Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Habarini Ndugu zangu.....naomba msaada kwa anaejua hili

Nilijifungua kwa operation sasa baada ya operation nikawa nachomwa sindano za kupunguza maumivu kwenye mapaja sikumbuki idadi ya sindano. Sasa ni miezi mitatu imepita paja nililochomwa sindano limepata ganzi afu kuna muda nasikia kama sindano zinanichoma kama vile nilivokuwa nachomwa ndo nasikia ivo. Hichi kitu kinaninyima raha maana kila siku zinavyozid kwenda tatizo linazidi kuwa kubwa kila mara hiyo hali inajirufia.

Nilishauliwaa niwe najikanda na barafu nimefanya ivo ila bado hamna mabadiliko.

Msaada please kwa anaejua.
Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba pitia hii link inaweza kukusaidia hilo tatizo huitwa gangery
 
[emoji256]MATATIZO YA GANZI MWILINI NA MIGUU KUWAKA MOTO NA KIHARUSI: #SOLUTION

[emoji736]Ganzi ni moja ya tatizo/ugonjwa unaowakumba watu wengine sana na ni tatizo ambalo linakera sana kwa sababu hata unapoenda hospitali Mara nyingi hawapati tatizo lolote

CHANZO CHA TATIZO HILI

[emoji736]UMRI
Kawaida mtu anapokua umri umeenda, mwili mzima uzeeka pamoja na mfumo mzima wa damu, hii husababisha mishipa midogo midogo ya damu kufa, au kuziba hii husababisha chakula na hewa ya oksijeni kutofika kwa ufasaha maeneo ya mbali kama miguuni na vidoleni hali hii hupeleekea mishipa ya fahamu kukosa chakula na hewa safi hivyo ganzi hutokea

[emoji736]:KISUKARI
Sukari inapokua nyingi kwenye mzunguuko wa damu hupelekea kuunguza mishipa ya damu halo hii husababisha mishipa kusinyaa ambalo hupelekea hewa ya oksijeni na chakula kutofika kwa ufadsaha maeneo ya mbali sana kama miguuni na mikononi hali hii husababisha mishipa ya fahamu kukosa chakula na hewa hivyo husababisha ganzi

[emoji736]MAFUTA MENGI MWILINI
Mafuta kujaa kwenye mishipa ya damu inapelekea damu kutokuweza kupita MTU kupata tatizo LA ganzi kwa ni husababisha kutofika kwa damu kwenye mishipa midogo midogo ya damu hii hupelekea ganzi pia

TIBA YA GANZI IPO NI STROKE OIL
Je? , umasumbuliwa na ganzi au jamaa yako anasumbuliwa na ngazi hadi kusindwa kufanya kazi zao.... Jipatie
#STROKEOIL : 10000TSH chupa 100ml

HUDUMA ZAIDI USISITE KUPIGA SIMU
+255684765575
1649109392031.jpg
 
Nada7 naomba msaada juu ya hili la visigino kuuma sana hasa napoamka na kukanyaga chin kwa mara ya kwanza kwa siku hyo, then baada ya hapo maumivu huenda yakipungua had kuisha kabsa au kuyahisi kwa mbali......hali hii imenichukua miez 2 na wiki kadhaa had sasa tangu imenianza.......
 
mimi miguu inaumwa mara kwenye mapaja mara kwenye visigino ila haiwaki moto tatizo linaweza kuwa nini na nitumie tiba gani
 
Kuna ndugu yangu anaumwa ugonjwa kama huu wa miguu kuwaka moto
 
Nilikuwa na huo ugonjwa zaida ya mwaka
Ulianza kama masihara baadae ukaongezeka
Nashukuru kupitia jamii forum doctor nimepata maarifa kidogo
Nikaenda google kikaongeza upeo kidogo hivi sasa namshukuru m , mungu nimepona kabisa na nimejitibu mwenyewe kwa kusoma soma tu mitandao..
Ulitumia dawa gani mkuu
 
Baadhi ya Tiba

Limao

kuhusu limao, mhusika anapaswa kuosha miguu na nyayo kwa maji ya moto na sabuni na baadaye kukata limao katika vipande viwili kisha kupaka sehemu zile ambazo huwa unahisi kama kuungua.

