Tatizo la kutapika

Tatizo la kutapika

mnyandzombe

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2015
Posts
245
Reaction score
194
Habari Za mapumziko ya wikendi.

Tangu niingie humu ni mengi Nimejifunza na hata kupitia maswali mengi ya watu tofauti kuhusu maisha.

Namimi leo ninaomba kufahamamishwa juu ya tatzo hili la kutapika hasa kwa mwanamke mjamzito kila mara hutokana na nini? Je, kuna tiba mbadala? Maana wife anapata shida ya kutapika akila chochote anatapika yaani ni shida.
Naamini wazoefu na madaktari wa haya mambo mtanisaidia kwa mawazo ya kitaalamu.
Ahsanteni na usiku mwema
 
Kuna dawa ya kuzuia nost sijui kitu kama hicho
 
Nenda duka la madawa kaseme hivyo watakusahihisha nost
 
Kutapika ni mojawapo ya dalili inayojitokeza sana katika kipindi cha ujauzito, hasa miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Ni dalili inayofahamika sana katika mambo ya afya kiasi kwamba inajumuishwa kama dalili mojawapo ya mimba. Yaani mara nyingi si dalili ya kuhofia sana, ni kitu cha kawaida kwa mama mjamzito.

SABABU kubwa ya dalili hii ni mabadiliko ya vichocheo vya mwili vinavyotokana ama vinavyosaidia kutunza mimba- kuna kemikali kadhaa zinazotengenezwa na mwili kipindi hicho na ndizo zinachangia kuleta kichefuchefu na/ama kutapika. Kuna uhusiano na mambo ya kisaikolojia pia( vile ambavyo anapata msaada kwa jamii inayomzunguka)

TIBA tunaanza na mabadiliko ya mfumo wa maisha. Inashauriwa kula vyakula visivyoleta kichefuchefu( mfano.. vyenye asili ya ukavu badala ya vyenye mafutamafuta), ale kiasi kidogokidogo kila baada ya muda fulani kuliko kula chakula kingi kwa wakati mmoja, apewe msaada wa karibu kutoka kwa wanafamilia( lakini waepuke kumdekeza kwani inahusishwa na kuongeza ukubwa wa tatizo). Anaweza pia kutumia dawa za kuondoa/kupunguza kichefuchefu zilizoidhinishwa ( si maadili ya afya kuzitaja).

TAHADHALI Kutapika kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa pia, hasa ikiwa inamdhoofisha mama mjamzito afya(mfano anakonda...) , inaendelea hasa baada ya miezi mitatu ya kwanza, anatapika kila anachokula ... No vema kuonana na wahudumu wa afya wachunguze vizuri kuhusu hali yake, hasa anapoudhuria kliniki.
Nafikiri umepata kuelewa kwa sehemu.
 
Hakuna aliemzidi wife kwa kutapika ndani ya mwez alibakia fuvu km ana ngoma anatapika mpk anashindwa hata kukaa anatapika zaidi ya Mara 70 kwa siku mpk nikawa naita madokta home wamuekee dripu nikaja kupata dawa moja ni kiboko aisee ina itwa VOMIDOXINE ya misri balaaa anameza kidonge kimoja before hajakula kitu
Kutapika alikuskia kwny bomba mpk Leo akishika ujauzito lzm nikazitafute hizo dawa imekua ni mkombozi wangu but shauriana na daktar wake ni dawa nzur mnooooo
 
Miezi mitatu ya mwanzo ni kawaida, ila kama hali ni mbaya apate dawa zinaitwa nosic zinasaidia.
Nb: asijinywee tu dawa bila kumuona daktari
 
Kutapika ni mojawapo ya dalili inayojitokeza sana katika kipindi cha ujauzito, hasa miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Ni dalili inayofahamika sana katika mambo ya afya kiasi kwamba inajumuishwa kama dalili mojawapo ya mimba. Yaani mara nyingi si dalili ya kuhofia sana, ni kitu cha kawaida kwa mama mjamzito.

SABABU kubwa ya dalili hii ni mabadiliko ya vichocheo vya mwili vinavyotokana ama vinavyosaidia kutunza mimba- kuna kemikali kadhaa zinazotengenezwa na mwili kipindi hicho na ndizo zinachangia kuleta kichefuchefu na/ama kutapika. Kuna uhusiano na mambo ya kisaikolojia pia( vile ambavyo anapata msaada kwa jamii inayomzunguka)

TIBA tunaanza na mabadiliko ya mfumo wa maisha. Inashauriwa kula vyakula visivyoleta kichefuchefu( mfano.. vyenye asili ya ukavu badala ya vyenye mafutamafuta), ale kiasi kidogokidogo kila baada ya muda fulani kuliko kula chakula kingi kwa wakati mmoja, apewe msaada wa karibu kutoka kwa wanafamilia( lakini waepuke kumdekeza kwani inahusishwa na kuongeza ukubwa wa tatizo). Anaweza pia kutumia dawa za kuondoa/kupunguza kichefuchefu zilizoidhinishwa ( si maadili ya afya kuzitaja).

TAHADHALI Kutapika kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa pia, hasa ikiwa inamdhoofisha mama mjamzito afya(mfano anakonda...) , inaendelea hasa baada ya miezi mitatu ya kwanza, anatapika kila anachokula ... No vema kuonana na wahudumu wa afya wachunguze vizuri kuhusu hali yake, hasa anapoudhuria kliniki.
Nafikiri umepata kuelewa kwa sehemu.
Ubarikiwe kwa majibu
 
Asanteni sana kwa majibu yenu nitayafanyia kazi
 
Back
Top Bottom