Tatizo la gari kutoa moshi mwingi

GYNEOCOLOGIST

Senior Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
171
Reaction score
110
Wakuu inapokuwa gari inatoa moshi mwingi tena wa bluu mara tu baada ya ku start engine, tatizo huwa inakuwa ni nini? matengenezo yake yanakuwaje?
 
Hapo hakuna uwiano mzuri kati ya mafuta na hewa ndo maana combustion haifanyiki ipasavyo
 
Wakuu inapokuwa gari inatoa moshi mwingi tena wa bluu mara tu baada ya ku start engine, tatizo huwa inakuwa ni nini? matengenezo yake yanakuwaje?
Mkuu na wengine ni vyema mnapo uliza swali au kuomba msaada muwe mnaandika maelezo ya kutosha mfano aina ya gari,inatumia diesel au petrol au gas,au umeme

Mnapo weka habari nusu nusu mtapewa ushauri ambao sio sahihi..
Mfano hapa ungesema gari yako inatumia petrol au disel ingekuwa ni rahisi sana harafu ina engine gani au ni gari gani.

Maana kwa ugonjwa wa gari lako utapewa ushauri tofauti na ugonjwa wako.

SABABU ZA GARI KUTOA MOSHI WA BLUE
Hapo ina maana oil inaunguzwa au inaingia kwenye combustion chamber kuunguzwa pamoja na mafuta.

SABABU ZINAZO SABABISHA OIL KUINGIA KWENYE COMBUSTION CHAMBER.

1.inawezekana valve seal zimechoka
2.cyrinder head gasket imechoka
3.rings za kwenye piston zimechoka
4.PVC imechoka
5.turbo imechoka kama gari ina turbo itakuwa inarudisha hapa.

Hapo 1,2 na 3 kama ni yes basi inabidi ufanye ovarhall engine.
 
Vitu kama petrol filter+plugs+engine filter zitakuwa zimekufa..
Sidhani kama vitu hivyo vinaweza kusababisha moshi wa blue.

Nadhani vitu hivyo kama vinakufa huwa vinasababisha black smoke
 
Hapo hakuna uwiano mzuri kati ya mafuta na hewa ndo maana combustion haifanyiki ipasavyo
Ungetoka moshi mweusi na siyo moshi wa blue mkuu.

Rangi za moshi zinatofautiana sana na huwa ni kiashiria kikubwa sana cha kutambua ugonjwa au ttaizo la gari
 
Nashkuru kwa ufafanuzi, gari ina injini ya 3s na inatumia petroli
 
Overhaul engine, yamaanisha nini Mkuu?
 
Kwa kuongezea:
Aina ya engine oil(brand name) inayotumika pia husababisha. Kuna recycled oil na virgin base oil. Unashauriwa kutumia virgin oil kwa uimara wa engine na uhifadhi wa hali ya hewa.
 
Overhaul engine, yamaanisha nini Mkuu?
Ni kufungua injini mkuu ucheki;
1- valve seal
2- ring piston
3- cylinder head gasket
Na mengineyo na kuzibadilisha kama zimechoka, hii huipa uhai injini yako na kuwa na nguvu karibia na mpya.
Wadau wamekuuliza aina ya gari na hujataja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…