Tatizo la kufeli figo na kufariki

Tatizo la kufeli figo na kufariki

BABA SANIAH

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2013
Posts
4,606
Reaction score
5,922
Habari za muda huu,naomba kufahamishwa kuhusu tatizo la kushindwa kufanya kazi figo.kuna jamaa zangu wawili na ndugu tangu mmoja wamefariki kwa tatizo hilo.naomba kujua yafuatayo
1.tatizo hili linasababishwa na nini?
2.ili kujiepusha na tatizo hilo unatakiwa utumie kitu au chakula gani na usitumie kitu gani.
Ahsanteni naomba kufahamishwa.
 
Figo dawa yake ni kuacha kutumia vyakula vyenye sumu au vyakula feki, kufanya mazoezi, na kunywa maji ya kutosha kila siku.
 
Mm nafikiri amemanisha mavya kula ya kusindikwa na pia madawa ya hospitalini,kila kiukweli penda sana kunywa maji,kula miwa,tikiti maji, na matunda yote kwa ujumla,angalia mlo unao faa,kumbuka kijijini uliko toka ulikuwa unakula nn.na fuata hata kama sip kila cku kupata chakula asilia lakn jitahidi
 
Habari za muda huu,naomba kufahamishwa kuhusu tatizo la kushindwa kufanya kazi figo.kuna jamaa zangu wawili na ndugu tangu mmoja wamefariki kwa tatizo hilo.naomba kujua yafuatayo
1.tatizo hili linasababishwa na nini?
2.ili kujiepusha na tatizo hilo unatakiwa utumie kitu au chakula gani na usitumie kitu gani.
Ahsanteni naomba kufahamishwa.

pia acha pombe. ni sumu
 
Jamani tumezungumza kuhusu kidney failure limekuwa tatizo kubwa TZ. Watu wanasema pombe feki...inawezekana. lakini kuna uwezekano pia ni dawa zetu hazina viwango. Ni fake. Kuna jamaa mmoja mwanae miaka 9 amepata kidney failure. Kwenye uchunguzi wa kina....inasemekana madawa mengi ni fake. Nadhani kuna umuhimu wa uchunguzi zaidi
 
Habari za muda huu,naomba kufahamishwa kuhusu tatizo la kushindwa kufanya kazi figo.kuna jamaa zangu wawili na ndugu tangu mmoja wamefariki kwa tatizo hilo.naomba kujua yafuatayo
1.tatizo hili linasababishwa na nini?
2.ili kujiepusha na tatizo hilo unatakiwa utumie kitu au chakula gani na usitumie kitu gani.
Ahsanteni naomba kufahamishwa.
Mpelelezi wa makosa ya jinai kazini.

Je hao marehemu walikuwa na familia?
 
sababu za kufeli kwa figo ni nyingi.Kuna Blood pressure kama huta idhibiti inaweza kuharibu figo, Pia ugonjwa wa kisukari, Pombe kali pia inaweza kuharibu, Ulaji vyakula vyenye sumu ,Utumiaji wa Dawa za Kienyeji bila vipimo au kujua kiwango cha sumu kilichomo ndani ya hizo dawa , Utumiaji holela wa dawa za hospitalini (kama dawa za Anti biotics)
 
Habari za muda huu,naomba kufahamishwa kuhusu tatizo la kushindwa kufanya kazi figo.kuna jamaa zangu wawili na ndugu tangu mmoja wamefariki kwa tatizo hilo.naomba kujua yafuatayo
1.tatizo hili linasababishwa na nini?
2.ili kujiepusha na tatizo hilo unatakiwa utumie kitu au chakula gani na usitumie kitu gani.
Ahsanteni naomba kufahamishwa

KIDNEY FAILURE/FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Imegawanyika kwenye makundi mawili:

1: Acute kidney failure/figo kushindwa kufanya kazi ghafla.

2: Chronic renal failure/figo kupoteza hali ya kufanya kazi taratibu na kwa muda mrefu

1: FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI GHAFLA
Ni hali inayotokea ghafla pale figo inaposhindwa kutimiza majukumu yake ya msingi kama kuchuja na kuondoa uchafu kwenye damu.

Hali hii inapojitokeza uwezo wa kuchuja, taka mwili hujilimbikiza mwilini kwa kiwango kikubwa ambapo huparaganyisha kemikali nyingine nyingi mwilini.

Upotezaji huu wa uwezo wa kufanya kazi wa figo hutokea ndani ya muda wa siku chache. Huwatokea watu wengi wanaolazwa hospitalini kwa matatizo mbalimbali hasa kwenye chumba cha watu mahututi.

Upotezaji huu wa uwezo wa utendaji kazi wa figo unaweza kupoteza maisha ya muhusika na huitaji uangalizi maalumu chini ya wataalamu wa afya. Pia, hali hii huweza kurejeshwa vyema au karibu na vyema kama utapata huduma sahihi na kwa wakati sahihi pia kama hauna tatizo la kudumu linaloathiri utendaji wa figo husika.

Dalili

Dalili za tatizo la figo kupoteza uwezo wa kufanya kazi ghafla zaweza kuhusisha:

A: Kutokupata/kutoa mkojo wa kutosha.
Husababisha: maji kujaa mwilini, kujaa miguu, visigino.

B: Kutokupumua vyema.

C: Uchovu

B: Kichefuchefu

C: Kuchanganyikiwa

D: Mapigo ya moyo kutokwenda sawa.

E: Maumivu ya kifua

D: Degedege

E: Kupoteza fahamu

NB: Yote haya hutegemea na ukubwa wa tatizo.

