Tatizo la maji limetatuliwa, la umeme litakwisha karibuni na miradi mingine yote inakamilishwa. Watanzania tuunge mkono juhudi za serikali yetu

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Serikali ya awamu ya sita haijawahi kupumzika katika kutatua kero za Watanzania, tatizo la maji lililokuwa limetokea hivi karibuni hasa kwa Wakazi wa Dar Es Salaamu limetatuliwa kwa asilimia 100, tatizo la mgao wa umeme liko mwishoni kuwa historia, kila kitu kinahitaji muda na fedha.

Watanzania tuendelee kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita, miradi yote ya maendeleo iiliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeanza kutekelezwa, fedha zimeshapelekwa, miradi iliyokuwa imeanza kutekelezwa miaka ya nyuma hakuna mradi hata mmoja uliosimama.

Ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mwendo kasi, madaraja, vivuko, SGR, JNHPP, Ujenzi wa madarasa, ujenzi wa mabweni, ujenzi wa nyumba za Watumishi, Ujenzi wa majengo ya kiutawala, miradi ya kilimo etc.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, iko kwa ajili ya Watanzania na ni ukweli usio pingika awamu hii hali ya Demokrasia ni ya juu kabisa, ndio maana kila mtu yuko huru kutoa maoni na akasikilizwa. Tatizo la vijana wengi wanaamini kutukana na kukosoa tu ndio kutoa maoni.

Tuipende Tanzania yetu, tuunge mkono juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
 
Watanzania tuendelee kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita, miradi yote ya maendeleo iiliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeanza kutekelezwa, fedha zimeshapelekwa, miradi iliyokuwa imeanza kutekelezwa miaka ya nyuma hakuna mradi hata mmoja uliosimama ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mwendo kasi, madaraja, vivuko, SGR, JNHPP, Ujenzi wa madarasa, ujenzi wa mabweni, ujenzi wa nyumba za Watumishi, Ujenzi wa majengo ya kiutawala, miradi ya kilimo etc.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, iko kwa ajili ya Watanzania na ni ukweli usio pingika awamu hii hali ya Demokrasia ni ya juu kabisa, ndio maana kila mtu yuko huru kutoa maoni na akasikilizwa. Tatizo la vijana wengi wanaamini kutukana na kukosoa tu ndio kutoa maoni.

Tuipende Tanzania yetu, tuunge mkono juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
 
Ishu ya Maji muiache. Ni mvua ndio zimetuonea huruma. Mindu dam na visima Kigamboni mnamuibia maza tu.
 
Mpumzisheni Mama, mnamwibia sana.2025 si mbali.
 
Nani kalitatua?

Sema tumshukuru Mungu kwa kutufanyia wepesi na kuamua kutetea watu wake kwa kuleta Mvua.

Viongozi wetu tuliowaamini wameshindwa kutumia maarifa na rasimali tulizobarikiwa kila mahala kutatua kero na kufanya wepesi kwa wananchi.

Suala la umeme toka uhuru tunapiga sarakasi mpaka leo.
 
Watanzania tuendelee kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita, miradi yote ya maendeleo iiliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeanza kutekelezwa, fedha zimeshapelekwa, miradi iliyokuwa imeanza kutekelezwa miaka ya nyuma hakuna mradi hata mmoja uliosimama.
Mradi wa bwawa la umeme nasikia mkandalazi mmempatia bil 134 Tshs kama asante, na mmekubali mradi huo uchelewe kwa miaka 2 - tunaomba majibu ya kina.
 
Tatizo la maji limetatuliwa au ni kwa sababu mvua zimeanza kunyesha, umeme nao tunatarajia hali kuwa shwari kwa sababu mabwawa mda si mrefu yatatengamaa kwa sababu za mvua basi, hakuna kitu serikali ya ccm inaweza kukifanya kwa 100%
 
Sio kweli mkuu Glenn
Mkuu nyie hamuoni kasoro wala hamuumizwi na haya ndio maana mnasifu na kusujudu tu.
Inyeshe isinyeshe, umeme uwepo usiwepo.

Ninyi mkipiga goti kusujudu tu asali inawaminikia.

Tunalalamika sio kwa chuki bali kukosa umeme na maji mnatupiga kwenye mshono wakuu
 
Mradi wa bwawa la umeme nasikia mkandalazi mmempatia bil 134 Tshs kama asante, na mmekubali mradi huo uchelewe kwa miaka 2 - tunaomba majibu ya kina.
Acha kusikiliza maneno ya mtaani, ni wahuni tu wanazusha, mradi unaendelea vizuri, watu wako kazini mpaka dakika hii..
 
Serikali ya awamu ya sita haijawahi kupumzika katika kutatua kero za Watanzania, tatizo la maji lililokuwa limetokea hivi karibuni hasa kwa Wakazi wa Dar Es Salaamu limetatuliwa kwa asilimia 100, tatizo la mgao wa umeme liko mwishoni kuwa historia, kila kitu kinahitaji muda na fedha.

Watanzania tuendelee kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita, miradi yote ya maendeleo iiliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeanza kutekelezwa, fedha zimeshapelekwa, miradi iliyokuwa imeanza kutekelezwa miaka ya nyuma hakuna mradi hata mmoja uliosimama.

Ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mwendo kasi, madaraja, vivuko, SGR, JNHPP, Ujenzi wa madarasa, ujenzi wa mabweni, ujenzi wa nyumba za Watumishi, Ujenzi wa majengo ya kiutawala, miradi ya kilimo etc.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, iko kwa ajili ya Watanzania na ni ukweli usio pingika awamu hii hali ya Demokrasia ni ya juu kabisa, ndio maana kila mtu yuko huru kutoa maoni na akasikilizwa. Tatizo la vijana wengi wanaamini kutukana na kukosoa tu ndio kutoa maoni.

Tuipende Tanzania yetu, tuunge mkono juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Unaonekana ni kama mtu mzima kumbe ni kasha tu la mautumbo na makorokoro mengine linalomiliki smartphone yenye uwezo wa kuingia JF
 
Back
Top Bottom