Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Amecheki sukari? Ana umri gani? Mpeleke hospitali aonwe na daktari haraka. Inawezekana ana allergy pia ya kitu fulani.
 
naomba mnisaidie kuna bibi yangu miguu na mikono imekufa ganzi na kifua kinambana mwenye kujua kinachosababisha anisaidie

kwa miguu na
mikono kufa ganzi ajaribu kupaka mafuta ya habasauda (black seed oil)itamsaidia.
 
Habari zenu wana jamvi, kwanza mnisamehe kwa ujumbe mrefu, imebidi niandike hivi ilie nipate kueleweka.

nahitaji msaada wenu ndugu zangu. Nina mdogo wangu wa kike wa miaka 26, tangu April mwaka huu anaumwa ugonjwa ambao mpaka sasa hatujauelewa.

Miguu inapata hali ya ganzi na kuhisi kama anaungua, hali ilikuwa mbaya kiasi cha kutoweza kulala usiku mpaka apewe dawa za usingizi.

Tukampeleka hospitali ya Mikocheni (Kairuki) wakachukua damu na mkojo wakapima vipimo vingi sana lakini ikaonekana hana tatizo wakampa dawa wakisema ana stress tu, hali haikuondoka tukampeleka mwananyamala ambako nako walichukupa vipimo vyote na halikuonekana tatizo wakamrefer muhimbili ambako aliishia kulazwa na kupewa dawa za usingizi gharama za matibabu zilitushinda, tukamtoa baada ya kuona hakuna hata nafuu kidogo, Tukampeleka kimara hospitali binafsi, dokta kapima upya hakuonekana na tatizo lolote lile akampatia dawa na kumchoma sindano mbili.Tulienda mara tatu hakuwa na nafuu yoyote ile.

Sasa tukageukia mitishamba tukapata mtu aliyetusaidia angalau kumuondolea maumivu lakini tangu July mpaka sasa anadai aina hali ya ganzi, uzito na wakati mwingine anahisi kama miguu imemwagiwa maji wakati ni mikavu. Hali hii inamtesa sana.

Ndugu zangu kuna mtu yoyote ameshawahi kuugua ugonjwa kama huu maana tumebaki kuassume ni stress ila yeye binafsi anadai hana stress za kumfanya augue hivi.

Tumejaribu maombi huku na kule ila hali ndio kama hivyo.

Je, kuna mitishamba yoyote ya kutumia angalau arudie hali yake? Natanguliza shukrani wana jamvi.
 
Mkuu mkatakona POLE,...

-je, alishawahi kucheki kisukari?
-anatumia pombe?..if yes, kiasi gani na kwa muda gani sasa?
-Ana ugonjwa mwingine wowote wa muda mrefu?
-

Kuhusu miguu:
-Inamuuma na kupata ganzi au ni ganzi tu na kuitafsiri kama miguu inamuuma?
-Ni kuanzia sehemu gani ya miguu hadi wapi(kimo)?
-Je, fahamu zipo miguuni..yaani anaweza kutambua mtu akimgusa, vitu vya moto na baridi?
-Anatembea?
 

Hapo kwenye nyekundu Sijui mlikwenda kwenye maombi gani? Kama ni maombi ya Kikristo yanayohusisha kutumia jina la Yesu, basi ushauri ni huu;

1. Unapokwenda kwa Mungu/Yesu usiende kwa kujaribu. Uponyaji hupatikana kwa njia ya imani, si kwa kujaribu.
2. Msimchanganye Yesu na waganga wa kienyeji hiyo ni sumu mbaya. Waganga wa kienyeji ni wachawi na washirikina wanafanya kazi za shetani. Epukaneni nao kabisa.

Hamtapokea uponyaji. Kumbuka mshika mbili moja humponyoka. Rudini kwa Yesu, ndiko kwenye uponyaji wa kweli; unapata uponyaji wa mwili na zaidi ya yote uponyaji wa roho.
 
