Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba

Una aleji na maji

 
Infection kwenye maji - Yamekaa muda mrefu
Aina ya maji -Chemicals ambazo una allergy nazo.
 
Pole sana mkuu kwa hali hiyo. Mimi nilisumbuliwa na hali hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka kumi. Ilikuja kuacha baada ya kuanza kuoga maji ya uvuguvugu na kuacha kujisugua na vitu kama dodoki au jiwe isipokuwa miguuni tu. Pia nikioga nahakikisha nakuwa sehemu yenye joto la kutosha. Aisee hiyo hali inasumbua sana. Solution kamili mpaka sasa sijaipata maana bado hiyo hali haijaacha kabisa
 
Hii ni mojawapo ya dalili za figo kushindwa kufanya kazi.
Waone wataalam wakikague uzima wa figo zako.
 
Taulo likiwa linauvundo yani taulo unapolitumia inabidi liwe kavu haswa,kila utumiapo anika juani
 
Duuh, pole sana mkuu
 
Kwa hiyo mkuu kuanzia uoge maji ya moto hiyo hali iliondoka kabisa?
 
Pole sana ndugu, JARIBU KWENDA KUPIMA LIVER TEST FUNCTION, inaweezekana hepatits A, B, C. n.k, pamoja na figo
 
Sabuni unayotumia inaweza kusababisha kuwashwa Mwili, jaribu kubadilisha sabauni ya kuogea.

Vyanzo vya Maji vinaweza kusababisha kuwashwa kwa Mwili punde unapomaliza kuoga.

Kama ni mtumiaji wa Maji ya moto mara kwa mara, nayo inaweza kuwa ni moja ya sababu ya wewe kuwashwa Mwili.

Taulo unalotumia inaweza ikawa ni moja ya sababu ya wewe kuwashwa Mwili unapomaliza kuoga. Anzisha utaratibu mpya wa kufua Taulo kila unapomaliza kuoga, kama kuna uwezekano jitahidi uwe na mataulo japo mawili nikiwa na maana, taulo utakalotumia kujifutia liwe limekauka, usijifute na Taulo bichi au lenye unyevunyevu.

Kuanzia hivi sasa ninapotoa haya maelezo anza kufanya hivi, usijikaushe unapomaliza kuoga, acha Maji yakukaukie Mwilini, ikiwezekana wewe jikaushe kichwani ikiwemo na uso, pamoja na sehemu za siri tu, sehemu nyingine ya Mwili iache Maji yakaukie Mwilini.

Ukiwa unasubiri mbadala, anza na zoezi hili la kutojikausha Mwili utakuja kunipa marejesho, tatizo limekwisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…