Jamani naomba msaada tiba au dawa gani inatoa harufu mbya mdomoni maana kma mswaki napiga tena sana ni tatizo la muda sana miaka miwili sasa. Nimetumia dawa mbalimbali lakini tatizo bado haliishi, mdalasini asali karafuu nimetumia sana lakini hakuna mabadiliko colgate, forever living , aloevera lakini bado hazisaidii.
Naomba msaada hata wa mawazo jamani siyo dhihaka mswaki napiga sana hata Mara 4 kwa siku lakini bado kunuka mdomo uko pale pale
Pole sana ndugu, Mimi mwenyewe nina tatizo kama lako nimedumu nalo takribani mwaka wa 4 sasa ila nimekuja kugundua chanzo ni kutokupata choo (vidonda vya tumbo) ndiyo chanzo na siyo kingine nilichoamua kufanya ni kubadili utaratibu mzima wa kula.
Yaani kwa ufupi ratiba yangu ipo hivi;
Asubuhi natandika
-chai yenye tangawizi, mdalasini, hiliki na karafu bila kusahau mchaichai(badala ya majani ya chai) , karanga mbichi za kuchemsha, mihogo au viazi vya kuchemsha(kama vitafunwa) matunda bila kusahau maji safi ya uvuguvugu.
Mchana -ugali wa dona, mboga za majani, matunda kwa wingi na maji ya kutosha.
Jioni/usiku - uji mwepesi wa dona, matunda na maji ya kutosha.
Epuka kabisa kutumia vitu hivi.
Vyakula vyenye gesi nyingi (Maharage, kunde mahindi ya kuchoma n.k), malimao, pilipili, nyama, vyakula vya kukaangwa na vyakula vya kwenye makopo (fast foods).
fanya hvyo mfululizo kwa wiki mbili mpaka nne uje ulete mrejesho hapa.
N.b kama bado tatizo litakuwepo fanya ukapime kisukari na magonjwa yanayohusisha mapafu.