Tatizo la Clutch

benja

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
320
Reaction score
215
Wakuu habari za asubuhi

Mimi nna Starlet ambayo ni Manual Transimission. Gari iliisha clutch plate nikabadilisha. baada ya kubadilisha likarudi kwenye hali yake lakini gia zikawa zinaingia na kutoka kwa shida ila baada ya muda lile tatizo la clutch plate likarudi gari likawa linakosa nguvu.

Baadae nikashauriwa nibalidi Clutch Plate pamoja na Pressure Plate. Kweli nikabadili tena kwa mara yapili lakini baada ya kubadili bado naona gari inakosa nguvu tena kuliko ilivokuwa mara ya kwanza yaan ata ukitaka ku overtake inakuwa kazi kubwa sana au kupanda mlima gari haina nguvu. Je, hii ni tatizo la nini kwa sababu kama kubadili vyote nimebadilisha tena kwa gharama nyingi?

Naombeni msaada wakuu
 
Mtafute huyu jamaa JituMirabaMinne atatengeneza gari na utafurah kwasabb ni mtaalamu wa mambo ya gear box
Mkuu nashukuru. Japo mimi nahusika sana na masuala ya Automatic gearbox. Si mtaalamu wa manual.

Hiyo gari yake labda aseme akiwasha ikiwa silent akikanyaga accelerator mshale unafika ngapi? Labda naweza kuwa na cha kumsaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…