Kutapika ni mojawapo ya dalili inayojitokeza sana katika kipindi cha ujauzito, hasa miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Ni dalili inayofahamika sana katika mambo ya afya kiasi kwamba inajumuishwa kama dalili mojawapo ya mimba. Yaani mara nyingi si dalili ya kuhofia sana, ni kitu cha kawaida kwa mama mjamzito.
SABABU kubwa ya dalili hii ni mabadiliko ya vichocheo vya mwili vinavyotokana ama vinavyosaidia kutunza mimba- kuna kemikali kadhaa zinazotengenezwa na mwili kipindi hicho na ndizo zinachangia kuleta kichefuchefu na/ama kutapika. Kuna uhusiano na mambo ya kisaikolojia pia( vile ambavyo anapata msaada kwa jamii inayomzunguka)
TIBA tunaanza na mabadiliko ya mfumo wa maisha. Inashauriwa kula vyakula visivyoleta kichefuchefu( mfano.. vyenye asili ya ukavu badala ya vyenye mafutamafuta), ale kiasi kidogokidogo kila baada ya muda fulani kuliko kula chakula kingi kwa wakati mmoja, apewe msaada wa karibu kutoka kwa wanafamilia( lakini waepuke kumdekeza kwani inahusishwa na kuongeza ukubwa wa tatizo). Anaweza pia kutumia dawa za kuondoa/kupunguza kichefuchefu zilizoidhinishwa ( si maadili ya afya kuzitaja).
TAHADHALI Kutapika kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa pia, hasa ikiwa inamdhoofisha mama mjamzito afya(mfano anakonda...) , inaendelea hasa baada ya miezi mitatu ya kwanza, anatapika kila anachokula ... No vema kuonana na wahudumu wa afya wachunguze vizuri kuhusu hali yake, hasa anapoudhuria kliniki.
Nafikiri umepata kuelewa kwa sehemu.