Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Kuna watu wanaswaki lakini wanaishia kusugua meno tu, ulimi anaacha,, sugua ulimi kwelikweli tena pale katikati karibia kooo
Sijui mgonjwa ana umri gani, maana mpaka anakuja kuomba msaada hapa, inaonyesha kabla, hakuwa na tatizo hilo, je unadhani amebadilisha namna ya upigaji mswaki.
 
Jitaidi uwe unasugua na ulimi vizuri pande zote..ukisafisha meno pekeee haitoshi..
 
Jamani naomba msaada tiba au dawa gani inatoa harufu mbya mdomoni maana kma mswaki napiga tena sana ni tatizo la muda sana miaka miwili sasa. Nimetumia dawa mbalimbali lakini tatizo bado haliishi, mdalasini asali karafuu nimetumia sana lakini hakuna mabadiliko colgate, forever living , aloevera lakini bado hazisaidii.

Naomba msaada hata wa mawazo jamani siyo dhihaka mswaki napiga sana hata Mara 4 kwa siku lakini bado kunuka mdomo uko pale pale
Pole sana ndugu, Mimi mwenyewe nina tatizo kama lako nimedumu nalo takribani mwaka wa 4 sasa ila nimekuja kugundua chanzo ni kutokupata choo (vidonda vya tumbo) ndiyo chanzo na siyo kingine nilichoamua kufanya ni kubadili utaratibu mzima wa kula.

Yaani kwa ufupi ratiba yangu ipo hivi;

Asubuhi natandika

-chai yenye tangawizi, mdalasini, hiliki na karafu bila kusahau mchaichai(badala ya majani ya chai) , karanga mbichi za kuchemsha, mihogo au viazi vya kuchemsha(kama vitafunwa) matunda bila kusahau maji safi ya uvuguvugu.

Mchana -ugali wa dona, mboga za majani, matunda kwa wingi na maji ya kutosha.

Jioni/usiku - uji mwepesi wa dona, matunda na maji ya kutosha.

Epuka kabisa kutumia vitu hivi.
Vyakula vyenye gesi nyingi (Maharage, kunde mahindi ya kuchoma n.k), malimao, pilipili, nyama, vyakula vya kukaangwa na vyakula vya kwenye makopo (fast foods).

fanya hvyo mfululizo kwa wiki mbili mpaka nne uje ulete mrejesho hapa.

N.b kama bado tatizo litakuwepo fanya ukapime kisukari na magonjwa yanayohusisha mapafu.
 
Kuna mtu ana kaharufu flani yaani uwepo wake unabadili hadi ladha ya mate mdomoni yaani kama uchachu flani au sweet lakini inayokera tena zaidi akiongea.

Wakati mwingine hunuka kama mothballs yaani ile dawa ya vidonge ya mende.

Inasababishwa na nini?Ni specialist doctor wa aina gani amuone?

Matibabu yake yakoje?
 
Habari ndugu...

Ebana nianze kwa kutanguliza pole za uchovu wa mihangaiko ya kila siku.

Leo naomba kujua kuhusiana na tatizo la "kunuka mdomo" hili tatizo husababishwa na nini...? Tina take ni nini...?

Shukrani.
 
1. Inaweza kuwa ni ishu ya usafi wa kinywa. Hii tiba yake ni kubrash/kuswaki vizuri sehem zote za mdomo ukiwemo ulimi, sugua mswaki juu ya ulimi hasa ile sehem inayoelekea kooni kuondoa uchafu unaobakia huko. Utakerekwa kdogo lakin inasaidia sana. Watu wengi huwa wanabrash meno tu wanasahau kuwa ulimi ndo unabaki na takataka nyingi za misosi ambazo zikikaa baada ya muda zinaanza kuleta hiyo harufu mbaya.

2. Ukiona namba moja hapo juu haijasaidia nenda uwaone wataalam wa afya ya meno inawezekana una shida fulani ya kiafya inayosababisha hiyo harufu mbaya.
 
Sidhani kama kupiga mswaki ni suluhisho tosha la hili swala.Ningependa kujua kama kuna dawa yoyote itakayo tumika katika kulidhibiti tatizo ili la kunuka mdomo.

Tafadhali msaada wenu
.
Ni kweli. Sio kila harufu ya kinywa inakuwa initiated katika eneo la kinywa.

Kuna harufu inatokea kooni na chanzo ni kutokea katika njia ya chakula au utumbo.

Hii huwa inatokana na matatizo kama kutopata choo kwa muda mrefu, hivyo zile taka mwili huwa zinaendelea kuwapo katika utumbo na kutoa harufu kali sana ambayo hurudi kinywani.

Dawa hapo ni dawa fulani jina limenitoka ambayo unakunywa usiku wakati wa kulala.... Balaa lake asubuhi..... Utakaga gogo refu na zito kama haujawahi kukata gogo maisha yote..
 
Ndugu nisaidie kufahamu hiyo dawa naweza kuinunua hata leo. Nisaidie
 
Ndugu nisaidie kufahamu hiyo dawa naweza kuinunua hata leo. Nisaidie
Nitakuelekeza ambapo inapatikana.

Nenda pale upanga, mtaa wa mindu (MINDU ST), opposite na jengo la Richmond tower, utaona kuna pharmacy ipo pale kwa chini ndogo hivi ya mzee m'moja wa kihindi, atakuelekeza dawa. Mwambie tatizo lako, mostly inakuwa ni constipation, then ataku guide.....
 
Miaka kumi sasa nanuka mdomo dawa mbali mbali nimetumia sana kienyeji pia za hospital mouthwash mswaki naujua sana meno meupe sana lakni hali bado tete kama kuna mtu alishawahi kupata hili tatizo na akapona basii nahitaji msaada pia hospitali gani bingwa ya kinywa naweza pata tiba ya vizuri NDUGU ZANGU
 
Pole mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au kuna uwezekano ana kamasi (sinus) zinasababisha kunuka mdomo pia
Hii hali inanisumbua kuna kamasi linashuka kutoa kwenye tundu za pua kuja kwenye koo likiwa na harufu kali, wakati mwingine linatoka puani likiwa na harufu kali sana.

Dawa gani nitumie?
 
Back
Top Bottom