Tatizo la magaga au makenya

Quetzal

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
6,343
Reaction score
10,799
Habarini,

Nimekua nikisumbuliwa na magaga kwa.muda Sasa..nimesugua na msasa wapi ..nikasugua na jiwe Bado Hali ni.ileile.

Kuna muda yanauma kabisa especially nikishasugua na jiwe.

Je Kuna Dawa inaweza nisaidia hili Tatizo.

Wassalam

Mrejesho
..Nilinunua footcream ambayo imesaidia kutibu Magaga kwa asilimia kuubwa Sana.

Asante
 
Tatizo hilo linasababishwa na ngozi ya kisigino kuwa kavu na hilo linaweza pia kuwa linachangiwa zaidi kama unatumia viatu vya wazi kwa mda mrefu kwahio inakuwa rahisi upepo na vumbi kuifanya ngozi ya miguuni kuwa kavu:

Cha kufanya:
Kila Siku kabla ya kulala Chukua maji ya vuguvugu changanya na Chumvi au Limau kisha loweka miguu yako humo kwa dakika 20 huku ukisugua miguu yako kwa jiwe laini.

Baada ya kumaliza paka mafuta ya Nazi miguuni yakolee vizuri kisha vaa soksi ulale nazo.

Kama unaweza kwa kipindi hiki cha tiba vaa viatu vya kufunika ila kulinda visigino na ukavu na vumbi mpaka magaga yatakapoisha.

Kama hutaweza basi jitahidi pia asubuhi upake mafuta ya kutosha kwa ajili ya kuifanya ngozi isiwe kavu.

Fanya zoezi hilo kwa uaminifu mpaka magaga yatakapoisha.
 
Asante Sana.... Ntalifanyia kazi
 
Pendelea kuvaa viatu vya kufunika ikibidi acha open shoes kbs hadi uwe sawa

Usiku oga paka lotion kwenye visigino afulala na socks

Msasa usitumie kupitiliza

Ni ishu nyepesi sana
 
Ooooh.... Sasa nmeanza kuelewa tatizo ni nini. Nlikuwa najiuliza....kwa hali hii ni sawa kabisa ulichosema. Na hayo huwa yanakuwa hadi kwenye ubongo...

Habarini,

Nimekua nikisumbuliwa na magaga kwa.muda Sasa..nimesugua na msasa wapi ..nikasugua na jiwe Bado Hali ni.ileile.

Kuna muda yanauma kabisa especially nikishasugua na jiwe.

Je Kuna Dawa inaweza nisaidia hili Tatizo.

Wassalam
 
Ooooh.... Sasa nmeanza kuelewa tatizo ni nini. Nlikuwa najiuliza....kwa hali hii ni sawa kabisa ulichosema. Na hayo huwa yanakuwa hadi kwenye ubongo...
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]....Magaga na ubongo kumbe Kuna uhusiano?... Aiseeee Sio Tatizo lako ni matatizo yako ya Akili.
 
Pendelea kuvaa viatu vya kufunika ikibidi acha open shoes kbs hadi uwe sawa

Usiku oga paka lotion kwenye visigino afulala na socks

Msasa usitumie kupitiliza

Ni ishu nyepesi sana
Thanks...Japo ninatarajia kununua Feet cream...nione itakuwaje
 
Baada yakunawa miguu.

Paka haya mafuta wakati wa kulala au ukiwa na muda kisha vaa soksi. Wiki mbili tu tatizo litapungua au kupotea kabisa
 
Nunua pumba ya mahindi fresh mashineni ifunge miguuni kwa mifuko ya nailoni kwa siku tano.
 
Nunua pumba ya mahindi fresh mashineni ifunge miguuni kwa mifuko ya nailoni kwa siku tano.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]...Mkuu hili nalo jipya.

Nimenunua cream nanimepata matokeo chanya
 
Duuh!! Pole mleta uzi mana nimeona uzi mungine tena unalalamikia tumbo lako kwamba ni kubwa na unahitaji namna ya kulipunguza.

Kila la kheri katika kuyapatia ufumbuzi.
 
Duuh!! Pole mleta uzi mana nimeona uzi mungine tena unalalamikia tumbo lako kwamba ni kubwa na unahitaji namna ya kulipunguza.

Kila la kheri katika kuyapatia ufumbuzi.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]...nikileta yote yanayonisibu humu...Basi mtakuwa mnani quote TU..hayo Ni machache...Tu kati ya yanayoniandama...ila Magaga yamenpona...asante
 
CreditAnalyst,kitambi wewe,magaga wewe?, Pole sana aisee.Mimi nahisi mbinu za kukwepa mtongozo
Mkuu...na magaga yangu na tumbo langu...natongozwa viZuri TU...

Wewe tafuta wasio na kasoro wapo wengi TU....

N.b magaga yamepona jamani...khaaa
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]...nikileta yote yanayonisibu humu...Basi mtakuwa mnani quote TU..hayo Ni machache...Tu kati ya yanayoniandama...ila Magaga yamenpona...asante
Jengine lipi..? Kama ni lakuonekana nionyeshe..😉😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…