikali hii hii ya Mbogamboga iwafanyie hayo? Iache kuwakamua sh.100/100 zenu kwenye simu
 
Mim nilimaliza chuo 2015 hadi leo sijapata ajira naendesha bodaboda ya mjomba hapa ..
Maisha ni magumu degree hainisaidii
 
Back
Top Bottom