Tatizo la engine kukwaruza kwenye Boxer BM 150 namba B

Nimenunua kwa mtu ila nimeanza kusikia kamlio tofauti kwenye injini kama inakuwa inakwaruza pale unapoanza kuondoka. Je shida ni nini?

inakwaruzaje? Ni wakati tu wa kuondoka au?

Mpelekee fundi akague tyming chain, piston + block au clutch plates. Hivyo ndio huwa vinabadilisha mlio mara nyingi kwenye boxer engine.

Ushauri: boxer usikurupuke kununua kwa mtu labda uwe unaifaham historia yake, kwa muonekano boxer inaweza kuonekana ipo ktk hali nzuri ila mmiliki huenda hakuwa anaifanyia engine service vizuri hivyo unakuta kuna kifaa kilishakongoloka humo lkn yeye akawa anaitembelea tu hivyohivyo, sasa ukikurupuka ukanunua kwa kuangalia muonekano wa nje basi unaumia.
 
Nilinunua Boxer last year kwa mtu ilikuwa ukiweka gear namba 3 inakwaruza..

Fundi wangu wa mtaani akaniambia hapa no way out tununue gear box nyingine tu..

Hivyo mkuu inawezekana hiyo shida ikawa hakuna namna zaidi ya hiyo ya kubadilisha gear box..

Kwa msaada zaidi ipeleke kwa fundi aikague physically.

Note: Yangu nilimpa dogo maana sikuwa naona umuhimu wake tena licha ya kubadilisha gear box nilimpa kijana alete hesabu lakini tulikuwa tunasumbuana sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo fundi anataka kukutia hasara kuna shaft ndani ya gia box imefyatuka au bering imesagika ....na yangu ilikuwa inakwaruza sana na kungu inapungua alipoisambaza kumbe ni beringi ya kushikilia kwenye shaft ya jino no 3 ilikuwa imefyatuka ..ikatoka katika njia yake .....usiogope mkuu peleka kwa fundi mzuri mwambie aifungue yote ....mfukoni uwe na kama 50 hivi bajeti inakaa poa

sent from toyota Allex
 
Mkuu kama inakwaruza ukiwa kwenye gear fulani na mlio unasikika kama vile unatokea kwenye chain box hapo ujue imeua jino..inabidi engine ishushwe ibadilishwe.
 
Nimenunua kwa mtu ila nimeanza kusikia kamlio tofauti kwenye injini kama inakuwa inakwaruza pale unapoanza kuondoka. Je shida ni nini?
Siyo kwenye injini huo mlio unatokea kwenye tairi la nyuma kushoto kuna bearing ya ndani ya tairi ni ndogo ina kutu inazunguka kwa shida wala injini haina shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo nje ya mada kidogo, kuna boxer inachafuka sana oil kuanzia usawa wa air cleaner kushuka chini hua ni nini shida
 

Aah piki piki ndo bei rahisi hivo😀😀 hilo tatizo nikajua laki

Kumbe baskeli yangu nafanyaga service bei ghali sana unakuta inatembea tu ila laki inaeza kukutoka sababu ya kuweka vitu genuine
 
Haitoi moshi mkuu kila kitu kipo sawa shida kuchafuka oil tu hasa pale umepiga ruti ndefu au fupi ambazo hujaiosha mda mrefu
Kungekuwa na moshi ningeweza kusema ni ring zimeisha au block imetanuka. Ila kama moshi hakuna labda inawezekana mzunguko wa oil sio mzuri kuna sehemu oil inapita kwa shida kutokana na baadhi ya matundu yameziba kutokana na uchafu hivyo oil nyingne inapanda juu na kutokea kwenye aircleaner.
Solution: mtafute fundi mzuri anayoijua boxer akuchekie ikiwezekana aisafishe. Imeshawahi nitokea na nikasolve kwa kuisafisha engine na tatizo halijawahi kurudia for two years now
 
Nipo nje ya mada kidogo, kuna boxer inachafuka sana oil kuanzia usawa wa air cleaner kushuka chini hua ni nini shida

Oil kufika hadi kwenye air cleaner inasababishwa na oil kuwa nyingi ndani ya enginekuliko kawaida,hii hutokea wakati unamwaga oil kuna iliyobaki then ukaweka na mpya ujazo ukawa mkubwa kuliko inavyotakiwa.
 
Ohoo shukran kwahiyo engine nzima itabidi ifunguliwe
 
Oil kufika hadi kwenye air cleaner inasababishwa na oil kuwa nyingi ndani ya enginekuliko kawaida,hii hutokea wakati unamwaga oil kuna iliyobaki then ukaweka na mpya ujazo ukawa mkubwa kuliko inavyotakiwa.
Huwa inamwagwa yote mkuu pikipiki inalazwa pande zote kuhakikisha inachuruzika yote
 
Chanzo cha uchafu inakua ni nini mkuu
 
1. Aina ya oil unayoweka
2. Kutokubadili oil filter mara kwa mara. Yenyewe tu ikichoka inazalisha uchafu
Nadhani kutobadilisha oil filter inawezakua sababu nitaibadilisha nione, kwa aina ya oil natumia Total quartz api SL
 
Nadhani kutobadilisha oil filter inawezakua sababu nitaibadilisha nione, kwa aina ya oil natumia Total quartz api SL
Oil Namba ipi? Boxer inatumia oil nyepesi sababu matundu yake ni madogo ukilinganisha na engine za pikipiki za kichina, ukiweka oil nzito lazima isumbue kwenye kupita kwenye matundu hayo, kwa sababu matundu yanayoruhusu oil kusambaa kwenye engine ni madogo sana tofauti na sanlg, fekon, haojue an the like. Recommended oil for boxer bm 150 ni 20w50, we unatumia ipi?
 
Natumia hiyo hiyo 20W50, naona watu wengi wanaweka hizo oil nyingine tofaut na ambazo boxer wamependekeza
 
Natumia hiyo hiyo 20W50, naona watu wengi wanaweka hizo oil nyingine tofaut na ambazo boxer wamependekeza
Kuweka oil tofauti na iliyopendekezwa ni chanzo kikubwa sana cha kuua engine ila watu wengi huwa wanachukulia poa tu anaweka yoyote tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…