Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Habari za Leo Waungwana. Nawasilisha hoja yangu kama ifuatavyo.
Hivi sasa kila mtu anadai hoja, anasema wengine hawana hoja, ukitoa maoni unaambiwa hauna hoja. Binafsi sielewi kwamba wanao dai hoja wanamaanisha au wanapuuza yaliyosemwa kwa excuse ya kukosa hoja?
katika namna ya pande mbili kutokukubaliana, maono na mitazamo kuhusu ukweli na hata maoni tofauti hupelekea mtu kudai hoja au kuona mwengine amekosa hoja.
Je kuna namna nzuri ya kutokukubaliana na hoja na watu wengine? Unaweza kuwa na hoja za kujenga?
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati wa kuomba au kuwasilisha hoja na namna gani utaweza kufanikisha hilo.
1. Sikiliza wengine wanasema nini
Katika hali ya kutaka kutoa ujumbe.
wengi wetu mara nyingi tunakataa kusikiliza mawazo ya mwingine. Lakini usipuuze mpinzani wako anachotaka kukisema. kwa kuwasikiliza wengine unapata ufahamu na kufunguliwa, pia kubadilisha, kuboresha msimamo wako.
2. Usifanye mashambulizi binafsi dhidi ya wengine.
Mgongano usiwafanye mkagombana, kuwa na mjadala wenye kujenga unapaswa kuepuka mvutano binafsi dhidi ya mwingine.
Mitandao ya kijamii imekua ikiruhusu mashambulizi kutoka kwa mtu asiyetambulika, lakini kwenye mjadala wenye kuhitaji mafanikio masuala haya hayaruhusiwi. Jaribu kuuzuia ulimi wako, vuta pumzi nyingi, kisha jadili.
3. Kubali ukikosea.
Sehemu ya kuwa na mjadala ni kukubali kukosea, wakati mwingine unaweza kuwa mwenye kosa. Inaonyesha kuwa una moyo na umepevuka, na hakuna haja ya kujisikia vibaya kwamba ulikosea jambo fulani.
Tuwe na mtazamo kuwa kuna nafasi ya kurekebisha na kujifunza vitu vipya.
4. Tumia ushahidi wa kimajaribio, ukweli na takwimu kuunga mkono madai yako. Hiyo itasaidia kuonyesha mwanga kwa yale unayo yasema na kukwepa maswali au maoni ya watu wengine kwamba hauna hoja.
Nahitimisha hoja yangu kwa kuruhusu maoni juu ya nini cha kuzingatia ili kuunda hoja makini. Karibu....
#BM