Tatizo la kukojoa kila mara

masanzu

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
605
Reaction score
217
Hbr zenu wanajr
mimi ninasumbuliwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara yaani kwa mchana moja na weza kwenda haja ndogo zaidi ya mara 8-10 kwa usiku nakwenda mara 3-5 kwa usiku mmoja.
UNYWAJI WA MAJI
nimekuwa nakunywa maji kupita kawaida yaani ni zaidi ya lt 3 kwa mchana kwa usiku lt 2.5 kwa usiku mmoja.
KIASI CHA MKOJO
Kila niendapo haja ndogo nakojoa mkojo mwingi sana unakuwa mweupe kama maji ya chupa na hauna harufu ya mkojo.
HOSPITAL
Kuna kipindi niliwah kwenda hospital nikamwelezea doctor akaniambia nipime sukari nikapima ikakutwa ni normal.
UZITO
nina uzito wa kg 85 urefu wa sm 170
SASA WANAJAMVI SIELEWI NINI SHIDA NAOMBA MSAADA
 
Kwa maelezo yako kuwa unakunywa maji mengi ndio maana unakojoa sana na figo lako linaonyesha linafanya kazi vizuri. Pendelea

kunywa maji ya Uvuguvugu kila siku asubuhi kabla ya kula kitu na kabla ya kupiga mswaki kunywa maji ya uvuguvugu glasi 2 kisha kapige

mswak,i ukimaliza kupiga mswaki kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi 1 kaa baada ya saa moja waweza kula chakula. Na mchana kabla ya

kula kunywa maji ya uvuguvugu glasi 2 kisha baada ya saa 1 waweza kula. Na wakati wa usiku kabla ya kula chakula kunywa tena maji ya

uvuguvugu glasi 1 kisha kaa baada ya saa 1 waweza kula. Na wakati wa kwenda kulala kunywa maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha ndio ulale.

Fanya hivyo kila siku kwa faya yako itakuwa ni nzuri punguza kunywa chai wakati wa usiku hiyo chai ndio inayokusababisha uende sana

chooni wakati wa usiku huo ndio ushauri wangu.Cc.@masanzu
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako ntaanza kuufanyia kaz
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako ntaanza kuufanyia kaz
Mkuu masanzu ninakutakia kila la kheri kukojoa kwa wingi kunasababishwa namtu kuwa na mawazo mengi jitahidi pia kupunguza mawazo inaonyesha wewe una mawazo mengi pia.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu masanzu ninakutakia kila la kheri kukojoa kwa wingi kunasababishwa namtu kuwa na mawazo mengi jitahidi pia kupunguza mawazo inaonyesha wewe una mawazo mengi pia.

Asante mkuu majanga te te te te
 
Last edited by a moderator:
Mkuu masanzu ninakutakia kila la kheri kukojoa kwa wingi kunasababishwa namtu kuwa na mawazo mengi jitahidi pia kupunguza mawazo inaonyesha wewe una mawazo mengi pia.

Asante mkuu hili ni majanga te te te te mawazo mkuu ni kwakila binadamu ingawa niyakawaida tu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…