Binafsi naona kama Magufuli ataondoka Ikulu basi atamwachia Rais ajaye Zigo kubwa mnoo lisilobebeka.
Kibwengo πΏ ni Kivuruge. Kavuruga kila kitu.
Mfumo wa ajira kavuruga, tangu 2015 hakuna ajira za kueleweka, imagine after miaka 10.
Biashara zimekufa, nchi imejaa vibanda ( Hawa ni machinga wameruhusiwa wazagae ili wasiwasumbue watawala walaji )
Nchi kibao za Ulaya n.k mpaka sasa mahusiano yetu na wao siyo mazuri.
Zigo la Deni la Taifa ( imagine miaka 5 kakopa pesa kama ya Kikwete ya miaka 10 je, miaka 5 ijayo itakuwaje )
Kesi kesi, tumeshtakiwa ndani na nje ya nchi, watu wamefutwa kazi watashtaki.
Watumishi wa umma, kupandishwa madaraja na annual increments ambazo zipo kisheria watadai, yote yatamhusu Rais wa awamu ya 6.
Mamaaaa!!!!!
Kina Ben Saanane, Azory Gwanda Alphonce Mawazo, Tundu Lissu kupigwa risasi mchana kweupee watu watataka kujua hilo ni jipu!!!
Korosho za wana Mtwara, hapa alilichomeka Jeshi ili asihojiwe
Summing up,
Nchi ina watu milioni 60 lakini serikali yenyewe imeajiri watu Laki 5 tu Kati yao, ambao na wao pia imeshindwa kuwadumia.
Hao watu wengine kwa mamilioni wanaungaunga sana.
Yaani hii nchi tangu Kibwengo πΏ ameingia, kwanza kapiga PAUSE matatizo yote yaliyokuwepo aiyoyaacha Kikwete, rais ajae atayakuta.
Pili, kavuruga zaidi na hivyo kurudisha nyuma na kutengeneza rundo la matatizo mengine.