Tatizo la kina cha msingi wa nyumba

Tatizo la kina cha msingi wa nyumba

Kwa huku dar na pwani huwa hakuna haja ya mawe unaweza kuweka mchanga wa kutosha cha msingi msingi tofali tatu au nne ziingie chini then unaendelea kwa mikoani hasa Arusha, moshi mawe ni muhimu kwasababu udogo ni mfinyanzi
Dar pia hawatumii mawe kwenye msingi? Ndiyo maana kujenga dar ni rahisi sana, mikoni huku vitu vipo juu sana kuanzia tiles, mchanga, tofali, mabati nk
 
Dar pia hawatumii mawe kwenye msingi? Ndiyo maana kujenga dar ni rahisi sana, mikoni huku vitu vipo juu sana kuanzia tiles, mchanga, tofali, mabati nk
Mkuu Dar huwa wanaangalia aina ya udongo. Kama ni kawaida kabla ya kuanza msingi unamwagwa mchanga wa kutosha then tofali zinafuata.
Kama kuna mfinyanzi inamwagwa zege.

Mawe kwa dar ni ghali sana na hayapatikani kiholela kama arusha na mbeya....
 
Niliwahi kumshauri baba abomoe msingi uliopindishwa akataka kunizaba makofi.. Wiki mbili baadaye akabomoa 'mwenyewe' na kuujenga tena.
 
Mkuu Dar huwa wanaangalia aina ya udongo. Kama ni kawaida kabla ya kuanza msingi unamwagwa mchanga wa kutosha then tofali zinafuata.
Kama kuna mfinyanzi inamwagwa zege.

Mawe kwa dar ni ghali sana na hayapatikani kiholela kama arusha na mbeya....
Msingi upi unakua imara kati ya mawe au wakutotanguliza mawe na kutumia mchanga nk
 
POLE NDUGU.

Unapotaka kujenga nyumba bora na imara lazima umpate fundi bora.

Kwakua watu wanaogopa gharama za kumlipa fundi mzuri wanaamua kuokoteza mafundi mtaani ,

Sasa haya ndio madhara yake.
Unaweza mpata fundi mbovu na akakulipisha pesa ndefu ukapata hasara mara mbili, ukajua ni fundi mzuri kumbe bomu kabisa so kiwango cha pesa anachokuchaji fundi sio kigezo cha fundi bora, mafundi ni wengi utapeli utapeli tu
 
Habari za humu jamvini waheshimiwa.
Nawapongeza sana kwa uwepo wenu kwenye jukwaa hili muhimu.

Mada:
Mimi nilifanya tathmini ya gharama za kujenga msingi wa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, sehemu ya chakula, jiko na choo.
Na tukaafikiana vizuri na fundi.

Nikapambana kununua materials zote ili kuanza ujenzi.
Siku ya kuanza ujenzi nikapatwa na safari ya dharura, nikamwachia mdogo wangu asimamie usalama wa vifaa na kuwalipa mafundi.

Kazi ikafanyika, baada ya wiki moja ikakamilika.

Changamoto niliyoibaini baada ya kurejea ni kwamba,
Mafundi wamejenga msingi ambao umeinuka sana juu, Ila haujaenda chini.

Kwenye msingi wa jumla ya kozi sita (6),
Chini imeenda tofali moja tu, halafu tano zote zimekuja juu.

Hata kama ardhi ni tambarare,
Je, hii haina madhara kwa nyumba waheshimiwa?

Na kama yapo, kuna namna m'badala ya kuiimarisha nyumba?

NB: Bado sijainua boma.
Kwa lugha rahisi msingi umeenda chini kwa 15cm tu daaah!!

Sasa hiyo hasara ungekua umetumia wataalamu ungeipata kweli?

Kwa ushauri tafuta mtu hata mwenye ka diploma ka civil engineering kama ukikosa kabisa injinia... mwambie aje atembelee site yako akupe ushauri.

NB: Nyunba ni msingi, ukiharibu msingi jiandae kuja kuangukiwa na nyumba.
 
Msingi upi unakua imara kati ya mawe au wakutotanguliza mawe na kutumia mchanga nk
Hakika wa mawe ni imara mno.
Lakini kama ardhi ni nzuri si mbaya tukitumia mchanga ku save cost.

