Tatizo la ganzi kutokushika(kutokufanya kazi)

Tatizo la ganzi kutokushika(kutokufanya kazi)

Bradha

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
8,787
Reaction score
45,257
Wakuu habari za mchana,

Nina ndugu yangu ambaye amekua akisumbuliwa na meno kwa nyakati tofauti.Ni meno ambayo ameshayang'oa lakini kila alipong'olewa jino ganzi(sindano tatu) haikufanya kazi.

Nimefuatilia hili tatizo kwenye mitandao na nimeona kuna watu wengi ambao wana tatizo hili licha ya kua madaktari hawaafikiani.Wapo madaktari wanaodai wanaochoma wanakosea ndio maana haishiki na wapo wanaokiri kuwa ni tatizo lililopo katika jamii japo hamna utafiti wa kutosha.Pia nimeona tatizo hili lipo kwa ganzi ya sehemu yoyote, sio mdomoni tuu.

Kama kuna mwenye ufahamu zaidi kuhusu hili anaweza kunisaidia kujua hii shida inatokana na nini haswa?Inaepukika?
 
Kuna watu wapo hivyo lakini pia tatizi hili huwakumba maranyingi wanaotumia dawa Kali za maumivu,ulevi uliokithiri subiri wengine wataongezea mkuu
 
Amethibitisha dawa haijaisha muda wa matumizi?
Ni wazo tu....
 
Back
Top Bottom