Maji ya uvuguvugu /chumvi.
Wakati umekaa, tumbukiza miguu ndani ya maji ya uvuguvugu, yaliyoongezewa na chumvi ya mawe yakiwa ndani ya karai kwa muda wa nusu saa, lakini wakati umetumbukiza miguu unakuwa unaosha sehemu ambazo huwa unajihisi kuwaka moto.

Msubili
Osha miguu na nyayo kwa maji moto na sabuni, kisha pondaponda jani la msubili na upake sehemu zote unazojihisi kuungua.
Huu msubili ndio mti gani mkuu?
 
Wadau nawasalimu
Naomba msaada nina tatizo la Tumbo kuunguruma chini ya kitovu na pia kutokupata choo kwa wakati je hali hii husababishwa na nini na Tiba yake ni ipi?
 
Wadau nawasalimu
Naomba msaada nina tatizo la Tumbo kuunguruma chini ya kitovu na pia kutokupata choo kwa wakati je hali hii husababishwa na nini na Tiba yake ni ipi?

XIANHE by Nature :
Tumbo kuunguruma au kutopata choo kwa wakati , hilo tatizo hutokana na Liver & Gallbladder system energy stasis

Mfumo wa Ini ndio hu control nishati mwilini ,
Pia husaidia umeng’enyaji wa chakula na kusaidia Mifumo mingine kufanya Kazi kwa usahihi ,
Ukiona tumbo linaunguruma, Maumivu ya kuhamahama, Maumivu ya Tumbo chini ya kitovu ( sore pain ), Acid reflux , Choo kigumu kabisa , choo kigumu mwanzoni n.k
Then tatizo ni nishati ya mfumo wa Ini kuwa Nishati Yabisi

Katika XIANHE treatment plan , lazima ku smooth Liver & Gallbladder system energy stasis , kuwezesha nishati kwenye mfumo kuwa sawa hivyo kuwezesha mfumo wa digestion kukaa sawa , na tatizo hilo litakuwa limeisha !
Tupigie dawa zipo ni asili kutoka Marekani ,

Hakuna tatizo la kiafya lisilopona , kila ugonjwa una kanuni yake ,na mfumo uliposhika na athari zake , na umri wa mtu husika pia hali ya hewa ikoje , so tunazingatia vitu vingi sana kwenye matibabu yetu ,

Hakuna ugonjwa usiopona , ukiona huponi basi Treatment formula iliyotumika sio sahihi !
Cont : +255757577995
a1e8db8d-bb88-4a80-998f-785c78412ba9.jpg
 
Body mass index yangu ni 36,Nahitaji kujua pia ni aina gani ya mazoezi nahitaji kufanya, Kwani physician wamenishauri nisianze mazoezi makali kwanza.

Nimewaona wataalam mbali mbali na dawa nimetumia lakini nafuu haipo kabisa.
kwanza nikupongeze kwa kutatua tatizo ilo kwa sasa. BMI ni uwiano wa uzito na urefu. kwa hiyo BMI yako uko kwny risk ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa ambayo kwa sasa yanaonekana kuwa hatari kuliko hata ya kuambukizwa Mfano ata kisukari hiyo ni moja ya dalili zake. Obvious urefu huwezi kuongezeka kwa sasa, ko inabidi upambane kupunguza mwili kwa ushauri wangu waone watu wa physio, pia kuna applications mtandaoni zitakusaidia.
 
