Tatizo la kiu ya maji mara kwa mara

Loeli

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
997
Reaction score
763
Wataalam nawasalimu. Nina ndugu Yangu amepata tatizo la kiu Mara kwa Mara. Yaani akinywa Maji haipiti hakika 10 midomo imekauka kiu. Amekwenda hospital amefanyiwa vipimo vya diabetes tena wanaita miezi mitatu mfululizo (sijui medical term yake) na ana sukari normal kabisa, H. Pylori negative, vipimo vingi tu normal. Ila pressure ikawa juu 135/85 (ana 50 years). Ila pia akawa na tatizo la kutosikia njaa na gas sana (alishawahi kupata H.Pylori akatibiwa akapona ila kaambiwa vidonda na kama vilipona). Hivyo basi Dr. Specialist wa last months alimpa dawa za vidonda na vitamins ila akaambiwa ajitahidi aweke uzito vizuri kwa sababu ya hiyo pressure na anazingatia.

Angalizo. Hakojoi Mara kwa Mara
Akiwa mikoa ya baridi kiu inatoweka. Akirudi DSM in shida. Kila siku anakunywa 4.5 LTS za Maji na bado kiu inampata. Jasho halimtoki ni kwa nadra sana. Na hivyo ngozi inakauka Fulani hivi.

Msaada Tafadhali.
 
Iv kwann wabongo wengi na hosptal nying zina komalia DM. Wakati pia kuna DIABETES INSPIDUS( kisukari cha maji.) Hii husababishwa na mapungufu ya ADH( ANT DIURETIC HORMONE) in the Hypothalamus.
Na kuhusu
H.pylory anaweza hakawa bado na hao gram negative bacteria maana vituo vingi vya afya vina pima kupitia blood( plasma) wakiwa na lengo laku detect antbody kitu ambacho hakiko 100%. Ni ushauri wangu kupima H.pylory kwaku tumia stool( choo) kwani kina detect antgent za bactria direct.

Huu ni mwangaza tu nimekupa mengine jiongeze.
 
Renal failure..?? Kwa kunywa maji mengi..? Thn yangekuwa yana kwnda wap maana nephron hapo zngekuwa hazna kazi..??
Maji mengi na pia anapata mkojo vizuri tu akiwa amekunywa Maji. Kama ilivyo kawaida asipokunywa Maji basi na mkojo ni kidogo pia. Nitamsisitiza vipimo zaidi hospital tofauti. Asante sana
 
Sukari iko ya aina mbili...
Pia kuna uwezekano mkubwa ana upungufu wa vitamin E ndo maana ngozi inakauka.. Mwambie aanze kutumia vidonge vya vitamin E.
 
Asante mno Mtaalam. Ukweli kipimo cha juzi h pylori walimpima kwa damu. Kikawa negative. Awali alipimwa stool ikawa positive. Tena akiwa amepata tatizo la gas nyingi mno tumboni mpaka akapata shida ya kupumua na ECG ikawa abnormal. Baada ya dose ya h pylori ECG ikawa Norma kabisa. Tatizo la kiu ya Mara kwa Mara haikuwepo. Hapo naongelea kama mwaka hivi umepita. Anyway, medical issues ni changamoto. Ngoja tumpeleke kwa wataalam na vipimo kichwani kama mlivyotushauri. Asante sana.
 
Sukari iko ya aina mbili...
Pia kuna uwezekano mkubwa ana upungufu wa vitamin E ndo maana ngozi inakauka.. Mwambie aanze kutumia vidonge vya vitamin E.
Asante sana Mkuu. Sure alipatiwa multivitamins mwezi Jana na kuna improvement mno kwa ngozi. Na matango tunampa sana. Tutamweleza Mtaalam pia. Na jasho sasa angalau anatoka maana alikuwa jasho kwa past 6 months hakuna kabisa.
 
Wakuu tulimpeleka mgonjwa kwa vipimo na cretinine test haina shida kabisa. Ana tatizo la vidonda I.e alcers na aneandikiwa endoscopy test kuangalia ukubwa wa tatizo maana kichwa kinamuuma pia. Pressure yake ilikuwa 133/84 na P.R 82. Yuko katika control kwa sababu ya uzito huko nyuma.
 
Kiu bado IPO japo siyo kubwa kama ilivyokuwa kabla hajapewa vitamins na dawa za alcers. Je kuna connection yoyote ya alcers na kichwa kuuma na kupata kiu?
 
Mh! Au kameza sponge..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…