Tatizo la mapafu kujaaa maji husababishwa na nini?

Baba Kenzo

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2017
Posts
224
Reaction score
149
Habari wadau wa mijadala !!!
Ninajambo la kiafya linanitatiza sana japo mie si muathirika wa jambo hilo.
Tatizo la mapafu kujaaa maji linasababishwa na nn?? Au ndo unywaji maji kupita kiasi?? Na nikiwango gani cha maji yanaitajika kwa siku mwilini yaani binadamu anashauriwa kunywa kiasi gani kwa siku???
 
mapafu kujaa maji husababishwa sana na matatizo ya moyo!ingawa kuna vyanzo vingine vya tatizo hili
 
Matatizo ya moyo
Matatizo yafigo
Matatizo ya INI
Nimonia
Matatizo ktk pulmonary..

Mkuu zipo nyingi.ila izo juu ndio common.
 
Kuto tibiwa vichomi kwa muda mrefu,kutumia air condition kwenye magari kwa muda mrefu,kuendesha pikipiki kifua wazi ,TB nayo inachangia sana .mkuu cha kufanya nenda hosp wakafanye yafuatayo.underwater seal drainage au thoracentesis pia dawa hizi hapa utatumia utapona tablet Lasix 40mg od 1/12,tabs spironolatone 50mg od 1/12,tabs predinisolone 20mg bid 5/7, 15mg bid 5/7, 10mg bid 5/7 , 5mg bid 5/7, 5mg od 5/7 .ukifanya hivo utapona tuu Nina miifano mitano na watu wamepona
 
mkuu umemwona mgonjwa mwenyewe? ume- confirm anachoumwa ni nini? umri wake je? medical history yake?
what if yuko contraindicated na dawa fulani hapo...??
 
kama wewe sio muathirika basi usiwe na shaka, we kunywa maji kadri uwezavyo wala haina shida.
 

1. Kifua Kikuu/Nimonia
2. Magonjwa ya Moyo [Heart Failure]
3. Saratani ya Mapafu [Lung Cancer]
4. Ugonjwa wa figo [Chronic Kidney Failure] n.k.....
 
Msisahau wale wanaofanya kazi za migodini ( zihusianazo na milipuko )
Katika ulipuaji kuna gas sumu inaitwa nitrogen dioxide. Hii pia husababisha flooding of the lungs.
Utahitaji kuzingatia namna salama ya kufanya kazi za milipuko
 
Wrong! wrong! wrong! wrong .... !! Sio rahisi hivyo , huwezi kutibu hivyo bila kujja chanzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…