Hilo tatizo linawapata watu wengi wenye umri wake ingawa severity inatofautiana, kitaalamu wanaita dysmenorrhoea, kwa umri wake na jinsi inavyotokea itakuwa spasmodic dysmenorrhoea, wengine maumivu yanakuwa makali mpaka anashindwa kufanya kazi. Sababu za hayo maumivu ni nyingi lakini nyingi ya hizo husababisha mwili kuzalisha vichocheo vinavyoitwa prostaglandins kwa wingi kuliko kawaida kwa watu wenye dysmenorrhoea, hizo prostaglandins husababishaspasmodic myometrial contractions (misuli ya uterus inakakamaa - inacontract - sijui kama ni tafsiri sahihi) ambayo ndio husababisha maumivu, yaani mtu anakuwa na maumivu kama ya uchungu wa kuzaa vile.

Matibabu yake ni kumpa dawa ambazo zinapunguza uzalishwaji wa hizo prostaglandins, hizo dawa zinajulikana kama non-steroidal antiinflamatory drugs (NSAIDS) zikijumuisha asprin, ibuprofen, mefenamic acid, indomethacin nk. Ibuprofen na mefenamic acid ni nzuri zaidi, ukimchanganyia na paracetamol, ataendelea na kazi zake kama kawaida. Hizi dawa atumie tu kwa muda akiwa kwenye hedhi akimaliza anaacha anasubiri mzunguko mwingine kama atapata maumivu tena. (Akitumia hizi dawa asipopata nafuu niPM nitakurudishia gharama zako, ingawa wewe hunilipi kwa ushauri wangu huu ninaokupa, ninajua zitamsaidia)

Maumivu yakiendelea anaweza akatumia combined oral contraceptive pills, natumaini hana mpango wa kuzaa kwa sasa, hizi nazo zimethibitishwa kufanya kazi vizuri, hupunguza maumivu ya hedhi, hupunguza kiasi cha damu kinachotoka na vile vile hupunguza duration ya menses.

Wengine pia wanaadvocate kutanua njia ya kizazi (cervical dilatation), hii inasaidia kwa wale ambao shida ni cervical stenosis (njia ya shingo ya kizazi kuwa nyembamba sana kwa hiyo hedhi inabidi itoke kwa kulazimishwa na huleta maumivu, lakini huyu wa kwako kwa sababu hedhi inatoka ya kutosha nadhani hana stenosis.

Wengi shida hii inakwisha wanapozaa, wengine huendeleanayo lakini severity ya maumivu hupungua.

Kuna watu wazima wengine pia huwa wanapata maumivu wakati wa hedhi, lakini hii ni aina nyinge ya dysmenorrhea, hii chanzo huwa ni tatizo kwenye kizazi, yaweza kuwa uvimbe, endometriosis (sijui kiswahili chake lakini hapa mtu anakuwa na vinyama vya ndani ya kizazi vimeota sehemu nyingine ya mwili kwa hiyo wakati wa hedhi vinamletea maumivu ya ajabu), au shida nyingine yoyote na dawa yake ni kutibu hicho chanzo.