Stranger94
New Member
- Sep 11, 2022
- 2
- 0
UTANGULIZI
Tatizo la ajira limekua mtambuka duniani Kwa sasa, nchi nyingi duniani zimekua zikikutana na changamoto hii hususani katika kipindi hiki ambacho dunia inashuhudua anguko la uchumi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo athari za ugonjwa wa virusi vya Corona pamoja na vita vinavyoshudiwa mashariki mwa bara la ulaya kati ya Urusi na Ukraine. Kwa mujibu ya shirika la kazi duniani (ILO, 2022), takribani vijana milioni 73 sawa na asilimia 23.3 ya vijana duniani kote hawana ajira.Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania kama zilivyo nchi zingine duniani, imekua ikishuhudia changamoto ya ukosefu wa ajira haswa kwa vijana wanaohitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati. Hali hiyo imeanza kushuhudiwa kuanzia miaka ya 2010 hadi sasa.
CHANZO CHA TATIZO
Tatizo hili ni matokeo ya mambo yafuatayo;
Kuanzishwa kwa shule za sekondari kwa kila kata kuanzia mwaka 2005. Ulikua ni mpango mzuri wa serikali kumfanya kila mtanzania kuwa na angalau elimu ya kidato cha nne. Lengo limefikiwa kwa zaidi ya asilimia 90, changamoto ni kwamba serikali haikuandaa mpango wa kuwasaidia wasomi hao baada ya kuhitimu.
Mfumo wa elimu haumuandai mhitimu kujiajiri bali unamtengeza mwajiriwa. Rejea mfumo wa elimu ya kujitegemea wa awamu ya kwanza chini Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ulikua unawaandaa wahitimu kujiajiri na kuweza kuishi maisha hususani ya Vijijini lakini kwa sasa imekua tofauti kwani hata shule zilizokua za ufundi kama Ifunda, Moshi technical na zingine zimekua shule za kawaida siku hizi, lakini hata shule za kilimo kama Kilosa Sekondari nazo zimekua za kawaida. Hali hii ipo hadi kwenye elimu ya juu kwani hakuna kozi za kumuandaa mhitimu kujiajiri, kozi nyingi ni za nadharia ambazo kiuhalisia huwaandaa wahitimu kufanya kazi za ofisini.
Wahitimu kushindwa kukubaliana na hali halisi. Baadhi ya wahitimu bado hawajawa tayari kuupokea ukweli kwamba Tanzania kama taifa, haiwezi kuwaajiri wote kwenye sekta ya uma lakini pia hata sekta binafsi imeelemewa. Hivyo basi vijana wanapaswa kujiandaa kukabiliana na maisha nje ya kuajiriwa na sio kukaa nyumbani na kuwa mizigo kwa wazazi wakisingizia kusubiri ajira.
NINI KIFANYIKE
Ili kupunguza changamoto ya ajira nchini serikali pamoja na wananchi kwa ujumla wanapaswa kufanya yafuatayo;
Kubadilisha mfumo wa elimu kuanzia elimu ya msingi mpaka elimu ya juu: ili kuwezesha mfumo mpya utakaowezesha kupata wahitimu wenye elimu ya kujiajiri na kujitegemea kwa ujumla. Mfumo wa elimu wa sasa ni tata kuanzia kwenye lugha za kufundishia hadi kwenye maarifa yanayopatikana ndani yake. Hivyo basi ipo haja ya serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknolojia kukaa chini na wadau wa elimu na kutengeneza mfumo mpya wenye tija kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Serikali kupunguza kodi kwenye biashara ndogo ndogo ambazo nyingi zimeanzishwa na wahitimu ili kuwawezesha kukuza biashara zao. Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) pamoja na ofisi za Halmashauri zimekua na tabia ya kuwawekea kodi kubwa wafanyabiashara na wakati mwingine kuwafungia biashara zao. Hali hii inawavunja moyo na kuwarudisha nyuma vijana wengi. Hivyo basi serikali isaidie katika kuwafanya vijana wenye nia ya kufanya biashara halali kuanzisha na kukuza biashara zao bila ya bughudha yoyote ili kupunguza watu wasio na kazi mtaani.
Kupunguza kidogo umri wa kustaafu. Umri wa kustaafu kupunguzwa kidogo kutoka miaka 60 mpaka 55, hiyo itawezesha kupatikana kwa nafasi nyingi za kuajiri vijana waliohitimu kutoka kwenye vyuo mbalimbali na kupunguza changamoto ya ajira nchini. Hili litaongeza ufanisi wa kazi pia, kwani waajiriwa wengi umri umewatupa mkono hivyo basi kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi ule ule waliokua nao mwanzoni.
Serikali kuajiri kila mwaka kulingana na uhitaji. Kumekuwa na upungufu wa watoa huduma za afya pamoja na walimu kwenye baadhi ya maeneo nchini lakini bado serikali imekua ikisisitiza hakuna uhitaji huo, hii inatokana na ukweli kwamba viongozi wengi tuliowaamini na kuwapa dhamana ya kutuongoza wana utamaduni wa kutekeleza majukumu yao kwa kuongozwa na siasa badala ya weledi. Serikali imekua ikijenga shule na hospitali mpya kila siku lakini haiajiri vijana wapya kufanya kazi kwenye majengo hayo mapya hali inayopelekea elimu za wahitimu wengi kuishia mtaani bila kuzifanyia kazi.
HITIMISHO
Mwisho niwaombe wazazi na jamii kwa ujumla iendelee kuwatia moyo vijana wasio na ajira nchini ili kuepusha athari za magonjwa kama sonona ambao hupelekea msongo wa mawazo na unaweza kumfanya mtu kutoona umuhimu wa kuishi. Hivyo basi vijana wanapaswa kutambua kwamba zipo njia nyingine nyingi za halali tofauti na kuajiriwa zinazoweza kumfanya mtu aishi kwa kwa amani na furaha. Lakini pia vijana ambao wapo shuleni na vyuoni kwa sasa, wanapaswa kuondoa kabisa wazo la wao kuajiriwa baada ya kuhitimu, hiyo itawasaidia kuwa na amani ya moyo na kuondoa matarajio ambayo yanaweza kuwaletea athari baadae na kuishia kuilaumu serikali hali ya kuwa wakati wanaanza kusoma walishaliona hili tatizo.

Upvote
1