Tatizo la kubana kifua

Habari wadau, sorry kwa anaefahamu dawa ya kifua kubana sana hadi kushindwa kupumua na kutoa sauti Kama filimbi. Msaada
Upo wapi??Kama Dar nenda kwa Dr Issaya anapatika mbagala mission kwa buruda
 
Duh hiyo kitu ilinitesa sana nikiwa mdogo. Nilikuwa namiss shule wiki nzima kifuta kimebana. Chai ya tangawizi au tangawizi henyewe ilinisaidia sana pamoja na vidonge vya aminophiline. Nilikuwa natembea navyo mfukoni yaani vumbi kidogo tu hichooo. Lkn nilipofika form 2 nikaanza cheza mpira tulikuwa na timu yetu daraja la nne na baadaye daraja la tatu. Yale mazoezi ya ligi yaliweza kutanua kifua kikawa mara chache mno. Mpaka sasa kikija kinakuja kwa mbali sana bado huwa nanunua aminophiline ingawa nikisikia zimepigwa marufuku lkn mie zilinisaidia sana.
 
Watakuja watu hapa na watasema hivi
" hata mimi nilikuwa nasumbuliwa na kifua ila tangu Bibi yangu anipe Dawa mpaka Leo kimetulia"
utauliza.
"Dawa gani ulitumia uniunganishe?" Atajibu.
"hata sijui na Bibi alishafariki"

Kuna watu wasengerema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…