Tatizo la kuishiwa damu wakati wa ujauzito

fedawa

Member
Joined
Dec 16, 2014
Posts
40
Reaction score
7
Hope wote mu wazima.

Mi ni mdada wa miaka 26, miezi minne nyuma kabla cjapata ujauzito nilipata tatizo kuishiwa damu nilizunguka hospital nyingi hadi regency wakasema sina tatizo, nikawa naendelea kuhangakaika huku na kule.

Mwezi wa tano nikapata mimba hadi sasa mimba ina miezi sabal, tatizo damu inapungua nimekula na kunywa kila kinachoongeza damu lakin haipandi ila inashuka.nilipima nilikuwa na damu 11 nikatumia vitu vya kuongeza damu ndo ikashuka had 10.

Naomba mnisaidie kwani nachanganyikiwa cha kufanya kwa sasa.
 
Kula maini kwa wingi, kula mboga za majani kwa wingi hizi mboga za majani siyo unakula tu wakati wa chakula, kula kama dawa unajaza bakuri unakula.
 
Kama unahudhuria kliniki utapatiwa vidonge vya kuongeza damu vyenye madini chuma(ferrous sulphate) pamoja na dawa za kinga ya malaria (SP).


mama mjamzito anapougua malaria anakuwa katika hatari kubwa inayopelekea kupungua kwa chembe hai nyekundu na hatimaye kupata upungufu wa damu.


otherwise lishe liwe suala la kipaumbele.

dont ignore.
 
Kula maini kwa wingi, kula mboga za majani kwa wingi hizi mboga za majani siyo unakula tu wakati wa chakula, kula kama dawa unajaza bakuri unakula.

nimekula matunda sana,mboga za majan kwa wing tena nachemsha tu,au nasaga matembele nakunywa.rozela lakin ndo hivyo inapungua
 

vidonge natumia toka miez mitatu na sp nimekunywa zimepita kama wiki mbili.
 
tatizo ulilinalo nami limenikuta, nakunywa maji ya matembele, maziwa, folic acid, dawa nyekundu za damu, matunda lakini damu imetoka 12.9 mpk 9.8. Nataka kesho niende hospital ya serikali nikahakikishe zaid, maana sijaamini kabisaa sasa nimepewa dawa inaitwa hemovit wameniambia inaongeza damu kwa haraka. Mimba ndo ina wiki 29
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…