Baada ya maumivu ya kuwaka moto kutoweka anaweza kutembea ingawa si umbali mrefu ila sasa anaweza kutembea angalau.
 

Mkuu asante sana kwa ushauri, ila hatujakanyaga kabisa kwa waganga wa kienyeji. Ingawa familia imegawanyika kila mtu anaamini vyake. wengine ugonjwa wa kawaida wengine wanaamini amechezewa lakini mgonjwa mwenyewe hajapelekwa kwa mganga ila tumejaribu tiba za mitishamba yaani dawa za asili kama zile za wamasai.

Tutazidi kumuomba Mungu siku zote na kumtegemea yeye bila kuchoka.
 
Nina uzoefu na watu kama wawili hivi, ila wao walipatwa na tatizo hilo baada ya kujifungua na hyo mgonjwa naye hivyohivyo.
 
Kwa imani yake/yenu fanyeni maombi dunia ina mambo.
 
pole kwanza mi ni daktari nimetaman kumuona huyo mtoto
  1. kwanza huyo ana tipical presentation za tertiary stage ya syphilis make kwenye late stage alipata deafness
  2. kwenye tertiary sasa amepata tatizo ambo syphilis ni moja wa visababishi TARBES DORSALIS ambo unasababisha haya neurological deficities kwa huyo mtoto na probably alipata congenital syphilis
  3. naomba uni PM au nieleze matatizo aliyo wai kuyapata tangia ututo wake kabla sija conclude na tukaangalia posibilities za solutions fanya ASAP
 



Mtakoma...Kabla sijaendelea zaidi naomba kwanza usome hiki kiparagraph hapa chini:

Somatoform disorder is a mental disorder characterized by physical symptoms that suggest physical illness symptoms that cannot be explained fully by a general medical condition. The symptoms that result from a somatoform disorder are due to mental factors, and are sometimes similar to those of other illnesses. May last for several years. Usually, the symptoms begin appearing during adolescence, and patients are diagnosed before the age of 30 years.

Naomba kutofautiana na Dr Kim Jong Un kwamba dada ana 'tertiary Syphilis', kufikia stage ya tertiary syphilis..lazima dada angekuwa amepitia dalili nyignine nyingine nyingi tu ambazo zingeshamsukuma kwenda kupata matibabu hospitali.

Niliposoma tu hiyo historia ya mgonjwa kitu cha kwanza ku'click' kwenye kichwa changu kilikuwa ni 'Somatoform Disorder', kwa sababu:
- Kutopata usingizi, na pia hospitali mbili walizompeleka wamehisi ana stress, mpaka akafikia kulazwa na kupewa dawa ya kumtuliza na kumsaidia usingizi
- Dalili zake haziko straight forward/specific kupelekea madaktari kumfanyia vipimo vingi (fishing) ili kugundua tatizo, hata hivyo vipimo vimeonyesha hakuna 'physical illness'

Usahuri: Dada anahitaji kumuona daktari bingwa wa magonjwa ya akili, pale Muhimbili kuna daktari amebobea kwenye matatizo hayo ya 'Somatoform Disorders' anitwa Dr Hogan, pia waweza muona Dr Phillip au Dr Kissa hapo hapo Muhimbili.

Angalizo: ugonjwa wa huo una athari ya kupelekea mgonjwa kupata 'Depression', muact mapema kabla hajaingia kwenye depression, because then she will have to deal with '2 devils' kichwani mwake, na inaweza isiwe rahisi kihivyo.
 

hajasema kaenda kwa mganga wa kienyeji kaulizia mitishamba kwani kutumia dawa za kienyeji ni dhambi?
 
yap Mkatakona unaweza kuwa right kuwa sio tertiary syphilis lakin pia nina dought na psychiatry presentation, kuna watu wanapata hiyo disorder lakini it doesnt show that much severity. Am still insisting of syphilis related disorder.

