N'na tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa fangasi sehemu za siri na nimetumia dawa nyingi za hospital bila mafanikio.
Pole sana. mbali na njia njinginezo ambazo mtu waweza kupata fangasi,vitu kama
1: kushare mataulo,
2: kutokujikausha vizuri unapotoka kuoga,au haja ndogo/kubwa.
3:kutokumwaga maji ya kutosha unapoenda kutumia choo(kumbuka kama wewe ni msichana hakikisha unamwaga maji ya kutosha unapoenda chooni iwe haja kubwa au ndogo hata kama unaona choo lulichoingia ni kisafi kwa macho kwa sababu mtu akishatumia choo hata tu ile kukojoa mkojo mdodo sana kama vijiko viwili, kama ana fangasi na hakusukuma mkojo wake vizuri ni rahisi sana utakapotumia na wewe kuondoka na bacteria hao.
4: kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri
5: kutumia taulo muda mrefu bila kulifua( kumbuka kupiga pasi taulo unazotumia na hakikisha hutumii mataulo ya kwenye mahoteli kwa hiyo unaposafiri beba taulo lako.
6: kuchangia soap dish(ni vyema ukajitegeme kifaa chako cha kuwekea sabuni zako za kuogea(kama ni mwanamke na una familia wengine wanaweza wasikuelewe,lakini kumbuka kila mtu anapoingia bafuni ana ustarabu anaoujua yeye wa kutumia vifaa vya bafuni so bora ujikinge hapa.
7: kutumia ndoo za kupigia deki kwa kuogea
8: kutumia muda mrefu pedi za kujisitiri siku za heshima kwa msichana
9: kukaa muda mrefu na nguo ya ndani bila kubadilisha n.k n.k
nakutakia matibabu mazuri upone na hizo fangasi zizirudi tena.