Bray...Fungus wanapokuwa sugu kwa dawa za kupaka unaweza pia tumia combination ya dawa za kupaka na kumeza (vidonge), huwa matokeo yana kuwa mazuri zaidi.
Pia kama unatumia dawa ya kupaka yenye 'steroid' unaweza pata tatizo la usugu wa fungus...steroid ikitumiwa kwa muda mrefu huwa na tabia ya kushusha immunity locally eneo hili inapopakwa, na ndio eneo hilo lenye fungus..na hivyo kuongeza tatizo zaidi ya kulipunguza au kulitatua.
Pia , kwa vile fungus wako ni wa sehemu za siri..inawezekana kuwa unapata re-infection kwa sababu ya nguo zako za ndani kama hazioshwi vizuri. Nakushauri usivae chupi moja kwa muda mrefu, kwa siku badili chupi angalau mara 2 hadi 3, na kila ukivua ufue kwa antiseptic (dettol), anika zikauke kabisa na ikiwezekana zipasi ili kuua spores za fungus ambazo kwa kweli ni taabu sana kuziua.
Zingatia hayo na nina hakika tatizo lako litaisha.