Tatizo la gonjwa la sukari Tanzania

Tatizo la gonjwa la sukari Tanzania

Marathon day

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2020
Posts
643
Reaction score
1,016
Kwa tatizo hili la ugonjwa wa kisukari hapa nzchini kwanini wanasiasa wanaotengeneza ilani ya vyama vyao asiwepo mmoja akaliona hili tatizo na kuja na sera ya matibabu yake yawe bure Kama magonjwa ya TB na Homa ya ini, hasa chanjo.

Kwani kwa Sasa swala la chanjo ya Homa ya ini ni tatizo kuipata na ukiipata bei yake ni kubwa sana kwa familia masikini ni ngumu kumudu.

Nadhani athari za ugonjwa huu nchini kwa Sasa ni kubwa sana. Zamani ilionekana ni ugonjwa wa matajiri, ila kwasasa ni kwa watu wengi hasa masikini.

Kuwe na muongozo wa wizara ya afya kwa vipimo na matibabu yawe bure.

Hilo ni wazo langu tu kwa wanasiasa!! Nawasilisha.
 
Lissu amesema kila m Tanzania atapewa bima ya afya. Hapo kila mtu atatibiwa bure. Itasaidia hata kucheki afya na tatizo likajulikana mapema.

Hili linawezekana hata akiongeza shilingi 100 kwenye mafuta na vinywaji au sigara ili hiyo hela iingie bima ya afya linawezekana.

Hali ya uchumi ni mbaya na dawa bei ziko juu sana ila serikali yangu tukufu inapambana na ndege na mambo ambayo siyo ya msingi.
 
Mkuu hapo naona umeisahau kansa na magonjwa ya moyo maana sasa hivi hayo ndio yanaongezeka kwa kasi, gharama za matibabu ni kubwa
 
Bima jana wametpa list mpya ya madawa yaliyoondolewa ni balaa
 
Mkuu naunga mkono hoja. Ni vizuri pia zikafanyika tafiti kujua chanzo halisi cha kuongezeka kwa tatizo la kisukari nchini kuliko kuishia kusema kitu kilekile kwamba ni suala la life style!!! Mimi naamini kuna shida mahali, ni ama kwenye vyakula au hata maji ya kunywa yanayotoka viwandani na kemikali zake
 
Ugonjwa wa kisukari unasababisha magonjwa mengine hatari kama
  1. Cardiovascular disease
  2. Nerve damage (neuropathy)
  3. Kidney damage (nephropathy)
  4. Eye damage (retinopathy)
  5. Foot damage
  6. Skin conditions
  7. Hearing impairment.
  8. Alzheimer's disease.
  9. Erectile dysfunction
Kwa kila anazotakiwa kutumia kwa mwezi gharama za dawa ziko juu sana kutegemea na hatua ya ugonjwa inaweza kufika au kuzid 150K. Bado upande wa chakula ni changamoto nyingine.
Pamoja na kuwa ni moja magonjwa yaliyopo katika kundi la msamaha wa matibabu maboresho zaidi yanahitajika. Wagonjwa hawanufaiki na msamaha wa matibabu hakuna vipimo hakuna dawa
 
Mkuu hapo naona umeisahau kansa na magonjwa ya moyo maana sasa hivi hayo ndio yanaongezeka kwa kasi, gharama za matibabu ni kubwa
Ongezea na matatizo ya figo
 
Hali ya uchumi ni mbaya na dawa bei ziko juu sana ila serikali yangu tukufu inapambana na ndege na mambo ambayo siyo ya msingi.
Ni kwel hii kitu uliyo sema , ila kwa upande mwingine ukitafakar zaid utagundua yupo sahh kwa asilimia kadhaa, maana uwezi anza kuezeka kabla uja jenga msingi na kuta imara.

Ni mfano tu lakin
 
Tena ombea usikutane na mgonjwa wa kisukari aliyeingia kwenye hatua ya kutumia insulin
Hizo garama zake utaweza hadi uza kibanda,

Ova
 
Back
Top Bottom