Unajua mbeya na arusha kuna nyumba zilizojengwa na mawe full.

Jaribu Dar hapa na hela zetu za SACCOS utajua hujui.....
 
Mkuu Dar huwa wanaangalia aina ya udongo. Kama ni kawaida kabla ya kuanza msingi unamwagwa mchanga wa kutosha then tofali zinafuata.
Kama kuna mfinyanzi inamwagwa zege.

Mawe kwa dar ni ghali sana na hayapatikani kiholela kama arusha na mbeya....
Vipi uki mwaga mchanga + zege juu ktk arshi ya mfinyanzi ..msingi unakuwa imara zaidi bila shaka
 
Dawa ni kumwaga jamvi la cm 15 au 20,kama una pesa jamvi liwe reinforced but kama una unga unga Basi tengeneza reinforced plinth beam yaani funga mkanda wa zege lenye nondo zilizosukwa kitaalamu la cm 20
 
Hawajapanga mawe mkuu.
Ila wameweka mkanda wa zege na nondo juu baada ya ile kozi ya 5.
Mkanda wa zege lenye chuma au? Pili hilo zege lina unene gani? Kama hawakuzingatia idadi ya nondo,spacing na ratio huo ni mtihani ila kama vimezingatiwa hiyo sio kesi maana hujengi ghorofa
 
Kwa lugha rahisi msingi umeenda chini kwa 15cm tu daaah!!

Sasa hiyo hasara ungekua umetumia wataalamu ungeipata kweli?

Kwa ushauri tafuta mtu hata mwenye ka diploma ka civil engineering kama ukikosa kabisa injinia... mwambie aje atembelee site yako akupe ushauri.

NB: Nyunba ni msingi, ukiharibu msingi jiandae kuja kuangukiwa na nyumba.
Ka diploma ndio nini mkuu,aisee bora utafute diploma holder anauzoefu wa changamoto za site kuliko graduate wa makaratasi

Nyumba za kawaida sio ghorofa haxihitaji injinia yeyote hapo
 
Hakika wa mawe ni imara mno.
Lakini kama ardhi ni nzuri si mbaya tukitumia mchanga ku save cost.

Unajua mbeya na arusha kuna nyumba zilizojengwa na mawe full.

Jaribu Dar hapa na hela zetu za SACCOS utajua hujui.....
Dar kujenga nyumba ni rahisi kuliko kununua kiwanja wakati mikoani ni kinyume chake maana tofari huko Dar ni 900 kitu ambacho hakipo mkoani,ukigusa block uwe na pesa kuanzia shs.1700-2000
 
Hapo umekwisha mkuu. Bomoa uanze upya, au chimba nguzo ziende chini kisha pitisha mkanda wa renta ya chini mkali.
 
Dawa ni kumwaga jamvi la cm 15 au 20,kama una pesa jamvi liwe reinforced but kama una unga unga Basi tengeneza reinforced plinth beam yaani funga mkanda wa zege lenye nondo zilizosukwa kitaalamu la cm 20
vipi kama ukitumia meshwire kwenye kufunga mkanda wa msingi badala ya nondo kwenye ardhi ya udongo wa mfinyanzi?
je msingi utakuwa imara kama mtu aliyetumia nondo?
 
Options mbili hapo:
1. Inua level ya eneo lako kwa tofali moja au mbili kwa kumwaga vifusi(umesema eneo lipo flat). Maana yake ni kuwa utazika moja+mbili.
2. Inua eneo la kuzunguka nyumba yako 1m away from the house kwa either kujenga kwa tofali au kumwaga zege, usawa wa tofali mbili tu zinatosha.

Factor muhimu ni soil structure, kama ni udongo mlaini au kichanga basi risk itakuwa kubwa na madhara utayaona nyumba ikishafika juu.
Wazo zuri ila nawaza kuwaje fundi afanye ujinga kiasi hiki?

Huyu fundi amemtia hasara sana jamaa maana hizo hesabu za kuuimarisha huo msingi angezitumia vinginevyo angesogea sana kwenye ujenzi wake.
 
Back
Top Bottom