Tatizo la kina cha msingi wa nyumba

Tatizo la kina cha msingi wa nyumba

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
787
Reaction score
1,056
Habari za humu jamvini waheshimiwa.

Nawapongeza sana kwa uwepo wenu kwenye jukwaa hili muhimu.

Mada:
Mimi nilifanya tathmini ya gharama za kujenga msingi wa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, sehemu ya chakula, jiko na choo.
Na tukaafikiana vizuri na fundi.

Nikapambana kununua materials zote ili kuanza ujenzi.
Siku ya kuanza ujenzi nikapatwa na safari ya dharura, nikamwachia mdogo wangu asimamie usalama wa vifaa na kuwalipa mafundi.

Kazi ikafanyika, baada ya wiki moja ikakamilika.

Changamoto niliyoibaini baada ya kurejea ni kwamba,
Mafundi wamejenga msingi ambao umeinuka sana juu, Ila haujaenda chini.

Kwenye msingi wa jumla ya kozi sita (6),
Chini imeenda tofali moja tu, halafu tano zote zimekuja juu.

Hata kama ardhi ni tambarare,
Je, hii haina madhara kwa nyumba waheshimiwa?

Na kama yapo, kuna namna m'badala ya kuiimarisha nyumba?

NB: Bado sijainua boma.
 
Aseee. vipi msingi ulikuwa wa mawe au ndio hilo tofali moja lililozama ardhini?[emoji848]

Kama hakuna mawe au tofali nyingine zaidi chini ya hizo tofali 6 basi kwa usalama wako na wa Jengo lako ikiwemo pia kuepusha hasara na ajali na vifo baadae basi ni vyema ukasitisha kwanza kupandisha boma badala yake imarisha msingi wa nyumba kwanza.
 
At least angeweka tofali 3 chini tena za kulaza ila moja tu hapo naona shida.
 
Mimi si fundi. Ila hapo kuna uwalakini kidogo.

But chanzo cha kuchimba kwenda chini mita 1 huwa ni kutafuta layer ngumu ya udongo ili nyumba inapojengwa ardhi isizidiwe na uzito na nyumba kuanza kutitia.

Cha kujiuliza hapo kwenye tofali moja ardhi ikoje? Ni ngumu? Je baada ya kuchimba msingi walitanguliza nini kabla ya tofali? Mawe? Kokoto? Zege au mchanga?

Pia jiulize mtazuia vipi maji kupita chini ya msingi wa nyumba wa tofali moja?

Mimi ningeshauri msingi wote uuzungushie tofali tatu kwenda chini na moja juu kwa pembeni yake na itakuwa kama urembo kumbe umedhibiti nyumba.

Ila onana na wataalamu zaidi ila hili ni wazo langu.

Ngoja nikuwekee kamchoro!!!

BUT WHY MTU AKUHARIBIE NYUMBA HVYO? HICHO KIFUSI CHA KUFUNIKA HIZO TOFALI 5 SI GHARAMA NYINGINE[emoji34]

[emoji34]

JPEG_20210208_134333_5728549076120107025.jpg
 
Options mbili hapo:
1. Inua level ya eneo lako kwa tofali moja au mbili kwa kumwaga vifusi(umesema eneo lipo flat). Maana yake ni kuwa utazika moja+mbili.
2. Inua eneo la kuzunguka nyumba yako 1m away from the house kwa either kujenga kwa tofali au kumwaga zege, usawa wa tofali mbili tu zinatosha.

Factor muhimu ni soil structure, kama ni udongo mlaini au kichanga basi risk itakuwa kubwa na madhara utayaona nyumba ikishafika juu.
 
Aseee. vipi msingi ulikuwa wa mawe au ndio hilo tofali moja lililozama ardhini?[emoji848]

Kama hakuna mawe au tofali nyingine zaidi chini ya hizo tofali 6 basi kwa usalama wako na wa Jengo lako ikiwemo pia kuepusha hasara na ajali na vifo baadae basi ni vyema ukasitisha kwanza kupandisha boma badala yake imarisha msingi wa nyumba kwanza
Msingi ni wa tofali tu za inchi 6, ambapo katika tofali 6 , tofali 5 zote zipo juu ya ardhi na 1 nd'o ipo chini ya ardhi.
 
Kweli kabisa
 
basi brother tambua huwa hakuna mbadala wa msingi wa nyumba, msingi ndio nyumba yenyewe, kwa hiyo namna pekee ni wewe kukubali hasara ila usikubali kupata hasara zaidi kwa kutafuta mbadala wa kuacha kuchimba upya msingi wa nyumba yako.

Ushauri uliopewa wa kuzungusha tofali nyingine nje hautokusaidia maana hauna uhakika hata kitako kilichopo sasa kwenye hizo tofali sita kitaweza kuhimili jengo, asee nyumba ni kitu kingine mkuu! tofali unazoshauriwa uzizungushe hazitabeba uzito wa nyumba bali zitazuia tu erosion , chimba msingi kwenda chini upate layer ngumu ndipo ujenge msingi wako wa nyumba. Ni kheri uchelewe ufike kuliko kuharakisha alafu usifike unakokwenda.