Pole sana mkuu , hilo tatizo ni kweli lipo nalinatokea wakati unapolala linaitwa sleep paralysis (SP) stayle ya kulala mfano supine position , kuwa na wasiwasi sana(execess stress),unywaji wa pombe au madawa ya kulevya .

wakati unapokuwa umelala utendaji wa shughuli wa nerve za nnoradrenergic au serotonergic kwenye sehemu ya ubongo inayohusika na usingizi (pons na pia sehem zingine za brainstem structures) zinapungua kufanya kazi au kuzuiwa kwahiyo misuli inapunguza kazi yake(loss of muscle function) na kusababisha mkono au kiwilili cha mwili au miguu kuparalys na pia hali hii huambatana na ndoto inayomfanya mgonjwa kuhisi na kuona kitu kama kimemkaba au kimembeba wengine wanaita jinamizi, (hallusination) .

pia hali hii hutokea kwasababu ya damu kupungua kufika kwenye mkono na kufanya misuli isipate oxygen na kufanya ipunguze kazi yake ,kwa namna nyingine tatizo hili huwa kubwa zaidi kunapotokea damage ya spinal nerve
View attachment 48274

kwa sababu tatizo la SP huwa ni tempo yaani wakati wa kulala au kuamuaka ,ukiamka na kutembea hupotea kama mpaka sasa linaendelea basi inabidii uende hospitalini kwaajili ya uchunguzi kama la kuja na kupotea basi epuka visabishi kama unywaji wa pombe au madawa ya kulevya , badilisha style ya kulala , na punguza wasiwasi
Mimi nnamauimivu ya miguu kama mwaka au zaid na mara nyengine nnapoanza kulala naskia kama vitu vinatembea kwenye miguu nshafanya vipimo vingi vyote viko fresh kati sehem nlizopita kuna sehem nlipewa amitripyline na gabapentin kwa mwezi ! Nkila dawa zikiisha tu maumivu yanarudi
 
kwanza nikupongeze kwa kutatua tatizo ilo kwa sasa. BMI ni uwiano wa uzito na urefu. kwa hiyo BMI yako uko kwny risk ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa ambayo kwa sasa yanaonekana kuwa hatari kuliko hata ya kuambukizwa Mfano ata kisukari hiyo ni moja ya dalili zake. Obvious urefu huwezi kuongezeka kwa sasa, ko inabidi upambane kupunguza mwili kwa ushauri wangu waone watu wa physio, pia kuna applications mtandaoni zitakusaidia.

Pole sana , katika elimu asili Uzito / BMI Kama unazidi au unaelekea obesity, tatizo lake ni ulaji wa chakula usio sawa na kutengeneza BLOCKAGE ,kusababisha overweight, Usitumie dawa za kupunguza hamu ya kula kwa sababu zitaharibu digestion system kusababisha matatizo makubwa zaid ,
Unachotakiwa kufanya ni kuzingatia muda wa ulaji wa vyakula

Fanya yafuatayo:
1. Kunywa chai [emoji477]️ 9:00 am
2. Kula chakula cha mchana 3:00 pm
3. Jioni tumia chakula chepesi sana au matunda tu saa 7:00 pm , usile chakula chochote zaidi ya saa 8:00 pm

Zingatia unapokula usishibe sana , yaani ukihisi kushiba tu then acha kula , Halafu ukishakula usile tena mpaka muda ukifika , yaani usile mara kwa mara !

MAZOEZI :
Inategemea umri wako , lakini kwa ujumla fanya mazoezi ya kutembea kwa Kasi Kama km 8 kwenda na kurudi , kila asubuhi au jioni

UNYWAJI WA MAJI :
Punde unapoamka tu bila kupiga mswaki , kunywa maji angalau lita 1 , hii itasaidia kulainisha nishati ya mwili !

Au kwa ushauri zaidi na matibabu kwa njia ya Natural medicine , pamoja na FOOT MASSAGE au CHIROPRACTIC,
Karibu tupo Mtongani mtoni Sokoni ghorofani

Appointment
+255757577995
a1e8db8d-bb88-4a80-998f-785c78412ba9.jpg
 
Lyrica tablets , neurobion tablets , amitriptyline tablets, Lexapro tablets , tranmed capsules, pristiq XR . Ila dawa hizi zitakuepo Tanzania Kwa trade mark nyingine. Mimi nilikuwa natumia nikiwa Thailand nilitibiwa na neurologist Dr Yuthana Huahin Bangkok hospital .
Ulipona mkuu
 
Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.

View attachment 367274

Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.

Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.

Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.

WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.






Ushauri, Kinga na Tiba...






