Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

TATIZO LA HARUFU MBAYA MDOMONI

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la kuwa na harufu mbaya mdomoni
hali inayopelekea kukosa mahusiano mazuri na watu kama vile kuchukiwa
na wapenzi wao mpaka kupelekea kubunjika kwa mahusiano yao, marafiki, na watu wengi wa karbu.

KINACHO SABABISHA HARUFU MBAYA MDOMONI

Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kwa kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni.
Maana Wengi wetu hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula.
Mabaki hayo uoza na kuzalisha bakteria ambao ndo chanzo cha mdomo kunuka.

NINI UFANYE ILI KUEPUKA HARUFU MBAYA MDOMONI??

Kuna njia za kawaida na rahisi sana unazoweza fanya ili mdomo wako usiweze kunuka

1. KUNYWA MAJI MENGI

Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo.

2. TUMIA MATUNDA KAMA VILE APPLE, TANGO NA PERA.

Matunda kama haya yanaongeza mate mdomoni na kuzuia uwepo wa bacteria ambao husababisha harufu mbaya. Kula kipande cha tango au apple hasa baada ya chakula. Pera husaidia wale wanaotoka damu kwenye fizi pia.

#KumbukaHii
Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji ya kutosha.

Lakini wengi wamejaribu njia mbali mbali kuondoa tatizo hilo lakin wameshindwa
Ila bado msaada upo.

Wasiliana nasi kwa msaada wa tatizo lako kama linakusumbua au limekusumbua kwa mda
Mrefu.

Sms/Call/Whatsapp +255 653216061

Tunajali na kusamini afya yako
Ahsante kwa ushauri
 
Unafikir pesa inapatkana kirahisi namna hii? yaani umeshindwa kutembelea mitandao mbalimbali ukasoma na kuelewa chanzo ni nin badala yake unakuja na uongo.
 
We jamaa hujafanya utafiti wa hili tatizo na bora hata usinge jinasbu kwamba ni mtaalam.

Hili tatizo huwa lipo hata ukipiga mswaki vizuri hata kila baada ya saa. Naona umerahisisha tu alaf unataka upigiwe simu,

Fanyeni tafiti ndo mjiite wataalam
 
Wakuu sababu kubwa za kutoa harufu mbaya kinywani ni kana zifuatazo
_kutosafisha ulimi wakati wa kupiga mswaki
_meno yaliyo toboka au yaliyoza mdomoni
_magonjwa ya mfumo wa mmengenyo wa chakula
-magonjwa ya mfumo wa upumuaji
_infection/au usaha eneo la nyuma ya kinywa(faucial and tonsilar region)
_Sababu nyingine ni ugaga wa meno(calculus),uvimbe mdomoni,vidonda n.k



Namna ya kuondokana na hili tatizo
_piga mswaki,kwakutumia dawa ya meno walau mara mbili kwa siku...kumbuka kusafisha ulimi mwishoni
_kama una jino lenye tobo/au limeoza nenda kamuone daktari wa kinywa na meno .....kuna kuziba meno,kusafisha meno na mengine mengi.
_matatizo ya mfumo wa upumuaji na mmengenyo wa chakula,nenda kamuone daktari...upate matibabu

_kwa infection kwenye tonsillar region, onana na daktari wa kinywa na meno upate matibabu...
 
Wakuu sababu kubwa za kutoa harufu mbaya kinywani ni kana zifuatazo
_kutosafisha ulimi wakati wa kupiga mswaki
_meno yaliyo toboka au yaliyoza mdomoni
_magonjwa ya mfumo wa mmengenyo wa chakula
-magonjwa ya mfumo wa upumuaji
_infection/au usaha eneo la nyuma ya kinywa(faucial and tonsilar region)
_Sababu nyingine ni ugaga wa meno(calculus),uvimbe mdomoni,vidonda n.k