Wakati mwingine, tatizo hili huja ghafla bila dalili kulingana na chanzo na huweza kugundulika wakati wa vipimo maabara.

Sababu/Visababishi

1: Unapokuwa na sababu zinazosababisha damu kutokwenda vyema kwenye figo.

2: Kuathiriwa moja kwa mija kwa figo

3: Unapokuwa na sababu ya kuzuia zao taka/mkojo kutokutoka vyema kwenye mfumo wa mkojo.

A: Sababu zinazozuia mzunguko mzuri wa damu
1: Upotezaji wa damu au zao la damu
2: Shambulio la moyo
3: Maambukizi makali mwilini
4: Ini kutokufanya kazi vyema(Matumizi ya dawa za maumivu bila kuzingatia ushauri wa kitaalamu).
5: Mzio/allergy kubwa mwilini
6: Kuungua kwa sehemu kubwa ya mwili
7: Upotezaji mkubwa wa maji mfano: kutapika au kuharisha

B: Madhira kwenye figo
1: Magonjwa, hali mbalimbali na matumizi ya dawa na vitu mbalimbali vinaweza kuwa na athari ya mija kwa moja kwenye figo.

2: Damu kuganda kwenye mishipa ya damu karibu na figo.

3: Mafuta/cholesterol kujaa na kuziba kwenye vishipa vidogo vya figo.

4: Kututumka kwa vishipa vidogo na chujio ndani ya figo.

5: Damu kupoteza uwezo wa kuganda kwa sababu mbalimbali.

6: Magonjwa ya mfumo wa kinga wa mwili kushambulia figo kimakosa/autoimmune.

7: Tiba kama antibiotik bila kufuata taratibu mahsusi, tiba ya kansa/chemotherapy.

8: Matumizi ya chemikali wakati wa kuchukua vipimo/dyes.

9: Magonjwa ya ngozi na misuli ambayo ni zao la mfumo wa kinga mwilini kutokutenda vyema.

10: Sumu mbalimbali zitokanazo na pombe, madini mazito na madawa ya kulevya.

11: Kufa kwa haraka kwa musuli/rhabdomyolysis.

12: Kufa kwa kiasi kikubwa kwa uvimbe mwilini/tumor lysis syndrome.

C: Uzibaji wa njia ya mkojo

Magonjwa na hali zinazosababisha kuziba kwa njia ya mkojo:

1: Kansa ya kibifu cha mkojo

2: Damu kuganda ndani ya njia ya mkojo

3: Kansa ya mlango wa uzazi/ kina mama

4: Kansa ya utumbo mkubwa

5: Kuvimba kwa tezi dume/akina baba

6: Vijiwe ndani ya mfumo wa mkojo

7: Kuharibika kwa mishipa ya fahamu ya kibofu cha mkojo.

8: Kansa ya tezi dume

9: Uvimbe toka sehemu yoyote kugandamiza ndani au nje ya mfumo wa mkojo.

Nani yuko kwenye mazingira hatarishi

Kila mara hali hii hutokea baada ya uwepo wa tatizo lingine la kiafya. Matatizo hayo huusisha:

1: Kulazwa hospitali
Hasahasa kwa tatizo kubwa la kiafya. Ukihitaji tiba kwenye chumba maalumu/ICU.

2: Umri mkubwa

3: Kuziba kwa mishipa ya damu kwenye maeneo ya mikono, miguu(vishipa vidogo).

4: Kisukari

5: Presha ya kupanda

6: Moyo kushindwa kufanya kazi/heart failure.

7: Ugonjwa wa figo

8: Ugonjwa wa ini

9: Aina mbalimbali za kansa na tiba zake

10: Matumizi makubwa ya pombe na kemikali mbalimbali.

Kuzuia hali hii

Si rahisi kutambua ujio wa tatizo husika. Ila unaweza kupunguza utokeaji wa tatizo kwa:

1: Kuwa makini kwa kusoma dawa zote utumiazo kwa kununua moja kwa moja toka duka la dawa kaajili ya maumivu/over the counter medications.
Fuata taratibu zilizoelezwa kutumia dawa husika.

Uchukuaji wa dawa hizi kupita kiwango huweza kusababisha tatizo husika hasa kama una tatizo la figo, presha, sukari nk.


2: Pata ushauri fasaha na mahsusi wa magonjwa tajwa hapo juu jinsi ya kuishi nayo na kuzingatia ushauri na tiba husika.

3: Fanya afya yako kuwa ajenda ya muhimu kwenye maisha yako. Kula vyakula asili/punguza vyakula vyenye kemikali (toka viwandani), balansi mlo wako kulingana na mahitaji ya mwili.

4: Kunywa pombe kulingana na jinsia yako kama ni sehemu ya burudani yako. Hakikisha aina ya pombe ni salama kwa afya yako.

5: Kunywa maji ya kutosha kwa kuzingatia uzito, aina ya kazi na hali ya hewa.
 
vijana wengi tunaangamia hapa kutokana na uraibu wa pombe, Energy drinks na matumizi holela ya dawa
 
Jamani tumezungumza kuhusu kidney failure limekuwa tatizo kubwa TZ. Watu wanasema pombe feki...inawezekana. lakini kuna uwezekano pia ni dawa zetu hazina viwango. Ni fake. Kuna jamaa mmoja mwanae miaka 9 amepata kidney failure. Kwenye uchunguzi wa kina....inasemekana madawa mengi ni fake. Nadhani kuna umuhimu wa uchunguzi zaidi
Ni kweli kabisa Nina ushuhuda wa Mimi mwenyewe.
 
Back
Top Bottom