Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Kinywa kutoa harufu mbaya Mdomo Mtu mwenye huo Ugonjwa atachukuwa Asali Safi ya nyuki iliyo mbichi haijapikwa, Asali vijiko 2 aikoroge katika maji

na ayachemshe katika moto mdogo mpaka yatoe moshi na avute puani moshi huo mdomoni kupitia kwenye paipu ya (bomba) iliyofungwa vizuri juu ya

chombo. Tiba hii atakuwa akiendelea nayo pamoja na kutafuna nta ya asali. Harufu mbaya ya Mdomoni itaondoka kabisa.

Maji kiasi gani mkuu,na chombo cha kuvutia cha ain gani.
 
Nina tatizo la kutokwa na harufu mbaya kinywani..je nitumie dawa gani ili tatizo langu liishe kabisa..

Pole sana mkuu. Kwa tatizo lako unatakiwa uwe makini wakati unasugua meno. Hakikisha mswaki unapenya sehemu zote zenye upenyo kwenye meno. Ndiyo maana kuna zile nyuzi maalum za kuundoa mabaki ya chakula kwenye meno. Maana yakioza ndiyo husababisha harufu mbaya.

Ndugu MziziMkavu karibu umsaidie zaidi ndugu yetu
 
Last edited by a moderator:
Kuna dawa ya kusukutua hapa Ujeruman ni nzuri kweli ndugu yangu na inauzwa Euro 8 mpaka 10 kila baada ya siku 3 unasukutua hauwezi amini ni kama pafyumu ya mdomo kk ila Umbali unatusumbua kk
 
Mwanangu anatumia vema mswaki kila asubuhi.lakini ukimsogelea anatoa harufu mbaya mdomoni akiongea,hivi tatizo inaweza kuwa nini,na tiba yake ni nini.

nitashukuru wadau
 
Kutoa harufu mdomoni si swala la kutokupiga mswaki tu,wakati mwingine hutokana na kutokula kwa muda mrefu na wakati mwingine inaweza kuwa ni asili ya kwenu
 
Mwanangu anatumia vema mswaki kila asubuhi.lakini ukimsogelea anatoa harufu mbaya mdomoni akiongea,hivi tatizo inaweza kuwa nini,na tiba yake ni nini.

nitashukuru wadau

Mdomoni kuna mengi, glands, mucosas na vingine vingi ambavyo madokta wanajua. Huenda amerithi baadhi ya viengeneza mwili aka vinasaba vya harufu
 
Mpeleke Hospital kisha amwone dentist atamwangalia atakupa jibu sahihi
 
Sio kila wakati mtu akitoa harufu mdomoni inatikana na kinywa chake. Harufu hiyo inaweza ikawa inatoka tumbon.

Nina mdogo wangu alikua na tatizo la kutoa harufu mbaya mdomon akiwa mdogo, tulimbadilishia toothpaste sana na kuhis alikuwa haswak vizuri.

Tulimpeleka hosp mara kadhaa akichekiwa kinywa kiko poa. Ndipo nilipokutana na doct mmoja nikawa namwelezea hilo tatizo.

Akashauri akafanyiwe vipimo vya tumbo. Iligundulika alikua na infection tumbon na baada ya kutumia dawa ile harufu ilikwisha kabisa.

Nakushauri uonane na doct kwa ushaur zaid
 
Nikusaidie number ya Mzee wangu Ana dawa Fulani ukienda atakusaidia Kama uko dar hapa 0656007439
 
Kuna sababu tofauti zinazoweza kusababisha harufu kutoka kwenye mdomo:

Mouth mucosa imejengwa na bacteriaflora wa aina tofauti ambao wanasaidia kulinda eneo hilo kupata infection za aina tofauti.Hawa bacteria flora wanasaidia kuondoa dead cells,na mabaki ya chakula yaliyopo kwenye mdomo na katikati ya meno.Sulphuric gases ndio zinasababisha harufu kwenye mdomo na zinatokana nakuvunjwavunjwa kwa organic materials(mabaki ya vyakula n.k).

