Tatizo la kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo…

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani

yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na

mstuko wa moyo.



Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si

vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.



Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.


  1. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
  2. Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?

  1. Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
  2. Umeinama au umelala
  3. Ukishakula chakula

Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.


Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili

na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka.


Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku.

Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.


Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia

mzunguko wa damu mwilini.


Hasa kama hunywi maji.


 
Mkuu kichomi hunijia kwa vitu viwili mfululizo, nikikimbia wakati nimeshiba, hapo vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…