Tatizo la goti kukunja

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Habari wakuu

MWEZI uliopita katika harakati zangu shambani nikajikata na panga maeneo ya goti nikawaishwa hospital wakanishona nyuzi Tano Hali ya kindonda inaendelea kuimarika ila bado gotiii halitaki kukunja
Halii hiii inanitesa sana je nichukue hatua Gani za kitabibu?
 
Pole sana
 
Nenda hospital rufaa za mikoa ukaonane na wataalam wa physiotherapy utapata msaada
 
2015 niliumia goti mpirani na likawa halitaki kukunja mguu wa kushoto nikawaelezea wachezaji mpira maveterani wakanambia ww ukunje mdo mdo tu utakubali kweli nikawa najikaza ivo ivo mwisho mpk goti likakubali ila uwe mvumilivu tu na hayo maumivu yake

Dah m ni yanki sanaaa 2015 namaliza F4 apo
 
Ilikichukua MUDA Gani hiyo hali mkuu
 
Ilikichukua MUDA Gani hiyo hali mkuu
Nadhani ni mwezi mmojamna niliumia mwezi wa tano nikaenda likizo ile mwezi wa 6 kurudi shule nipo fresh nasakata kabumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…