Kutosafisha mdomo vizuri na ugonjwa kwenye mucosa ya mdomo inasababisha pia muongezeko wa harufu.
Matatizo mbali ya mdomo pia yanasababisha harufu kama matatizo ya mafigo,matatizo kwenye production ya mate au matumizi ya dawa yanayosababisha kukauka kwa mdomo.Kama mtu ana utapia mlo,kisukari au infection kwenye koo.


  • Mpigishe mswaki na msafishe ulimi vizuri,mabaki ya organic materials kwenye ulimi yanasababisha harufu kwenye mdomo pia !!
  • Kula mara kwa mara insaidia pia kuondokana na harufu.Kwasababu kutokula kwa muda mrefu kunsababisha muongezeko wa harufu.
 
maji kiasi gani mkuu,na chombo cha kuvutia cha ain gan
Paipu ni ni mpira wa

bomba la plastiki dogo Asali safi mbichi ikorege kwenye maji kasi cha glasi 3 kisha chemsha

kwenye moto sio mkali mpaka itowe mvuke weka hiyo paipu bomba la plastiki kwenye hiyo dawa

uvute moshi kama wazee wanavyovuta moshi wa ugolo. uingine puani moshi wako utafanya

hivyo asubuhi na jioni. Na huku ukitafuna nta ya asali kinywa chako harufu kitaondoka. Au Tumia

Dawa nyingine rahisi uwe unakula kila siku Tangawizi mbichi kwa muda wa mwezi mmoja

harufu yote mbaya mdomoni itakwenda zake. tumie kisha uje unipe Feedback.



 

Attachments

  • GINGER.jpg
    GINGER.jpg
    24.2 KB · Views: 183
Utafanyaje sasa mkuu wakati unataka unukie vizuri?
Kuna wakati mwanamke anataka asikie kiharufu cha mumewe cha asili (and vice versa), sasa ukiondoa yote unataka mdomo unukie harufu ya SUPERMARKET muda wote....
 
Kunywa kizibo cha karafuu kila umalizapo kupiga mswaki pia Weka kwny pamba mafuta ya karafuu na kupakaa meno ndani na Nje then acha kipande cha pamba ndani ya mdomo usikimeze kwa masaa 6.
 
Kunywa kizibo cha karafuu kila umalizapo kupiga mswaki pia Weka kwny pamba mafuta ya karafuu na kupakaa meno ndani na Nje then acha kipande cha pamba ndani ya mdomo usikimeze kwa masaa 6.
Mmmmhhh...hapo tu ndipo kwenye utata
 
Dawa ya harufu mbaya ni kusukutua na mswaki kila wakati na pia jitahidi kusafisha mdomo usikae umeufunika mdomo muda mrefu. Ikiwezekana tafunatafuna big G kama uko idle na kila ukitaka kulala piga mswaki na dawa nzuri ili kuua bacteria. mabaki ya chakula na bakteria mdomoni ndiyo yanafanya harufu isiishe.
 
Nina mtoto mdogo waa miaka 4 mwezi huu amekuwa na harufu mbaya mdomoni na anapiga mswaki vizuri but harufu haitoki lakini mtoto akawa amekosa hamu ya kula na akaanza kuloose uzito na kuonekana mdogo.

Akapelekwa kwenye hizi hospitali za serkali akapima mkojo akaonekana ana uti akapata dozi but dogo akaendelea kuluz na harufu kuendelea kutoka.

Tukaamua kumpeleka private akapimwa na akagundulika na uti akapata dozi siku ya pili tuu harufu ikakata na akawa anakula mwenyewe na mwili kuanza kurudi vizuri.

Je, kwa madaktari na wajuzi kuna uhusiano wa UTI na harufu mdomoni hasa kwa hawa watoto?
 
Uti hahusiani kabisa na harufu mbaya , hiyo harufu ilitokana na gum disease ambayo incause fizi kublead kwa hiyo ile damu ikikauka inatioa harufu mbaya na amepona mtoto probably ya zile antibiotic , be careful some drs get careless
 
Back
Top Bottom