Tatizo la kutopata choo na suluhisho lake

cheupr

New Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
3
Reaction score
0
Naweza kukaa wiki mbili mpaka tatu bila kupata choo kikubwa, mwenye ufahamu namna ya kutatua tatizo hili anisaidie.
 
Labda unakula nutrients tupu ambazo hazina makapi

Jaribu kula 'mabumunda' au kula mapapai
 
Naweza kukaa wiki mbili mpk tatu bila kupata choo kikubwa,mwenye ufaham namna ya kutatua tatizo hili anisaidie

UKOSEFU WA KUTOPATA CHOO: SOMA TIBA RAHISI

UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili

kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
Cha kufanya
1. Kunywa maji(vuguvugu)ya kutosha mara kwa mara.
2. Kula matunda ya aina mbalimbali kila siku
3. Pendelea Kala mboga za majani
4. Punguza au acha kabisa ulaji wa nafaka zilizo kobolewa (eg. Sembe, Wali etc)
5. Punguza sana au acha kwa muda ulaji wa nyama (Red meat) - hii huchukua muda mrefu sana kumeng'enywa tumboni.
6. Jitahidi kila siku ufanye mazoezi japo kwa dakika zisizopunga 30.
7. Kula kwa kiasi. usile ukashiba sana. Kula mpaka uhisi njaa imeisha basi.
 
Mimi sina ufahamu lakini ningekushauri uende hospitali na mambo yoote utapata majibu
 
kati ya yote uliyo shauriwa ni mazuri sana pia uwe na utaratibu wa kunywa dawa za minyoo
 
go for peptic ulcers test may be ur victim of it
 
Mkuu kunywa dawa za minyoo.alafu pichanisha milo kwa nusu saa.Fanya hivi:baada ya kula kaa nusu saa ndipo ule tunda alafu kaa tena nusu saa ndipo unywe maji.unapokula chakula na kuunganisha na vimiminika husababisha usagaji wa chakula usifanyike vyema.Tatizo lako ni kubwa nenda kanunua ukwaju alafu chemsha kisha unywe juice yake glasi 2 asubuhi kabla ya kula ukae kama nusu saa ndio uanze kula.unaweza kuni pm ili nikupe maelezo zaidi.
 
Naweza kukaa wiki mbili mpaka tatu bila kupata choo kikubwa, mwenye ufahamu namna ya kutatua tatizo hili anisaidie.
weekend hii gonga nyama ya kuchoma ya kutosha na ugali halafu jaribu kugonga dreep(bia tena safari lager ama Guinness za kutosha!

Ukikosa tena kesho au usiku huo huo utuambie tukupe dozi ingine!
 
Hii ni hatari sana kiafya, wataalamu wanasema kuwa mtu anaweza kupoteza maisha iwapo atakaa muda wa siku saba bila kupata choo, mbaya zaidi ni kuwa unakuwa katika hatari ya kupata asilimia 90 ya magonjwa sugu ikiwamo SARATANI YA UTUMBO MPANA,

FUATILIA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI.
 
Naweza kukaa wiki mbili mpaka tatu bila kupata choo kikubwa, mwenye ufahamu namna ya kutatua tatizo hili anisaidie.


Hii ni hatari sana kiafya, wataalamu wanasema kuwa mtu anaweza kupoteza maisha iwapo atakaa muda wa siku saba bila kupata choo, mbaya zaidi ni kuwa unakuwa katika hatari ya kupata asilimia 90 ya magonjwa sugu ikiwamo SARATANI YA UTUMBO MPANA,

FUATILIA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI.
 
Haya nyogeza hiyo
 

Attachments

  • IMG-20140522-WA014.jpg
    52.2 KB · Views: 512
Mboga mboga na matunda yanasaidia.

Maji ya kutosha yanahitajika, na vizuri kama yatakua ya uvuguvugu ndo mazuri.

Mazoezi nayo pia yanasidia.

Katika izo mboga mboga mchicha ndo bomba tena vizuri km utafanya mchemsho tu
 
weekend hii gonga nyama ya kuchoma ya kutosha na ugali halafu jaribu kugonga dreep(bia tena safari lager ama Guinness za kutosha!

Ukikosa tena kesho au usiku huo huo utuambie tukupe dozi ingine!
Hii ngumu kumesa aree
 
Hii ni hali ambayo unakuta mtu anakula mlo vizuri mara tatu kwa siku lakini anapitisha siku kati ya moja au tatu,bila kupata choo yani ana tatizo la kukosa choo.

Pia kupata choo kigumu kama cha mbuzi na maumivu makali ama kufikia kutoa choo kikiwa na matone ya damu,ni dalili za tatizo la kukosa choo.

Tafiti zinazonyesha kuwa mtu anaweza kupoteza uhai, endapo atakosa choo siku tano mpaka saba mfululizo.
Sababu za kukosa choo.

1.Kukosa mlo kamili ama kula vyakula vingi vyenye kiwango kikubwa cha wanga na mafuta
2.Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda.
3. Kunywa maji yasiyo salama
4. Kuvuta hewa chafu
5. Mifumo hatarishi ya maisha kama matumizi ya pombe na sigara kwa wingi
6. Kula vyakula vilivyokobolewa na vilivyochanganywa madawa ili visiaribike.

Je wafahamu athari zake
1. Bacteria wenye madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine.
2. Chakula kutomeng!enywa vizuri.
3. Maumivu makali wakati wa kupata choo.
4. Uchafu uliokaa mda mrefu kugeuga sumu.

Pia yaweza sababisha magonjwa sugu kama haya,
1. Presha
2. Saratani ya utumbo mpana
3. Magonjwa ya ini
4. Magonjwa ya ini
5. Tumbo kujaa gesi
6. Kuongezeka uzito
7. Kusukari
8. Magonjwa ya ngozi.
9. Figo kushindwa kufanya kazi
10. Kukakamaa kwa mishipa ya damu

Hili tatizo ni janga la wengi,na suluhisho lipo unatibiwa unapona kabisa,kama una tatizo hili,karibu upate tiba ipo ya kumaliza tatizo lako.

Kwa maswali na mahitaji no 0717556768.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…