Tatizo la kutopata haja kubwa (mimi ni mtu wa aina gani)

Tatizo la kutopata haja kubwa (mimi ni mtu wa aina gani)

NTALYAGA

Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
19
Reaction score
4
Ndugu wana JF habari za leo.

Mwenzenu nina tatizo la kiafya sipati haja kubwa kabisa. Ninachukua hadi siku 5 ndo napata hali ya kwenda haja kubwa lakini nikienda hata sipati haja nzuri sometimes natoa tu hewa na kama mapovu hivi.

Naomba ushauri wenu wapendwa; ni tatizo gani? Maybe naweza pata tiba humu humu kwa wanaJF wenzangu.

Asanteni.
 
Usile ugali wa sembe mkuu.
Pia jitahidi kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama maembe na jamii zake.
 
Mkuu, inaonesha una tatizo liitwalo constipation... Jitahidi kula vyakula vya roughages yani matunda kama maembe na mapapai na mboga za majani ili kulainisha choo, pia unywe maji na juisi za kutosha itasaidia.... Pia waweza muona daktari kwa ushauri zaidi. Zipo dawa ambazo zinafungua tumbo kama hujapata choo kwa muda mrefu.
 
Kula vyakula vya asili vyenye nyuzinyuzi, epuka sukari na chumvi nyingi, punguza mawazo mengi au msongo kwa kufanya mazoezi mepesi ya viungo itakusaidia kuondoa constipation!
 
Polee sanaa mkuu nahic dawa ya kukusaidia hapo ni kama Bisacordily na buscopan nenda ukatoe maelezo ya kina kwa daktari juu ya tatizo hilo!! Ni kama bowel irritability syndrome!!
 
Jaribu kunywa juice ya ukwaju kila jioni mara baada ya kula. iwe concentrated kiasi ( 1 kg ukwaju ikupe 2 kg juice )
nenda kwa uwiano huo. Kwa maelezo yako kama ukipata asali ni vizuri weka asali kijiko kimoja kikubwa kwenye glass moja ya juice ( glass ya kawaida ni kati ya 200 hadi 250 mls) . Hii itakusaidia sana , ikitokea umekunywa ukaharisha aidha punguza kiasi cha asali ama usiweke kabisa,
Jaribu halafu ulete mrejesho
 
Pole sana ndugu yangu, ni tatizo kubwa sana hilo kwa hivyo sio la kupuuza yaweza kuwa:

1. Redundant colon
2. Chakula ulacho ni kiasi kidogo na ni aina ambayo haina fibres so kuna kuwa hakuna wastes za kutosha kuweza kupata choo.

Suluhu:
1. Kula vyakula vyenye fibres kwa wingi mfano salads, matunda na maganda, brown rice, brown bread na dona for sometime, like a month kama hiyo hali haita change basi ufanye vipimo kama

1. Barium enema examination
2. CT Scan examination with oral contrast.

Waweza nicheki kwa suala la vipimo.
 
Pole sana, kunywa maji mengi sana, kula matunda jioni hasa mapapai, usile kitu kingine chochote zaidi ya maji na matunda pengine itasaidia, vinginevyo nenda hospital au kwa wamasai wana dawa ila ni kali sana
 
Kunywa maziwa fresh asubuhi kabla hujala chochote, then baada ya kula lunch kula papai. Hivyo vyote vitasaidia kuflash mfumo.
 
Back
Top Bottom