Mrejesho/Ushuhuda

Miguu kuwaka moto​


miguu kuwaka moto


ganzi mguuni

Nini maana ya miguu kuwaka moto?​

Miguu kuwaka moto ni tatizo kubwa sana kwa sasa. Maumivu haya yanaweza kuwa ya mda mfupi au yakakaa mda mrefu bila kuisha. Miguu yako itahisi hali ya kuungua na kufa ganzi. Maumivu huwa makali sana hasa nyakati za usiku.
Matibabu ya changamoto ya miguu kuwaka moto yanategemea na chazo cha tatizo lako. Endelea kusoma zaidi makala hii ili ujue chanzo cha tatizo lako na tiba sahihi inayokufaa.

Sababu 10 zinazokufanya upate tatizo la miguu kuwaka moto​


1.Miguu kuwaka moto kwasababu ya kisukari-Diabetic Neuropathy​

Kisukari kinapokusumbua kwa mda mrefu kinapelekea mishipa midogo ya fahamu kuathirika. Mishipa inapoathirika inakwamisha pia usafirishaji wa taarifa ndani ya mwili.
Taarifa zisiposafirishwa vyema inapelekea changamoto kwenye kuhisi matukio ya ndani na nje ya mwili. Pia kisukari kinaharibu mishipa ya damu ambayo inabeba hewa safi ya oksijeni ndani ya mwili.
Mishipa ya fahamu inaweza kuathiriwa maeneo mbalimbali ya mwili. Na athari hii inaongeza endapo una
  • uzito mkubwa na kitambi
  • presha ya kupanda imeongezeka
  • unavuta sigara
  • kunywa pombe

Aina za ganzi ya kisukari​

Athari za mishipa ya fahamu kitaalamu tunaita neuropathy, lakini kuna aina za neuropathy. Aina kubwa ambayo inawatokea zaidi wagonjwa kisukari ni peripherial neuropathy.
Peripherial maana yake ni maeneo ya pembezoni, hivo ni athari ya mishipa ya fahamu iliyo kwenye viungo vya pembezoni mwa mwili. kama vidole vya miguuni na mikononi.
Dalili zingine za hii peripherial neuropathy ni pamoja na
  • kuhisi mguu na mikono kufa gani
  • kuhisi kama umevaa kitu cha kubana mfano wa sox
  • maumivu makali ya haraka na kupotea
  • kutokwa jasho jingi kupita kiasi na
  • miguu na mikono kukosa nguvu
Ni muhimu sana kumwona daktari endapo umegundua una dalili za ganzi ya kisukari. Kwenye kutibu tatizo lako utatakiwa kurekebisha kwanza kisukari ili mishipa isiendelee kuathirika zaidi.

2.Matumizi ya pombe​

Watu wanaokunywa sana pombe wapo kwenye hatari ya kuathirika mishipa ya fahamu, na hii kitaalamu inaitwa alcoholic neuropathy. Aina hii ya ganzi inaweza kusababisha maumivu kwenye unyayo na miguu kukosa nguvu.
Tiba kwa ganzi ya aina hii kuacha kwanza pombe na kubadili lishe yako kwa kula mlo kamili. Endapo utaacha pombe itapunguza athari zaidi na pia kuondoa zile dalili mbaya.

3.Upungufu wa lishe.​

Upungufu wa Vitamin B kwenye lishe yako kunaweza kupelekea upate tatizo la miguu kuwaka moto.
Kupungukiwa damu pia inatokana na upungufu wa vitamin B.
Dalili zingine za kwamba una upungufu wa damu na kupelekea ganzi ni pamoja na kukosa nguvu, uchovu, kushindwa kupumua vizuri na kizunguzungu

4.tatizo kwenye tezi ya shingo-thyroid​

Kuna changamoto mbili za tezi ya shingoni. Ni aidha tezi inafanya kazi chini ya kiwango- hypothyrpoidsm au inafanya kazi kupita kiasi-hypethyrodism. Tezi inapofanya kazi chini ya kiwango, yaweza kupelekea mishipa ya fahamu kuathirika na hivi kukufanya miguu yako iwake moto.

