Tatizo la gari kuchanganya oil na maji

Tatizo la gari kuchanganya oil na maji

Oil inapochanganyika na maji kwenye injini ya gari lako, huashiria tatizo kubwa, mara nyingi huhusiana na hitilafu katika sehemu moja au zaidi ya injini. Sababu za kawaida ni pamoja na:

Kichwa cha Gasket kupasuka:
Kichwa cha Gasket hufunga injini kati ya block ya injini na kichwa cha silinda. Ikiwa imeharibika, oil na maji yanaweza kuchanganyika, na kusababisha uchafuzi wa maji au oil.

Block ya Injini au Kichwa cha Silinda Kimepasuka:
Ikiwa kuna mpasuko kwenye sehemu hizi, oil na maji yanaweza kuchanganyika, na kusababisha uvujaji wa ndani.

Oil Cooler Iliyovunjika:
Ikiwa gari lako lina oil cooler na imeharibika, oil inaweza kuvuja kwenye maji au kinyume chake.

Kichwa cha Silinda Kimepinda:
Injini inapopata joto kupita kiasi, kichwa cha silinda kinaweza kupinda, na kuunda mianya ambapo oil na maji yanaweza kuchanganyika.
 
sponser ntapata😂😂

namwambia baby nataka kununua nissan Juke nina 600k naomba uniongezee
Yani una laki 6 halafu unataka gari ya million 25? Hio hela uliyonayo ni ya madalali kugawana posho tu😂
 
Gari ni toyota vanguard ya 2009. Inachemsha mkuu, na ukiongeza maji hayavuji mahali lakin huyaoni pia kujaa
Straight head gasket issue, na kwa sababu inakula oil pia, utakuwa na tatizo la rings na valve seal. Labda kwa kufuata mtiririko wa matatizo ndo maana fundi kakushauri ununue engine nyingine.
Ukisema utatue matatizo ya hiyo gari yako kwa kifanya rebuild, utatumia pesa nyingi na bado chombo itakuwa haina uhakika
 
Back
Top Bottom