Nini kinasababisha kuwashwa mwili baada ya kutoka kuoga? Tatizo limenisumbua miaka 10 sasa.. Nikijisugua ndo nawashwa kabisa, nisipojisugua nawashwa kidogo afadhali lkn mtu huwezi kuoga bila kujisugua. Najisugulia kitambaa laini kabisa, nikitoka kuoga nachanganyikiwa kwa kuwashwa mno na daktari aliniambia ninywe piriton kila kabla sijatoka kuoga na nikitoka kuoga lkn haikunisaidia kabisa.
Naombeni ushauri nifanye nn manake nimekata tamaa sina raha ya kushika maji hata kidogo. Mvua ikininyeshea nawashwa haswaa. Mwili unatutumka unavimba kila nikijikuna.
Aisee, nimekumbuka mbali sana, huo ugonjwa ulinitesa sana, mpaka nikawa nahisi ninaumwa UKIMWI. lakini kwa sasa nilipona baada ya kupitia mateso makubwa. Ilikua nikitoka kuoga nawashwa mwili mzima, hasa kwenye mapaja na miguu, pia kuzunguka kiuno.
Nilishawahi kuandika tangazo kama hili kuomba msaada wa kupata Ushauri nifanyeje nipate nafuu. Niliambiwa SCABIES kama ulivyoambiwa wewe hapa, nikatafuta hiyo SCABOMA nikawa napaka kila nikitoka kuoga, Pia nilishauriwa nifue nguo zangu zote kwa maji MOTO ili bacteria wa SCABIES wafe, pia nizifungie nguo katika mfuko wa nylon (PLASTIC) ili bacteria wakose hewa wafe hayo yote ninifanya.
Lakin haikusaidia au ilisaidia in long run, yaan labda matibabu hayo yalikua yanasaidia kwa taratibu sana. Mpaka sasa sikumbuki hali ile iliisha lini maana ilikua inapungua taratibu taratibu sana. Nilishaenda hadi kwa wamasai wakanipa dawa za kupaka zina harufu mbaya sana, nilipaka lakini hazikuonyesha kusaidia kabisa.Hata ngozi ya maeneo yaliyokua yanapata adha hiyo ya miwasho haikua na muonekano mzuri, kiukweli niliogopa hata kupima nikajua lazima ntakua VICTIM.
Kuna Siku nikaenda kwenye Hospital moja inaitwa SINO Hospital, ipo SINZA mapambano, kupima full blood picture nione labda Vitu kama CD4 kwa uwelewa mdogo nilionao vinaweza vikanipa picha halisi ya afya yangu, lakin yalitoka fresh, component zote za damu zipo OK.
Wife alipopata ujauzito baada ya kukaa muda mrefu tunapiga gem bilabila, Hatimae akapata Mimba, alivyopima akawa NEGATIVE ndipo nikapata HOPE niko sawa, nami ndio nikaenda sasa Kupima. lakin wakati huo miwasho imeshakwisha. Mwili kuna kipindi huwa unawashwa lakini sio kwa kiwango kile.
Kwa hiyo ndugu mtoa mada, pambana sana. Fanyia kazi ushauri unaopewa hapa, na wewe jiongeze kwa tiba mbadala za mitishamba.