Tatizo la kucopy na kupaste, Wasabato na matibabu ya Bure kupitia Mkuu wa Mkoa wapi na wapi?

Tatizo la kucopy na kupaste, Wasabato na matibabu ya Bure kupitia Mkuu wa Mkoa wapi na wapi?

Tunapaswa tupongeze kwa mema na sio kuonesha mshangao kama mtoa mada unavyoashiria kupitia post yako

Je kuna ubaya kwa RC kumobilose utoaji wa huduma za Afya???

Jambo jema lipongezwe, na liwe chachu kwa wengine kujitoa kwa ajili ya kuigusa jamii
Na ni vizuri pia kuiga jambo zuri.
 
Mleta mada tatizo lako nini hapo. Hebu tufiche upuuzi tafadhali
Yawezekana huna uelewa wowote kuhusiana na masuala ya tiba. Tiba kamwe haiwezi kutolewa kwa mtindo wa makambi.

Tiba inahitaji investigation, diagnosis na monitoring. Hapo kwenye makambi huwezi kuvipata hivyo vyote.

Tiba siyo sawa na tamasha la ngoma, ambalo watu wanaimba, wanashangilia na kuondoka, wakisubiria jingine mwakakesho.

Tuache usanii kwenye afya za watu. Tuwekeze kwenye hospitali ziluzopo, tuendelee kuongeza idadi ya hospitali kwa kuzingatia kuwa idadi yetu inaongezeka kwa kasi. Na wala tusitafute sifa kwa hadaa kwenye matatizo ya afya za watu.
 
je unamhukumu RC kukurupuka kwa hoja ya udhani kama kambi yao ya matibabu itakuwa na package kamili? je vipi ikiwa dhana yako si kweli? Tafuta taarifa sahihi na za uhakika kisha toa hukumu.
Ninazijuwa hizi kambi nilikuwa kwenye sekta. Wewe kama ni mnufaika nenda tu kakinge hizo posho, lakini hakuna tija yeyote zaidi ya kuonyesha udhaifu wa mfumo wa tiba nchini.

Worse enough ina CRIPPLE huduma za tiba kule ambako watoa huduma wanatolewa kwenda kwenye kambi.
 
Punguza chuki kuna ubaya gani watu wakifanyiwa full body check up ambayo asingeweza fanya kwenye hospital kubwa sababu hana pesa au bima?

Kingine kuna madaktari Bingwa kutoka nje na ndani, kama tatizo ni kubwa si obvious wanaku recommend kwenye hospitali zao ukawaone at a reduced cost kuliko ungekosa kabisa daktari kisa hauna pesa au bima!!

Ni initiative nzuri so tupunguze chuki za kisiasa
 
Mleta mada apelekwe Mirembe hospitali ya vichaa upesi kabla hajavua nguo humu jamii forums

Tuwapongeze wasabato kwa kujitoa kwa jamii
 
Punguza chuki kuna ubaya gani watu wakifanyiwa full body check up ambayo asingeweza fanya kwenye hospital kubwa sababu hana pesa au bima?

Kingine kuna madaktari Bingwa kutoka nje na ndani, kama tatizo ni kubwa si obvious wanaku recommend kwenye hospitali zao ukawaone at a reduced cost kuliko ungekosa kabisa daktari kisa hauna pesa au bima!!

Ni initiative nzuri so tupunguze chuki za kisiasa
Unazungumzia bima za NHIF?
Hio si ni kama huna bima tu
 
Punguza chuki kuna ubaya gani watu wakifanyiwa full body check up ambayo asingeweza fanya kwenye hospital kubwa sababu hana pesa au bima?

Kingine kuna madaktari Bingwa kutoka nje na ndani, kama tatizo ni kubwa si obvious wanaku recommend kwenye hospitali zao ukawaone at a reduced cost kuliko ungekosa kabisa daktari kisa hauna pesa au bima!!

Ni initiative nzuri so tupunguze chuki za kisiasa
Huo ndiyo udhaifu wa mfumo wa afya wa Serikali. Najuwa wewe una akili hebu jaribu kufikiria "outside the box", utaelewa hoja yangu.

Kwa nini hawa watu wasipate hiyo huduma kwenye mfumo unao exist?
 