Namna ya kuondokana na hili tatizo
_piga mswaki,kwakutumia dawa ya meno walau mara mbili kwa siku...kumbuka kusafisha ulimi mwishoni
_kama una jino lenye tobo/au limeoza nenda kamuone daktari wa kinywa na meno .....kuna kuziba meno,kusafisha meno na mengine mengi.
_matatizo ya mfumo wa upumuaji na mmengenyo wa chakula,nenda kamuone daktari...upate matibabu

_kwa infection kwenye tonsillar region, onana na daktari wa kinywa na meno upate matibabu...
Ni kweli kabisa [emoji120]
 
Mkuu nitafte nikuunganishe na mtaalam wa kinywa, ana dawa nzuri sana na utaleta mrejesho.
Dawa yake 100% ni mitishamba na ameitafiti kwa miaka 5 kwa kushirikiana na Daktari toka Usa.
Wameipaki vizuri mno.
Mimi nilipatwa na tatizo la meno kuwasha sana, nilitumia siku 3, tatizo lilikoma sasa ni mwaka.
Kuna watu waliokuwa na matatizo ya midomo kunuka sana, wengine meno kuoza hiyo dawa imewaponya.
Naomba uniaunganishe mkuu
0657613151

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za muda huu waungwana;

Mimi ni kijana wa kiume, umri 24 yrs...

Nimekuwa nikisumbuliwa sana na hili tatizo la harufu mbaya kinywani kwa takribani miaka 3 sasa nikiangaika huku na kule katika kutafuta tiba ila sijafanikiwa.

Nimekwenda Hospitali kwa Wataalamu wa Kinywa/Meno 《Dentist》 Baada ya kunifanyia vipimo na uchunguzi kwenye fizi na Meno wakakuta nipo safi sina tatizo lolote ila Wakanishauri nitumie Hydrogen Peroxide《Mouth Wash》na Ant-Biotic lakini bado tatizo liko pale pale.

Naombeni mnisaidie Waungwana nini kifanyike niondokane na hali hii, mahusiano yangu yanayumba...

Nakosa amani, kwa ufupi sina furaha nahisi kukata tamaa kabisa.
 
sijui nielezee vipi ila tambua kwenye mahusiano yangu kiukweli ninapitia kipindi kigumu sana imefikia hatua hata mpenzi niliye naye sasa ameanza kunichoka uvumilivu umemshinda anahitaji tuvunje mahusiano yetu.
Polee! I feel it.

Hakikisha unasugua ulimi vizuri na si meno tu. Ulimi unachangia sehem kubwa kuwa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ziko dawa za kinywa nzuri..ntakupa jina lake badaye.

Pia
Baada ya kula tu na kusukutua kinywa unaweza kutumia limao, yan unakamua unakunywa namanisha unakamua hlf unakunywa..kama unasukutua hiv, au kulamba kwa ulimi pia.

Limao linasaidia kuua bacteria hao. Unaeza tumia limao baada ya muda fulani. Ukiulizwa kwanini unatumia limao unaeza sema ni kwa ajili ya kuzuia gesi tumboni kila wakati au tumbo lisikuume baada ya kula.

Wengine wanatumia tangawizi kutafuna kipande kidogo tu nayo inasadia. Ni chungu kiasi ili dawa nzuri tu unaposukutua nayo kinywani. Unaeza tafuna pia baada ya muda fulani.
Zote njia unaweza tumia hata usiku kabla hujalala na asubuhi kupiga mswaki unatumia pia
 
Nilikuwa na hii shida nikiwa sekondari ila shida yangu nikajua ipo sehemu gani.

1. Kama una tabia ya kutafuna vinyama ndani ya kinywa acha, mimi baada ya kuacha niliona mabadiliko makubwa.

2. Piga mswaki kwa dawa ambazo ni herbal. Unaponunua dawa ya meno itazame mwisho kabisa ina alama ipi? Je ni red, blue or green? Tumia saana green maana hiyo natural, red ni chemical na blue ni natural+chemical. Nitaweka picha ya hizi alama.

3. Jizoeze kupiga mswaki kila ulalapo na uamkapo, ata kama ni mchana wewe piga.

4. Kuna maji flani ya kusukutua ktk kinywa, supermarkets wanauza, uwe unatumia mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom