Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Ahsante kwa ushauri
 
Unafikir pesa inapatkana kirahisi namna hii? yaani umeshindwa kutembelea mitandao mbalimbali ukasoma na kuelewa chanzo ni nin badala yake unakuja na uongo.
 
We jamaa hujafanya utafiti wa hili tatizo na bora hata usinge jinasbu kwamba ni mtaalam.

Hili tatizo huwa lipo hata ukipiga mswaki vizuri hata kila baada ya saa. Naona umerahisisha tu alaf unataka upigiwe simu,

Fanyeni tafiti ndo mjiite wataalam
 
Wakuu sababu kubwa za kutoa harufu mbaya kinywani ni kana zifuatazo
_kutosafisha ulimi wakati wa kupiga mswaki
_meno yaliyo toboka au yaliyoza mdomoni
_magonjwa ya mfumo wa mmengenyo wa chakula
-magonjwa ya mfumo wa upumuaji
_infection/au usaha eneo la nyuma ya kinywa(faucial and tonsilar region)
_Sababu nyingine ni ugaga wa meno(calculus),uvimbe mdomoni,vidonda n.k



Namna ya kuondokana na hili tatizo
_piga mswaki,kwakutumia dawa ya meno walau mara mbili kwa siku...kumbuka kusafisha ulimi mwishoni
_kama una jino lenye tobo/au limeoza nenda kamuone daktari wa kinywa na meno .....kuna kuziba meno,kusafisha meno na mengine mengi.
_matatizo ya mfumo wa upumuaji na mmengenyo wa chakula,nenda kamuone daktari...upate matibabu

_kwa infection kwenye tonsillar region, onana na daktari wa kinywa na meno upate matibabu...
 
Ni kweli kabisa [emoji120]
 
Naomba uniaunganishe mkuu
0657613151

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za muda huu waungwana;

Mimi ni kijana wa kiume, umri 24 yrs...

Nimekuwa nikisumbuliwa sana na hili tatizo la harufu mbaya kinywani kwa takribani miaka 3 sasa nikiangaika huku na kule katika kutafuta tiba ila sijafanikiwa.

Nimekwenda Hospitali kwa Wataalamu wa Kinywa/Meno 《Dentist》 Baada ya kunifanyia vipimo na uchunguzi kwenye fizi na Meno wakakuta nipo safi sina tatizo lolote ila Wakanishauri nitumie Hydrogen Peroxide《Mouth Wash》na Ant-Biotic lakini bado tatizo liko pale pale.

Naombeni mnisaidie Waungwana nini kifanyike niondokane na hali hii, mahusiano yangu yanayumba...

Nakosa amani, kwa ufupi sina furaha nahisi kukata tamaa kabisa.
 
Pole sana kijana, hapo kweli mahusiano lazima yayumbe.
 
sijui nielezee vipi ila tambua kwenye mahusiano yangu kiukweli ninapitia kipindi kigumu sana imefikia hatua hata mpenzi niliye naye sasa ameanza kunichoka uvumilivu umemshinda anahitaji tuvunje mahusiano yetu.
Polee! I feel it.

Hakikisha unasugua ulimi vizuri na si meno tu. Ulimi unachangia sehem kubwa kuwa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ziko dawa za kinywa nzuri..ntakupa jina lake badaye.

Pia
Baada ya kula tu na kusukutua kinywa unaweza kutumia limao, yan unakamua unakunywa namanisha unakamua hlf unakunywa..kama unasukutua hiv, au kulamba kwa ulimi pia.

Limao linasaidia kuua bacteria hao. Unaeza tumia limao baada ya muda fulani. Ukiulizwa kwanini unatumia limao unaeza sema ni kwa ajili ya kuzuia gesi tumboni kila wakati au tumbo lisikuume baada ya kula.

Wengine wanatumia tangawizi kutafuna kipande kidogo tu nayo inasadia. Ni chungu kiasi ili dawa nzuri tu unaposukutua nayo kinywani. Unaeza tafuna pia baada ya muda fulani.
Zote njia unaweza tumia hata usiku kabla hujalala na asubuhi kupiga mswaki unatumia pia
 
Nilikuwa na hii shida nikiwa sekondari ila shida yangu nikajua ipo sehemu gani.

1. Kama una tabia ya kutafuna vinyama ndani ya kinywa acha, mimi baada ya kuacha niliona mabadiliko makubwa.

2. Piga mswaki kwa dawa ambazo ni herbal. Unaponunua dawa ya meno itazame mwisho kabisa ina alama ipi? Je ni red, blue or green? Tumia saana green maana hiyo natural, red ni chemical na blue ni natural+chemical. Nitaweka picha ya hizi alama.

3. Jizoeze kupiga mswaki kila ulalapo na uamkapo, ata kama ni mchana wewe piga.

4. Kuna maji flani ya kusukutua ktk kinywa, supermarkets wanauza, uwe unatumia mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…