Tatizo la maandishi kujirudia kwenye display, Masada natatua vipi?

Tatizo la maandishi kujirudia kwenye display, Masada natatua vipi?

At Calvary

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
4,533
Reaction score
3,595
Jambo wapendwa wa jamii forum. Ni matumaini yangu mko poa wote, kwa wenye changamoto nawaombeeni kwa Mungu awafanyie wepesi.

Moja kwa moja kwenye mara. Karibuni nimekuwa nikipata uzoefu mbaya katika utumiaji wa simu yangu. Iko hivi mara kwa mara nikiwasha simu kama ilikuwa imelala imekuwa ikileta mistari mistari au kama kujirudia rudia kwa chochote kionekanacho kwa kioo, kunakuwa na rangi ya grey, ila baada ya muda kunakaa sawa.
Nimejaribu kusolve kwa njia tofauti lakini tatizo halijaisha, nilifanya update ila mambo Bado.
Kwa yeyote anaeweza kufahamu chanzo cha tatizo na njia ya kutatua naomba anisaidie nimekwama.

NB: Simu ni Redmi 12C ina miaka 2 kasoro. Ila mwaka Jana mwezi wa 9 ilipata mpasuko kidogo. nimeendelea kuitumia vivyo hivyo, sijaiweka screen protector wala cover.

Msaada Kwa yeyote afahamuye. Natanguliza shukurani.
 
Search kwenye YouTube kuna video nyingi zinaelezea jinsi ya kusolve tatizo hilo
 
Huo mpasuko sio ndio source ya kitu hicho? Yng ilipasuka kdg baada ya hapo ikawa inaonyesha kwny kioo utazani ni hitachi ya kizamani ukiwa una rewind mkanda kwny deki
 
Huo mpasuko sio ndio source ya kitu hicho? Yng ilipasuka kdg baada ya hapo ikawa inaonyesha kwny kioo utazani ni hitachi ya kizamani ukiwa una rewind mkanda kwny deki
Huo mpasuko unazaidi ya mwaka.

Inakuja na kupotea.
 
Back
Top Bottom