Tatizo la kuku kudonoana

Tatizo la kuku kudonoana

farmersdesk

Senior Member
Joined
May 26, 2012
Posts
164
Reaction score
125
Habari wafugaji!!watu wengi wameuliza kuhusu tatizo la kuku kukudoana.kuku kudonoana husababishwa na vitu vingi sana kwa uchache kwa kuvitaja ni hivi.

1. Kuku kubanana au banda kua dogo ukilinganisha na idadi ya kuku.

2. Kuchanganya kuku wa umri tofauti

3. Upungufu wa madini

4. Vyombo vya maji na chakula kua vichache

5. Kuwaacha kuku walioumia bandani bila kuwatenga hii hupelekea kuku hawa kuanza kudonoa kidonda cha kuku alieumia na hatimae kumuua na hivyo tatizo la kudoana huanza hivyo.

Na kwa uzoefu wangu namba 4 ndo vyanzo vingi vya kuku kudoana.

Namna ya kusolve namba 4.(KUKU KUDOANA)
Hakikisha kuku walioumia huwaachi bandani.
Watundikie kuku majani wapate kudonoa
Pia unaweza waninginizia vitu vyenye rangi hasa rangi nyekundu ili wapate kudonoa.
Kwa kuku wa mayai.
Glp inaweza kuwa msaada sana .

Ungana nasi
Telegram ""farmer sdesk
Instagram @farmers-tanzania
 
Back
Top Bottom