Habari za humu jamvini waheshimiwa.
Nawapongeza sana kwa uwepo wenu kwenye jukwaa hili muhimu.
Mada:
Mimi nilifanya tathmini ya gharama za kujenga msingi wa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, sehemu ya chakula, jiko na choo.
Na tukaafikiana vizuri na fundi.
Nikapambana kununua materials zote ili kuanza ujenzi.
Siku ya kuanza ujenzi nikapatwa na safari ya dharura, nikamwachia mdogo wangu asimamie usalama wa vifaa na kuwalipa mafundi.
Kazi ikafanyika, baada ya wiki moja ikakamilika.
Changamoto niliyoibaini baada ya kurejea ni kwamba,
Mafundi wamejenga msingi ambao umeinuka sana juu, Ila haujaenda chini.
Kwenye msingi wa jumla ya kozi sita (6),
Chini imeenda tofali moja tu, halafu tano zote zimekuja juu.
Hata kama ardhi ni tambarare,
Je, hii haina madhara kwa nyumba waheshimiwa?
Na kama yapo, kuna namna m'badala ya kuiimarisha nyumba?
NB: Bado sijainua boma.