Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ukifuatilia waumini wa dini kubwa mbili za Ukristo na Uislamu utagundua huwa wanajikita au wanajielekeza katika mambo mepesi zaidi huku wakiwa hawatilii mkazo yale mazito ambayo yangeboresha maisha ya watu wanaowazunguka.
Mfano katika dini ya Ukristo kuna kitu kinaitwa Golden rule/ sheria ya dhaba inayosema "Watendee wengine vile ambavyo ungependa wewe kutendwa". Utakuta Wakristo wachache sana wanazingatia hii, ila wengi wao wamejikita kwenda kanisani, kutoa sadaka, wanasali kabla ya kula, kuvaa rozari na mambo mengine madogo madogo kama hayo.
Kwa upande wa uislamu nao kuna mambo mazuri yanayosisitiza utoaji haki kwa watu wote, kutoonea, kutodhulumu n.k lakini wengi wao wamejikita katika masuala mepesi ya kuswali mara nyingi kwa siku, kuvaa ushungi, kanzu, kutokula kitimoto n.k
Kama watu wa dini wangeyapa uzito mkubwa zaidi mambo yanayogusa binadamu wenzao wanaowazunguka hakika dunia ingekuwa sehemu iliyo bora zaidi na yenye furaha zaidi.