Bt ndo maana pia nimemwomba atupe brief history ya mgonjwa
 

MKUU SAMAHANI SANA kwa kuchelewa kujibu, niwie radhi kwa hilo lilikuwa nje ya uwezo wangu ndugu yangu. Kusema kweli binti hana historia ya kuugua ugua chochote cha ajabu wala ugonjwa wa aina yoyote.

isipokuwa alipokuwa na miaka 14 akiwa kidato cha pili alianza tu kuhisi kuwa hasikii vema yaani speech inakuwa inapotea anasikia mtu anaongea ila hapati maneno vizuri. Tulianza dispensari ya Prof. fulani wa ENT (Ear,Nose, Throat) akampa rundo la vitamini complex lakini hali ikazidi kuwa mbaya hususai darasani ndio tukampeleka Muhimbili ambako alianza clinic Mhimbili kitengo cha ENT.

Mwaka juzi tuliomba refer Kenyatta Hosp. ya Kenya ambako walihitimisha kuwa hawaoni chanzo cha tatizo na pia inaonekana hearing aids zilizopo hazimsaidii hivyo communication yake iwe lip reading na njia nyingine ya kumfanya aweze kuwasiliana.

Amaeishi na tatizo hilo kawaida kabisa bila kuugua chochote kile zaidi ya huo ulemavu wa kutokusikia vizuri (hard of hearing) na sio KIZIWI (Deaf) mpaka mwaka huu alipoanza kusikia ganzi vidole vya miguuni na kudevelop hadi magotini.

Tumepima mkojo na damu kucheck magonjwa ambayo madaktari walikuwa wanayahisi kama kisukari ikaonekana hakuna kituHosptali ya mwisho ya kimara kuna dokta mmoja wa wanawake ambaye naye alitumia vipimo vyake akasema haoni kitu chochote kile ndio tukaamua kugeukia dawa za asili ambazo angalau zilimuondolea maumivu ya kuwaka moto ila tatizo la ganzi, kuhisi uzito na hali ya kuhisi miguu imelowa ndio inayomtesa sasa hivi.
 

Mkuu asante sana kwa maelezo yako. Nashukuru sana ndugu yangu naanza kuhisi ni kweli anaweza kuwa na tatizo hili ana linaloelekea na hili.

Amejitahidi kusoma mpaka chuo kikuu tena ufahulu licha ya kuw ana ulemavu huu ambao naona kama watu wanauchanganya na uziwi. lakini pamoja na kutafuta kazi sana mara kadhaa wameacha na wengine wamempa jibu la wazi kuwa kutokana na hali yake hawezi kumudu nafasi anayoomba.

Ile hali ya watu kumshangaa wakati wa interview nakadhalika na kule kukosa nafasi za kazi kama vijana wenzake aliohitimu nao nahisi inaweza pelekea akate tamaa ya maisha au kujiona hafai katika jamii.

Sasa tukiongeza na hali yake ya ulemavu nadhani kwa asilimia kubwa inaweza kuwa chanzo cha hili tatizo. Asante mkuu nitaongea na familia tufikirie kumtafutia hao madaktari. Nashukuru sana Mkuu
 
Wadau habari za leo. Naomba msaada wa maelezo kwa anaejua sababu, na ufumbuzi wa tatizo la ganzi katika baadhi ya viungo mwili.

Kwa kifupi takribani miezi minne hivi sasa miguu yangu (kuanzia maeneo ya enka kuelekea nyayoni na vidoleni), maeneo ya viganja vya mikononi, na mdomoni (lips na ulimi) yamekuwa na tatizo la ganzi ambayo sioni dalili kama itaisha.

Pamoja na ganzi pia huwa nahisi miguu kuwa na joto kali, hasa nyakati za usiku ninapokuwa nimelala. Naomba anayejua tiba anipe maelekezo. Nina umri wa miaka 45.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…