Hizi ni SIASA tu

Wangekua specific kwamba kutakua na clinic ya bure ya kuonana na kupata ushauri wa kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa na check up

Matatibabu ya kibingwa ni full package inayo husisha vipimo kama ct scan, mri nk nk kisha tiba...... na unapo ongelea tiba ina maanisha vitu kama upasuaji mkubwa na mdogo, upandikizaji viungo, radiation/chemotherapy nk nk
Hivi vitu kwa nmana yoyote ile haviwezi kupatikana kwenye kambi ya siku 3
 
Asante Mkuu kwa kuliona pia. Ila watu wanashangilia UJINGA kwa vile hawajui namna wanasiasa wanatafuta popularity.

Kwenye mafanikio ya Awamu ya 6 ndaniya sekta ya afya, moja ya vitu wanavyovitaja ni ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya afya zaidi ya 400 kupitia fedha za IMF/ COVID-19. Wanataja vilevile kujenga vyumba vya theatres, ununuzi wa CT scan, kuongeza bajeti ya dawa na kuimarisha mifumo ya referral.

Sasa kama hivyo vitu vimeenea nchi nzima kama wanavyosema, kwanini uwaite wananchi wagonjwa kwenye kambi?

Halafu yasemekana madakatari waliohitimu walio jobless nchini wanafika 3000. At the same time kuna vituo vya afya havina medical officers.

Health system is in big mess in this country
 
Seventh day Adventist REFORMS si ndio wale wasabato wenye msimamo mkali..wale wa kwenda airport, vyakula vingi hawali na matibabu hawataki...imekuwaje? Maana Hawa sio Hawa wasabato wa kawaida walio wengi na makanisa
 
Huo ndiyo udhaifu wa mfumo wa afya wa Serikali. Najuwa wewe una akili hebu jaribu kufikiria "outside the box", utaelewa hoja yangu.

Kwa nini hawa watu wasipate hiyo huduma kwenye mfumo unao exist?
Labda exposure ya kimataifa huna
Kambi za matibabu pote duniani hufanyika kama sehemu ya social service

Kuna mamilioni ya wahudumu wa afya husafiri duniani kote wakitoa huduma bure kwa jamii.Wasisoweza hutoa referral mtu aende hospitali za juu

Hata mitaami mfano wakati mwingine hupita na kliniki za macho ukionekana unahitaji miwani wanakupima na kukupa bure

Wewe mchawi hutaki watu wapate huduma bure unataka wafe kama pesa au bina ya afya hawana

Mwanga mkubwa wewe
 
Seventh day Adventist REFORMS si ndio wale wasabato wenye msimamo mkali..wale wa kwenda airport, vyakula vingi hawali na matibabu hawataki...imekuwaje? Maana Hawa sio Hawa wasabato wa kawaida walio wengi na makanisa
Sio hao wa Tanzania wao ni sabato masalia dini yao iko Kyela

Sabato marekani kuna branches nyingi .Kuna madhehebu mengi ya sabato Marekani.Hao wanaokuja ni dhehebu mojawapo la wasabato ambalo ni kubwa sana kule marekani wao huamini Biblia zaidi sio mafundisho ya Mwanamama Hellen White kama wasabato wengine
Afrika pia wapo wasabato wengine ambao ni sehemu ya dhehebu hilo japo wana majina tofauti

Mfano Tanzania kuna makanisa kama Deeper life Ministry lilioanzishwa Nigeria na Dr Kumuyi liko kila kona duniani .Ni wasabato wapentekoste pia kuna kanisa lingine la reformed la Sabato la kipentecoste nalo linaitwa Mountain of Fire and Miracles Ministries lilianzishwa Nigeria na Dr olukoya na lina matawi dunia nzima

Hivyo hao wasabato wa Reformed na dhehenu kubwa sana la kanisa la sabato na ni watu wenye uwezo kifedha tofauti na wale wasabato.Masalia wa kyela waliokuwa wakishinda Airport wakiwa mfukoni hawana hata mia .
Ni watu tofauti wale kiingereza ni Remnants yaani masalia hawa wanaokuja kutoa huduma za afya ni Reformed
 
Hata Yesu alilisha watu 5000 na bado wakamuua. Kwahiyo watu kama mleta mada hawawezi ona jema lolote hata wafanyiwe nini. Kama umeumia kanunue sumu unywe upate raha ya nafsi.
 
Back
Top Bottom