Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Jamani mimi nakaribia kuchanganyikiwa.Tatizo ni kuwashwa ngozi ya korodani. Yani ikichachamaa ukianza kuzibinyabinya hutoi mkono.Ngai!

Nimishawaona madaktari wa ngozi, nimepewa vidonge, za kupaka na hata sindano.Utapozuga kupoteaa kisha unarudi.Kuna muda ngozi ya pumbu inakuwa kama ya kenge kabisa, inatoa ungaunga.

Ugonjwa umenipa adabu, ninapasi boxer, nina taulo maalumu za kujifuta pumbu tu.Nina boxer za wiki nzima, ninavaa boxer moja kwa siku. Taulo na boxers zinaanikwa juani. Kunyoa kila wakati kama mdada, nikiacha tuvuzi tu nitakoma.

Jamani nifanyeje? Nadata kabisa
 
Kama unatatizo la Fangasi za Muda mrefu au Muda mfupi kwenye Nyeti zako (Corodani, Mapaja, na Jogoo) basi dawa yako ni hii 👇

Kanunue Vidonge vya Vitamin B Complex (Vit. BCO) then kwa siku 3 za mwanzo kunywa Viwili asubuhi na Viwili jioni (2×2).
Baadae kwa Muda wa Siku 14 kunya Vidonge 2 kwa siku.
Kama hajijapona endelea wiki moja zaidi, kama zimepona na kuisha basi sitisha kwa siku 30 ikisha kunywa tena siku 7 kwa Vidonge 2 kwa siku.
Fanya hilo zoezi kwa Muda wa wastani wa miezi 6 utakuja kunishukuru.

ANGALIZO:
  1. Hii dawa haijatengenezwa kwa ajili ya Kutibu Fangasi, lakini matokeo ya Wanywaji wake yameonesha inatibu Fangasi kwa ufanisi Mkubwa zaidi kuliko zile dawa zenyewe za Fangasi.
  2. Epuka kuvaa Boksa/Chupi za kubana hasa kama unaishi maeneo yenye Joto kama Dar au Zanzibar.
  3. Usafi wa kila siku unahitajika.
Usisahau kuleta Mrejesho hapa.
 
Ukimumwa huo muda ni mchache sana.
Mhhh navyojua mbona kuna tiba za wiki moja tu baada hapo uwe msafi/mkavu muda wote

Haina madhara kuitumia muda mrefu hivyo?

Naona heri kuboresha 'lifestyle' kwa ujumla for the long run
 
Mhhh navyojua mbona kuna tiba za wiki moja tu baada hapo uwe msafi/mkavu muda wote

Haina madhara kuitumia muda mrefu hivyo?

Naona heri kuboresha 'lifestyle' kwa ujumla for the long run

Hujapatwa na maambukizi ya Fungus ndiyomana ukasema maneno hayo.

Wengi wa Watu ambao hawajawahi kupata Fungus wanaishia kuwasimanga waliopata maambukizi ya Fungus kuwa ni Wachafu. Huu ni uongo na udhalilishaji! Fungus ni maambukizi kama maambukizi mengine, yakikukuta haijalishi kuwa wewe ni msafi au mchafu.

Dawa nyingi za kutibu fungus let say Whitefield's Ointment, Clotrimazole cream, Griseofulvin na nyenginezo unapotumia zinaondosha fungus kwa kipindi kile tu unachotumia, hivyo kwenye wiki moja unaweza ona umeshapoa lakini ukimaliza dawa baada ya wiki 2 au 3 fungus zinajitokeza tena wala haijalishi usafi wako.

Mimi niliugua Fungus kwa zaidi ya miaka 11 nikamaliza takriban dawa zote lakini mwisho wa siku Vidonge vya Vitamin B Complex ndiyo vikaniokoa.

Enewey! Katika dawa zenye sumu zaidi ni Ant-TB (RH na RHZE) lakini Watu wanakunywa Vidonge 112 kwa mwezi kwa muda wa miezi 6 na wanaishi viziri tu.
 
Hapa kwa usahihi ni bora ule vyakula vinavyoleta vitamini B's mwilini, B1, B2,B5,B6,B12 nk.
 
Dawa hii inatibu na kifua pia
 
Poleh sana

Sina maana hio dear i know inakua so uncomfortable
Nishawahi ugua pia zamani na mi ni msafi sana sikuzote hadi nikawa najiuliza nakwama wapii

ila nilipata tiba ya wiki moja baada ya hapo nkapunguza vyakula vya sukari na kuboresha kukaa mkavu muda wote (mi na tissue tissue na mimi i must stay dry 24/7) na cotton underwear tu hicho ndo nilikua sizingatii

Hadi leo ishakua historia

Hivyo fatilia lifestyle pia
Na kulala bila nguo ya ndani usiku is a big bonus pia
 
Hellow wadau!


Ndg yangu anasumbuliwa na fangasi ukeni kwa muda mrefu, ametumia anibiotics mbalimbali na dawa nyingine nyingi zikiwemo za kuinset ukeni lakini hajapata nafuu kwa maana ugonjwa huwa unaondoka na baada ya muda unarejea. Na hili limewahi hata kusababisha ujauzito kutoka.

Naomba msaada ni wapi tunaweza pata mtaalamu wa kumaliza tatizo hili sugu kwa ndugu yetu maana tulianza zahanati mbalimbali za hapa tunapoishi, hospitali ya rufaa mkoa na hata baadaye tulisafiri hadi Regency hospital Dar es Salaam na bado tatizo hili halijakwisha.

Tafadhali tunaomba msaada.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…