Kila la kheri
 
Mwenye uzi kaingia mitini.....

May be kabla ya kuvunja ajiridhishe na hiyo layer iliyopo sasa!!! Ni ngumu?
 
Ahsante kwa ushauri ndugu. Kwa ujenzi wetu wa kuzichanga kidogokidogo huu itanichukua muda mrefu kuanza upya.
 
Mwenye uzi kaingia mitini.....

May be kabla ya kuvunja ajiridhishe na hiyo layer iliyopo sasa!!! Ni ngumu?
Sawa mkuu.
Nitamtafuta mtaalam wa masuala ya udongo na ujenzi,
Nimpeleke saiti akapaone ili anishauri kwa uhalisia anaouona yeye.
 
Habari za humu jamvini waheshimiwa.
Nawapongeza sana kwa uwepo wenu kwenye jukwaa hili muhimu.

Mada:
Mimi nilifanya tathmini ya gharama za kujenga msingi wa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, sehemu ya chakula, jiko na choo.
Na tukaafikiana vizuri na fundi.

Nikapambana kununua materials zote ili kuanza ujenzi.
Siku ya kuanza ujenzi nikapatwa na safari ya dharura, nikamwachia mdogo wangu asimamie usalama wa vifaa na kuwalipa mafundi.

Kazi ikafanyika, baada ya wiki moja ikakamilika.

Changamoto niliyoibaini baada ya kurejea ni kwamba,
Mafundi wamejenga msingi ambao umeinuka sana juu, Ila haujaenda chini.

Kwenye msingi wa jumla ya kozi sita (6),
Chini imeenda tofali moja tu, halafu tano zote zimekuja juu.

Hata kama ardhi ni tambarare,
Je, hii haina madhara kwa nyumba waheshimiwa?

Na kama yapo, kuna namna m'badala ya kuiimarisha nyumba?

NB: Bado sijainua boma.
Si watakua wamepanga mawe chini mkuu wakaminina zege au
 
Kabla ya tofali? Hupangwa mawe kwanza mzee kwenye msingi
 
Aseee. vipi msingi ulikuwa wa mawe au ndio hilo tofali moja lililozama ardhini?[emoji848]

Kama hakuna mawe au tofali nyingine zaidi chini ya hizo tofali 6 basi kwa usalama wako na wa Jengo lako ikiwemo pia kuepusha hasara na ajali na vifo baadae basi ni vyema ukasitisha kwanza kupandisha boma badala yake imarisha msingi wa nyumba kwanza
Na mimi ndiyo nimemuuliza hilo ni lazima mawe yaanze kwanza ndiyo yaje tofali
 
At least angeweka tofali 3 chini tena za kulaza ila moja tu hapo naona shida
Lazima itangulie mawe kwanza mkuu, msingi sio tofali msingi ni namna mawe yamepngwa then tofali ya inch 6 ilazwe, ila tofali sasa ndiyo ita determine nyumba yako iende juu sana au lahasha kwa maana ni idadi kiasi gani ziwekwe
 
Mimi si fundi. Ila hapo kuna uwalakini kidogo.

But chanzo cha kuchimba kwenda chini mita 1 huwa ni kutafuta layer ngumu ya udongo ili nyumba inapojengwa ardhi isizidiwe na uzito na nyumba kuanza kutitia.

Cha kujiuliza hapo kwenye tofali moja ardhi ikoje? Ni ngumu? Je baada ya kuchimba msingi walitanguliza nini kabla ya tofali? Mawe? Kokoto? Zege au mchanga?

Pia jiulize mtazuia vipi maji kupita chini ya msingi wa nyumba wa tofali moja?

Mimi ningeshauri msingi wote uuzungushie tofali tatu kwenda chini na moja juu kwa pembeni yake na itakuwa kama urembo kumbe umedhibiti nyumba.
Ila onana na wataalamu zaidi ila hili ni wazo langu......
Ngoja nikuwekee kamchoro!!!

BUT WHY MTU AKUHARIBIE NYUMBA HVYO? HICHO KIFUSI CHA KUFUNIKA HIZO TOFALI 5 SI GHARAMA NYINGINE[emoji34][emoji34]View attachment 1697492
Upo sahihi sana
 
Lazima itangulie mawe kwanza mkuu, msingi sio tofali msingi ni namna mawe yamepngwa then tofali ya inch 6 ilazwe, ila tofali sasa ndiyo ita determine nyumba yako iende juu sana au lahasha kwa maana ni idadi kiasi gani ziwekwe
Kwa huku dar na pwani huwa hakuna haja ya mawe unaweza kuweka mchanga wa kutosha cha msingi msingi tofali tatu au nne ziingie chini then unaendelea kwa mikoani hasa Arusha, moshi mawe ni muhimu kwasababu udogo ni mfinyanzi
 
Mimi arusha hiyo upo sahihi basi, ila naona mawe hufanya nyumba kuwa imara zaidi
 
Back
Top Bottom