Mimi nilipata shida hiyo nikiwa advance. Niliteseka sana, na kabla ya shida hiyo kunipata nilikuwa kipa wa kutegemewa. Sasa nikawa nawaambia wenzangu kuwa siwezi kusimama golini coz sioni vizuri lakini wakawa wananilazimisha. Mipira ilikuwa inapita kama hakuna MTU golini.
Baadaye nikaja kwenda hospitali nikapimwa miwani, lensi zote zikagoma kusapoti uoni. Nikarudishwa kwa daktari akanipa vidonge vitamin B, lakini wapi? Baada ya dozi ile kuisha nilienda duka la madawa nikihitaji vitamin B lakini wakasema hawana ila wana vitamin B complex, wakanipa hivyo. Baada ya kutumia hali ilibadilika kidogo.
Sisemi moja kwa moja kuwa vilinisaidia, ila hali yangu ya sasa si kama zamani. Nadunda tu bila miwani. Ila kipindi kile, magari yalikuwa yakipita pembeni yangu siwezi soma hata plate number. Mungu ni mwema.