5.Magonjwa ya kuambukiza​

Mishipa ya fahamu inaweza kuathiriwa kutokana na magonjwa mbalimbali ya kuambukiwa, na hivo kukufanya upate ganzi kwenye miguu. Magonjwa haya ni pampja na
  • ukimwi
  • kaswende
  • mkanda wa jeshi
Kama unahisi una magonjwa haya ya kuambukiza, ongea na daktari ili aweze kukupima.

6.Fungus ya Miguu-athletes foot​

Hii ni aina ya fungus ya miguu inayoambukizwa kwa kasi sana, na inaathiri unyayo, mikono na kucha pia. Ugonjwa huu pia huitwa tinea pedis.
Dalili kubwa ya fungus kwenye miguu mi kuwasha kwenye unyayo na dali zingine ni pamoja na
  • malengelenge kwenye unyayo
  • ngozi kunyonyoka katikati ya vidole na kwenye unyayo
  • ngozi kuwa kavu pembeni ya mguu na kwenye unyayo
  • kucha kugeuka rangi kuwa yeusi na nene sana kuliko mwanzo

7.Magonjwa ya figo​

Kazi ya figo ni kuchuja mkojo na kutoa taka kupitia njia ya mkjo na jasho. Kama figo hazifanyi kazi vizuri, inapelekea sumu kujikusanya kwenye mfumo wako. Sumu zinapojikusanya zaweza kupelekea ganzi kwenye na miguu kuwaka moto.
Karibu asilimia kumi ya watu wenye magonjwa ya figo wanapata hili tatizo la kuvimba miguu kunakoambatana na kuwaka moto.
Wagonjwa wa figo waliopo kwenye huduma ya kusafisha damu yani dialysis, wanapta hii changamoto ya miguu kuwaka moto. Hii ni kwasababu wanakuwa na upungufu mkubwa wa virutubishi mwilini. Tiba ya kusafisha damu-dialysis inaondoa vitami B1 kwenye damu.
Kufeli kwa figo oia kunasababisha dalili hizi
  • kuvimba miguu
  • muwasho
  • kichwa kuuma
  • maumivu
  • joint kuwa ngumu na kujaa maji
  • kuhisi ganzi na viungo kukosa nguvu

8.Peripherial artery disease​

Artery ni mishipa inayosafirisha damu yenye hewa safi ya oksijeni mwilini. Kwahivo kama damu isipofika eneo fulani la mwili, inapelekea ganzi na hali ganzi na kuwaka moto maeneo ya miguu na vidole vya mikono.

9.Matibabu ya Chemotherapy​

Tiba hii inahusisha matumizi ya dawa zenye nguvu sana ili kuharbu seli za saratani. Chemotherapy ina madhara kiasi kwenye mwili, ikiwamo kuleta matokeo mabaya kama
  • ganzi na kuchoma kwenye miguu na mikono
  • uchovu mwingi na kukosa hamu ya kula
  • misuli kulegea na
  • maumivu

10.Kukaa kwenye mazingira yenye sumu​

Unapofanya kazi maeneo yenye kemikali nyingi, mfano viwandani au kwenye mionzi yaweza kukupelekea uathirike mishipa ya faham na hivo kupelekea miguu kuwaka moto. Pia dawa baadhi mfano za ukimwi na kifafa zaweza kupelekea athari kwenye mishipaya fahamu.

Tiba ya nyumbani itakayokupa nafuu kwa miguu kuwaka moto​

  1. Chovya miguu yako kwenye maji baridi au kwenye barafu kwa dakika chache kisha utoe
  2. Chovya miguu yako kwenye maji yenye chunvi au apple cider vinegar. Kama una kisukari muulize kwanza daktari wako kama njia hii ni sahihi
  3. Tumia chai ya manjano. Manjano ya kiambata cha curcumin ambacho kinapunguza maumivu kwenye neva
  4. Fanya masaji kwenye mguu ili kurahishisha usafirishaji wa damu. chanzo. Sababu 10 Zinazopelekea Miguu Kuwaka Moto na Tiba ya Siku 30
 
Back
Top Bottom